Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ngoja akutane na mama mwakitwange....atazimia huyu.....
Hivi Mkuu tukiacha kukumbatia imani za kichama ...be fair wewe ungekuwa rais kwa miaka mitano iliyopita, ukaulizwa maswali alopewa kikwete ungetoa majibu kama alotoa huyo raisi wetu, hana coherent ni kama hajui nini watanzania tunahitaji. Amejaa uongo kwenda mbele.
Tunahitaji watu makini kutufikisha tunapotaka kufika si huu usanii ndugu.
Kila anachofanya Rais Dr Slaa lazima na Kikwete aige?
Fairness ni pamoja na kuwapa wengine nafasi ya kupata taarifa za ukweli na sio kuvuruga.
Jana walivuruga hotuba ya prof. Lipumba na leo wamekuja na matusi yao hayo hayo kuvuruga watu wengine wasipate taarifa za ukweli juu ya nini kaongea JK, sasa hapo fairness iko wapi
Tuwasikilize wagombea na baada ya hapo ndio tujadiliane. Lakini kujaribu kuandika matusi ili wengine wasipate kusikilizwa hiyo sio demokrasia.
Kama unaona mgombea hafai, basi kagombee wewe na kamshinde kwenye kisanduku cha kura na wala sio kwenye matusi. Au nenda kamchague mgombea wako, hiyo ndiyo demokrasia.
Nimesikiliza katoa ujumbe mzuri tu uchaguzi wa haki na uhuru ndio anachokitegemea....uchaguzi mwema jumapili jamani msikae kwenye forum mkajisahaau kwenda kituoni..
Wakuu,
Mdahalo wa JK kupitia Clounds umemmaliza badala ya kumjenga! Anapiga porojo, uelewa mdogo, vicheko visivyo na msingi, anazungukazungukaa wee hajibu swali. Anaulizwa maswali mazuri sana ambayo kama angekuwa mtu mwenye uwezo na upeo angejibu kwa umahiri kabisa na angegeuza mtazamo uliopo sasa hivi kwamba uwezo wake wa akili ni mdodo na hana uwezo wa kuleta mabadiliko.
Kwa maoni yangu, hii ina maana watu ambao wamemsikiliza hata kama bado walikuwa na imani naye basi amewakatisha tamaa. Ameshindwa kuonesha uwezo wake wa kuelewa mambo, kujibu maswali, na kukabiliana na changamoto tulizo nazo sasa hivi. Amethibitisha kwamba yeye hana uwezo wa kutuongoza.
acheni unafiki, kwenye ukweli semeni na kwenye propaganda zenu semeni, kila mtu amesikiliza mahojiano yale..hata kama mtu hamumpendi basi msionyeshe udhaifu wenu na chuki zenu, narudia kila mtu amemsikiliza na amemuelewa