Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

Hii kuikimbia haijaa kaa sawa kwa mujibu wa ratiba si ilikuwa leo aondoke tu leo? sasa hii sensationalization kuwa jk "kuikimbia" ndio ushabiki mwenyewe huu.

Lakini mkuu si alitakiwa ahutubie kwa kufanya hitimisho leo au majuumuisho ya safari yake?
Sasa kwa nini kaondoka bila kufanya hivyo anakimbilia wapi?anakimbilia kwenye kahawa?Au ndo anapaa usa?
 
*Kamanda wa Polisi azungumza
*Msako zaidi waendelea kijijini

Na Charles Mwakipesile, Mbeya

SIKU mbili baada ya msafara wa Rais Jakaya Kikwete kushambuliwa kwa mawe na watu wasiojulikana na wanausalama kumwagwa kwenye kijiji cha Kanga wilayani Chunya, watu zaidi ya 60 wamekamatwa na Polisi Mkoa wakihusishwa na tukio hilo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini.

Habari za kiuchunguzi za Majira zilizopatikana jana na baadaye kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Bw. Zelothe Stephen, zilisema msako mkali wa Polisi unaendelea, huku watu wengi wakiwa wamekamatwa, hakutaka kutaja idadi kamili.

Kamanda Stephen alikiri kuwepo tukio la watu kukamatwa lakini alisema asingeweza kwa sasa kutaja idadi kamili ya waliokamatwa, kwani ni mapema mno.

Jumatano iliyopita, watu wasiojulikana waliyatupia mawe magari ya viongozi waliofuatana na Rais katika ziara yake mkoani hapa, kutokana na hasira ya kutopata fursa ya kuzungumza na Rais na kumpa kero zao.

Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Kanga Mkwajuni, baada ya wananchi hao kusubiri kuanzia asubuhi kwa matarajio kuwa Rais angesimama na kuzungumza nao, lakini ilipofika saa 1.30 usiku msafara huo ulipita bila kusimama na ndipo watu hao wakachukua hatua hiyo.

Katika toleo lake la jana gazeti hili liliripoti kuwa siri kuu iliyowafanya wanachi hao kufikia hatua hiyo ni kutokana na kukerwa baada ya kuona wameshindwa kutoa kero zao kwa Rais baada ya kumsubiri kwa muda mrefu.

Baadaye, taarifa za Jeshi la Polisi zilithibitisha wanausalama kupelekwa kijijini hapo wakiwemo askari kanzu, ili kuchunguza na kujua kiini cha tatizo ikiwa ni pamoja na kukamata wahusika.

Jana Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa Rais alisikitishwa na tukio hilo.
 
CCM mbeya ni issue kuuza sera zake,na kama wana busara hawa CCM they need to work on that bse watu wamechoka na kukerwa na siasa za kisanii za JK na uongozi wake.
Wakati wa ukombozi ni sasa Mbeya Keep it up just like Tarime
 
Mbeya wana Rais wao.Nashangaa kwanini Jk alikuwa hajua kipindi chote hiki!
 
Ana mwaliko wa kutembelea Brazil. Halafu atapitia tena Marekani.
Habari ndiyo hiyooo!

Huko kutakua na ahueni kwake,angalao hatakua na wasiwasi wa kutunguliwa mawe.Lakini akumbuke hata huko kuna wabongo wenye usongo nae.

Sijui akija Marekani Mwafrika wa kike na Mwanakijiji hawatarusha hata changarawe? Kwi kwi kwi!
 
Kama kweli anakimbia ataishia wapi?

Lakini huo ni mwanzo mzuri. Alimwambia Mbowe kuwa aachwe aruke ruke na helikopta akitu yeye (JK) atakuwa tayari yuko Magogoni (Ikulu). Sasa kama naye ameanza kuruka ruka na kimbia akitu sijui atakuta nini pale Ikulu.........??? Sisi yetu macho.
 
...wakuu ni kweli kwa mujibu wa ratiba...leo muhashimiiwa rais ana mkutano mkubwa wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake mbeya ......kabla ya kuagana na viongozi na wazee wa mbeya na kurejea dar es salaama

hata wale vijana wa mwanjelwa waliomsimamisha aliwaagiza waandike madai yao na kuwakilisha ili ayajibu kwenye mkutano wa leo.....

