Wakati mwaliko wa waandishi wa habari kwa ajili ya Press Conf ya Kikwete leo Anatoglou, Ilala Dar es Salaam unatolewa kwa waandishi waliokuwa naye kwenye kampeni tu, waandishi hao sasa wanaandaa pati kubwa ya kusherehekea ushindi wa CCM.
Anayesambaza mialiko hiyo ni Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima (Gazeti la Mbowe), mwanamke mwenzangu Irene Mark, ambaye naye pia ni mmoja wa waandaaji wa sherehe hiyo ya waandishi kusherehekea ushindi. Irene ndiye aling'ang'aniwa na Ikulu kwenda kwenye hizo kampeni kuanzia mwanzo hadi mwisho hata alipokwenda MWandishi mwingine Tamali Vulu, alirudishwa na kuendelea Irene.
Hii ni aibu tupu na nadhani afadhali ya Manyerere Jacton wa Mtanzania (gazeti la Rostam) ambaye alikataa kuvalishwa koto la 'Kikwete Press 2010" akisema iko siku waandishi wanaume watavalishwa sketi.
Maadili ya uandishi wa habari vipi?