Elections 2010 Kikwete Live on Power Breakfast (Clouds FM)

Elections 2010 Kikwete Live on Power Breakfast (Clouds FM)

Ulitarajia Clouds waulize nini1 Subiri leo jion uone Tifa hili lilipofikiswha na ukosefu wa maadili ,lakini mapambono yanaendelea .......,mapambazuko yanakuja CCM ni nyumba imara iliyojengwa juu ya mchanga .....it is a matter of time .....
 
ngoja akutane na mama mwakitwange....atazimia huyu.....

A a a! yule mama hatufai kabsaaa, alikuwa anazuia maswali ya msingi sana kwa Dr. Slaa, nafuu Dr. alimpuuza akawajibu, sasa Jeykey akimskiliza asipowajibu-si hatojibu swali hata moja?
 
Hivi Mkuu tukiacha kukumbatia imani za kichama ...be fair wewe ungekuwa rais kwa miaka mitano iliyopita, ukaulizwa maswali alopewa kikwete ungetoa majibu kama alotoa huyo raisi wetu, hana coherent ni kama hajui nini watanzania tunahitaji. Amejaa uongo kwenda mbele.

Tunahitaji watu makini kutufikisha tunapotaka kufika si huu usanii ndugu.

Fairness ni pamoja na kuwapa wengine nafasi ya kupata taarifa za ukweli na sio kuvuruga.

Jana walivuruga hotuba ya prof. Lipumba na leo wamekuja na matusi yao hayo hayo kuvuruga watu wengine wasipate taarifa za ukweli juu ya nini kaongea JK, sasa hapo fairness iko wapi

Tuwasikilize wagombea na baada ya hapo ndio tujadiliane. Lakini kujaribu kuandika matusi ili wengine wasipate kusikilizwa hiyo sio demokrasia.

Kama unaona mgombea hafai, basi kagombee wewe na kamshinde kwenye kisanduku cha kura na wala sio kwenye matusi. Au nenda kamchague mgombea wako, hiyo ndiyo demokrasia.
 
Fairness ni pamoja na kuwapa wengine nafasi ya kupata taarifa za ukweli na sio kuvuruga.

Jana walivuruga hotuba ya prof. Lipumba na leo wamekuja na matusi yao hayo hayo kuvuruga watu wengine wasipate taarifa za ukweli juu ya nini kaongea JK, sasa hapo fairness iko wapi

Tuwasikilize wagombea na baada ya hapo ndio tujadiliane. Lakini kujaribu kuandika matusi ili wengine wasipate kusikilizwa hiyo sio demokrasia.

Kama unaona mgombea hafai, basi kagombee wewe na kamshinde kwenye kisanduku cha kura na wala sio kwenye matusi. Au nenda kamchague mgombea wako, hiyo ndiyo demokrasia.

Ni kweli watu wanaharibu kwa sababu zao kwa matusi, hatuwezi kuwazuia ndo siasa za kuvumiliana. Lakini mkuu hujanijibu swali langu la msingi! usiweke jaziba hata kidogo. "wewe ungekuwa rais kwa miaka mitano iliyopita, ukaulizwa maswali alopewa kikwete ungetoa majibu kama alotoa huyo raisi wetu?"
 
Jamani punguzeni hasira, muoneeni huruma sasa

IQ ndogo ni ulemavu, tusimcheke Bali tupange mikakati ya kusaidia wanaye wasije wakarithi huo ulemavu
 
Nimesikiliza katoa ujumbe mzuri tu uchaguzi wa haki na uhuru ndio anachokitegemea....uchaguzi mwema jumapili jamani msikae kwenye forum mkajisahaau kwenda kituoni..

Hivi Clouds FM inasikika mpaka Arusha??
 
Yaani JK utafikiri alikuwa nahojiwa kwa kijerumani, lugha asiyoifahamu!
 
ilishindikana jamani maana alifika tu clouds pale akaanguka!! kina hando wamepepeaje
 
Wakuu,

Mdahalo wa JK kupitia Clounds umemmaliza badala ya kumjenga! Anapiga porojo, uelewa mdogo, vicheko visivyo na msingi, anazungukazungukaa wee hajibu swali. Anaulizwa maswali mazuri sana ambayo kama angekuwa mtu mwenye uwezo na upeo angejibu kwa umahiri kabisa na angegeuza mtazamo uliopo sasa hivi kwamba uwezo wake wa akili ni mdodo na hana uwezo wa kuleta mabadiliko.

Kwa maoni yangu, hii ina maana watu ambao wamemsikiliza hata kama bado walikuwa na imani naye basi amewakatisha tamaa. Ameshindwa kuonesha uwezo wake wa kuelewa mambo, kujibu maswali, na kukabiliana na changamoto tulizo nazo sasa hivi. Amethibitisha kwamba yeye hana uwezo wa kutuongoza.

hii tisa kumi ni leo sa mbili atakapokuwa kwenye mahojiano live kwenye TV inaonekana anatapatapa na kumuiga Dr. Slaa kila anachofanya ila mi nadhani kama wakiiba kura na kushinda watakuwa wamekiona cha moto na watatekeleza nbaadhi ya sera za CHADEMA...
 
acheni unafiki, kwenye ukweli semeni na kwenye propaganda zenu semeni, kila mtu amesikiliza mahojiano yale..hata kama mtu hamumpendi basi msionyeshe udhaifu wenu na chuki zenu, narudia kila mtu amemsikiliza na amemuelewa

acha crap wewe mwenye craps za kifisadi
 
lakini hawa watu wanashangaza, si walisharudia mara zote kwamba wao hawahitaji kuongea kupitia vyombo vya habari badala yake wanakwenda moja kwa moja kwa wapiga kura? sasa hii abrupt change of strategy ni kwa ajili ya nini? Hebu tuhabarisheni je Kubenea, Kibanda, Johbson Mbwambo, Jesse Kwayu, Msaki, Makunga wameshapewa mualiko maana mpaka jana waliambiwa tu na wapambe wa mchakato huo kwamba majina yao yamo lakini walikua hawajapata kadi. Habari za kuaminika ni kwamba hata vyombo vya nje vilivyoomba kualikwa vilijibwa kwamba wanaweza kwenda tu kama watafunga mabakuli yao na kukubali kutouliza maswali yoyote. Makubwa hayo.............
 
Is Kikwete serious? Kuhusu swala la ajira la vijana - anaelezea ajira za glosari. Anasema tuongeze vijana wanaofungua vizibo vya soda. Inatisha kwanini rais wa nchi anaongelea ajira za aina hii kama ndio model.
 
Mimi nawambieni JK hafai hata kidogo.

Stammering za leo zimenua, anarudia rudia maneno, no cohesion katika majibu yake. RIP JK, achia wenye uwezo!!!:tape:
 
Hehe, eti Kikwete anafafanua nini maana ya kauli "Vijana ni hatima ya Taifa"

Nimecheka kweli, hivi kuna mtu hajui maana ya hii kauli, hadi nyimbo tuliimbishwa utotoni kuhusu vijana kuwa taifa la kesho?

Ila wakuu haya maswali kwa mheshimiwa siyo marahisi kama tunavyoyaona sisi (si unajua tunatofautiana uwezo wa kujenga hoja), lazima alikuwa anatokwa jasho!

God Bless everybody...
 
Back
Top Bottom