Elections 2010 Kikwete on ITV, maswali na majibu toka kwake

Elections 2010 Kikwete on ITV, maswali na majibu toka kwake

Naona Maswali ni Yale yale aliyokuwa anaulizwa Asubuhi, Hi Story ya Meatu na Daraja si aliipiga asbh kama ilivyo? Ngoja nikalale miye
 
tanesco arusha wazalendo wa kweli. Wamekata umeme safi saaaaaaaaaaaaaaaaaaana!
 
ahadi tamu, nzuri na zakupendeza. Mimi nimezipenda... Hivi kweli huyu ni mwandishi wa habari kweli au msoma matangazo?
 
tuchagueni tutajenga. change the sentence into negative
 
Amekiri hana imani kabisa na watendaji wake,kila kitu akaunti yake mikopo kwa wanafunzi,nyumba za walimu ili pesa zisitumike hovyo!alipwe contractor.sasa sijui kama kweli huyu bwana ataweza kupambana na ufisadi
 
Maskini wee jamaa yangu hapa kaanza kutapika na kulia, nimemshauri akalale!!! naona jamaa kajipigisha makofi lakini hamna kitu, kau-neutralize ule mgomo wa watu waliomgomea kwa kutaka wajengewe daraja!!!AIBU
 
Sijasikia Mwanahalisi, Raia Mwema wala Tanzania Daima
 
huu mdahalo sijui ni press conference ni uozo mtupu. hakuna challenge yoyote ile jamaa anaongea tuuuu, waandishi hata kumkatiza wanamwangalia tuuu, dah kweli huu ni upumbavu mtupu
 
akili hizi ndio anguko la upinzani nchini, hizi ndio issue mnazoweza ku discuss kwenye draft

Tunaongelea mstakabali wataifa toa ukoko kichwani mwako ukitegemea kwamba sisi wote ni wapinzani nyakati za ujinga na upofu zilishapita tutaongea chochote tunachotaka nchi yetu wote sio ya mama yako
 
ahadi tamu, nzuri na zakupendeza. Mimi nimezipenda... Hivi kweli huyu ni mwandishi wa habari kweli au msoma matangazo?
Kuna waandishi wa habari na waandishi wa taarifa, natumai yeye ni mwandika taarifa.
 
"naamini kwamba mengi ya haya tuliyoyaahidi tutayatekeleza"-JK
du kumbe sio yote yatakayotekelezwa
 
Siku ile ya tarehe 5.5.2010 akiwa mbele ya wazee wa Dar,JK huku akiwaita wafanyakazai mbayuwayu alitamba akisema ''Mimi ndiye mwajiri wa wafanyakazi,hivyo atakayegoma nitamfukuza kazi'' Mpendwa mfanyakazi nasi wakati wa kutamba umefika,31.10.2010 kwa nguvu zote mbele ya karatasi ya kupigia kura nenda kasitishe ajira yake,mwajiri Dr SLAA ambaye atajali maslahi yako.Tuma ujumbe huu kwa wafanyakazi wote unaowafahamu,okoa taifa lako.Inawezekana!
 
Back
Top Bottom