Kikwete: Mkutano wa Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) utafanyika Afrika kwa mara ya kwanza

Kikwete: Mkutano wa Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) utafanyika Afrika kwa mara ya kwanza

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rais Mstaafu awamu ya nne, Jakaya Kikwete, amesema anajivunia kuwa Mwafrika wa kwanza kuongoza bodi ya wakurugenzi ya taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), ambalo liilianzishwa miaka 20 iliyopita.

Kikwete ambaye ameanza kuongoza bodi hiyo mwaka 2021 amesema baada ya kumaliza muda wake wa uongozi wa nchi, alipigiwa simu na mtu akiambiwa kwamba ameonekana anafaa kuwa katika nafasi hiyo.

Akizungumza leo wakati wa hafla ya kutambua mchango wa wadau kwenye sekta ya elimu, Kikwete amesema hata yeye hafahamu kwanini alichaguliwa katika nafasi hiyo.

“Hili shirika sio jipya lilianza miaka 20 iliyopita, lakini bodi yake haijawahi kuongozwa na mwafrika, mimi ndiye wa kwanza na sijui ilikuwaje wakaona nafaa. Nilipigiwa simu na mtu mkubwa huko duniani kuniambia kuhusu hilo nikasema sawa,” amesema na kuongeza;

“Vikao vya bodi ya GPE, havijawahi kufanyika Afrika au katika mataifa ya kati, ni Paris, Ujerumani, Marekani, Uingereza lakini mwaka huu nimeomba na wamenikubalia mkutano utafanyika Zanzibar Tanzania,” amesema Kikwete.

Amesema kuaminiwa kwa mwafrika mwingine katika nafasi hiyo kutategemea na yeye atakavyofanya vizuri kwenye uongozi na anajitahidi kufanya kazi yake vyema.

Shirika hilo kwa sasa linasaidia nchi 88 duniani kwa kutoa fedha kuwezesha sekta ya elimu, lengo likiwa ni kuhakikisha hakuna mtoto anakosa haki ya kupata elimu.
 
Ngoja wajuvi waje

Watoe mafanikio ya hiyo gpee

Kwa hapa bongoland

Ova
 
Duh kachaguliwa alafu hajuwi kwanini kachaguliwa ,aise

Jk Ana mazali sana

Ova
 
Back
Top Bottom