1. Nyuso nyingi za huzuni kwa waliohudhuria
2. Wauliza maswali ni wanachama wa CCM tu (wamechujwa)
3. Ushangiliaji wa kinafiki (makofi ya kujilazisha
4. Hakuna mlalahoi aliyehudhuria
5. Ni kama alikuwa anaongea na Kamati Kuu ya CCM maana ndio waliojaa mule ndani (Makamba, Kinana, Bilali, Kingunge, Januari, Tido Mhando, Kusaga, Abdulazizi (Ag. RC Dar), Paul Rupia, Idd Simba, Mwantum Mahiza, Hadija Kopa, Abasi Mtemvu,
6. Wauliza maswali walipangwa (walikuwa wanajulikana) na huenda majibu yalitayarishwa
Asha Mtwangi: Unaonaje muelekeo wa kampeni? (stupid question)
Suzana Mongi (TBC): Watuhumiwa kuwanadi kama watu safi? Jibu: Bado ni watuhuniwa tu hata ndani ya CCM tulishajadiri hili, ila wakihukumiwa na mahakama tutawaondoa madarakani.
Reifred Masako (ITV): Kilimo ulifanya nini katika miaka 5 iliyopita?
Flora Malya (Star Tv): Wizi wa kura alikiri kuwa tume inaweza kukosea kujumlisha kura mfano badala ya kuandika 2,120 tume wakaandika 1120.
David Ramadhani (Channel 10) Kuendeleza elimu una mpango gani? Hakutoa jibu la mkakati, anaongea kupata wahisani.
Hamisi Dambaya (Mlimani TV): Tafiti za kura za maoni, unazungumzia nini? Akajibu wanatuonea
Modesta Mahiga (EA Tv): Ajira kwa vijana ungependa watanzania wajue mafanikio na hatua mlizozichukua miaka 5 iliyopita na baadae
Ephraim Kibonde (Clouds tv): Tupe sura ya serikali utakayoiunda na kipi umekiandaa cha kutupeleka 2015. Akajibu, kutakuwa na sura mpya za wizara (https://jamii.app/JFUserGuide this is obvious), akasema zaidi ya hapo niseme nini?
Festus Kijo (ATN): Utapenda watanzania wakukumbuke kwa lipi (legacy) baada ya 2015? Akajibu: Tulizani helikopta ina unafuu kwenye kampeni, shughuli ya kampeni haifanyiki kila mwaka na hufanyika mara mbili katika maisha yako. Nataka watanzania wanikumbuke niliwakuta hapa na nimewapeleka pale (vigezo hakuvitoa)
Martin Kuhanga (Tv Tumaini): Vitambulisho vya uraia, hilo limekwama wapi? Akajibu: Ahadi ya vitambulisho ni ya Nyerere, Bomani alikuwa Artoney General alishindwa, Mwinyi kashindwa, Mkapa kashindwa, mimi mwenyewe (JK) hola. Watu wachache wanaamua nje ya mfumo wazi. Majibu yalijaa kigugumizi kingi. Kaahidi miaka miwili ijayo mpaka 2012 vitambulisho tayari. Kuna mgongano wa kimaslahi ambao tunaushughulikia.
Asha Mtwangi: Hatua zipi zimechukuliwa baada ya tume ya madini? Mimi mkwere natoka Chalinze ila tumeongeza mrahaba sio ni mrabaha hawa wanatuchanganya.
Susan Mongi (TBC): Secta ya afya, viongozi wanatibiwa nje kwa fedha nyingi (hata uzito mnaenda kupima nje?). Akajibu: Sio viongozi peke yao wanaokwenda huko wapo watu wengine pia. Mtoto wangu anafundisha pale Muhimbili alisaidia kuniletea mahitaji yao na Prof. nikawasaidia, kwa hiyo matibabu ya kinywa yapo hapa hapa. Nilimkaribisha Prof Roger kuja kutembea na kutibu pale MOI. Prof. Kinasha ameshastaafu lazima tupeleke watu nje ama watakufa.
Reifraid Masako (ITV): Muungano muelekeo ni nini? Jibu: Kuna vyombo vya kushughulikia muungano na havifanywi kama inavyotakiwa. Kamati ile ikutane mara kwa mara. Maswala mengi majawabu tayari bado swala moja tu la mafuta.
Flora Malya (Star tv): Ahadi nyingi sana, je ahadi hizi zitatekelezwa vipi. Jibu: Ahadi zipo kwenye ilani. Zipo ahadi za papo kwa papo ndio nyingi nimezibeba mimi mtihani mkubwa sana huu. (jibu ni pumba tu). Mapesa alinisifia sana jimboni kwake.
David Ramadhani (Channel 10): Rushwa unaahidi nini kulishughulikia? Jibu: Mimi ni mmoja nachukua rushwa (sura inamsuta) sheria tumetunga tayari. TAKUKURU ipo kila wilaya na fedha tumewaongezea.
Hamisi Dambaya (Mlimani tv): Haki mahakamani una mikakati gani? (JK kigugumizi kidogo). Tunaboresha bajeti za mahakama, tunaahidi kuleta usasa katika mahakama iwe kama "hansadi" za bungeni, tumeongeza majaji hili la maadili hilo ni la kwao mahamaka yenyewe.