..sio rahisi akfuta mkutano wa sokoine ...maana ndio ziara yenyewe...ni kama aende mwanza akakimbia ccm kirumba ...au taborra ali hassa mwinyi stadium
 
rais amefuta mikutano ya sokoine, mwanjelwa, na jana alishindwakuhutubia rujewa mjini, jukwaa likahamishwa usiku usiku hadi madibira km 80 toka rujewa, ninavyoandika hapa ndo keshapaa nusu saa iliyopita kuelekea dalisalama!

ziara yake jana ilingia mushkeli. baada ya gari aliyopan
 
goari aliyopanda mkewew ilpata tyre burst eneo hilo la mwanjelwa, na kwa jasiri wa dereva tu leo tungesikia mengine, however, aliwahi kuhamishiwa kwenye gari ingine salama.

wakazi wa mbeya wanaianza week end saa, hizi baada ya kuzingirwa na FFU waliobeba silaha, misafara kusubiri ipite hadi masaa 2.

pengine itakuwa ziara ngumu sana kwa kikwete, na ziara ilyowakera sana wakazi wa mbeya, ambao kwa kawaida ni wakarimu kwa wageni kuliko wahabeshi wa ethiopia
 
Nina hakika hakuwakimbia wakazi wa Mbeya, anakimbia kivuli chake na kama ni hivyo ana mbio ndefu !!!!
 
Atafanyaje kampeni 2010? au ndio anathibitisha ni rais wa kipindi kimoja? au 2010 polisi, jeshi FBI na CIA, vitamlinda?

waberoya
 
Hivi wale jamaa waliokamatwa kwa kumzomea fisadi Mkapa walishaachiwa huru?
 
wanausalama wanadai eti kafuta mikutano yake, kwa kuwa anawahi fund raising ya albino association!
 
wanausalama wanadai eti kafuta mikutano yake, kwa kuwa anawahi fund raising ya albino association!

....kwani ratiba ya rais si inapangwa miezi kabla???..afteral safari ya dar mbeya kwa gulfstream haifiki masaa mawili...inakuwaje mikutano ya tangu asubuhi ifutwe??
 
....kwani ratiba ya rais si inapangwa miezi kabla???..afteral safari ya dar mbeya kwa gulfstream haifiki masaa mawili...inakuwaje mikutano ya tangu asubuhi ifutwe??
Ratiba ya siku hizi ni ad hoc. Si umeona juzi amefupisha ziara kwenda Tanga sherehe za mwenge na kurudi kuendelea na safari?
 
....kwani ratiba ya rais si inapangwa miezi kabla???..afteral safari ya dar mbeya kwa gulfstream haifiki masaa mawili...inakuwaje mikutano ya tangu asubuhi ifutwe??

Mwanangu inafikia mahali hata fundo la mate kumeza inakuwa tabu, japokuwa ni ya kwako mwenyewe.

Hiki kitendo kimemhuzunisha na kumfadhaisha sana JK, mzee wa ushindi wa kishindo ambacho leo wananchi wameu "Reciprocate". Japokuwa kitendo walichomfanyia sio cha kiungwana, lakini nadhani Wananchi walifikia uamuzi huo baada ya kuchoka na mengi nae kuonekana kama asiye elewa nini kiunaendelea TZ. Kama alivyosema Maalim, nchi imevimba na rais anatakiwa awe anaufahamu ukweli na sio kuzungukwa na watu wa kumdanganya tu kama alivyo sema Salva kuwa mapenzi ya wananchi kwa rais yanaongezeka kutokana na uchapaji wa kazi uliotukuka. Huo, utendaji, mie sijui, ila kwa hali hii, SIJUI mwishowe itakuwa kitu gani.

Hao washauri wake wamgeukie tu wampe ukweli kuwa yeye ni mzee wa singlllllllllllllle term. Ingekuwa marekani wangemu 'impeach'
 
Back
Top Bottom