Kikwete siyo safi! - yes I said it!

I know.. Watanzania hatuna kumbukumbu nzuri mambo mengine ni kama time warp continuum..

Hapo umesema kweli Mzee Mkjj. Lazima watz tutunze kumbukumbu za viongozi wetu ili tusije tukazugwa na clash of personalities tukaamini kuwa ni clash of policies. Maana wote wanafanana kwenye policies za kutuibia
 
yote niliyoyasema ni kweli tupu! wao wanajua na wanajua ninajua.. na wapo watu wengine ambao wanajua.. Lowassa anasema "waligongana kwa bahati mbaya na Karamagi pale Hotelini"...


sasa hapa Mnaongela issue kwani siku za nyuma mlikuwa na kasumba mlizopandikizwa na viongozi hao hao mnao waongelea hii leo naimani kwa msaada wa Jf itawazinduwa wa TZ wengi na kuelewa ukweli ndani ya serekali yetu na chama chake wakati wa mabadiliko umefika
 
Adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu ni Jakaya Kikwete kwasababu ni mnafiki na hawatendei haki watanzania kwa kuwalinda watu wanaohujumu uhuru na uchumi wa nchi yao; kwakufanya hivyo amepoteza amani iliyokuwainatawala nchi hii na ndio maana watuwanauawa hovyo, watu wanajifungia kwenye nyumba zao kama wako jela, zote hizi zikiwa ishara ya nchi iliyokosa amani; lakini Jakaya na chama chake ishara zote hizi za utovu wa amani kwao wao ni 'AMANI". Ni vyema kwa wazee wenye hekima na wanaharakati wakawa mstari wa mbele na kuuambia umma wa Tanzania kuwa nchi yetu inakwenda kubaya; haya mauaji ya albino ni ishara tosha kuwa utawala wa nchi yetu umeshindwa kuthibiti umaskini na ndio maana watu wamerudia mambo ya kuamini ushirikina kama short-cut ya kutatua matatizo yao badala ya kufanya kazi kwa bidii!!
 
Last edited:
Nashukuru Mungu sana Kikwete ni Muungwana sana kwenye Uhuru wa habari, maana sipati picha kipindi cha zama za uwazi na ukweli sijui kama tuneongea hivi. Kila la Kheri Tanzania maana nahisi tunaelekea kwenye demokrasia ya kweli
 
Nashukuru Mungu sana Kikwete ni Muungwana sana kwenye Uhuru wa habari, maana sipati picha kipindi cha zama za uwazi na ukweli sijui kama tuneongea hivi. Kila la Kheri Tanzania maana nahisi tunaelekea kwenye demokrasia ya kweli

Tulipo sasa ni ngumu kutuzuia kama ni mbuzi tunasema ashakata kamba,maana wanajua fika wakitaka tu kutuzuia, msemo wa kisasa wanasema "itakula kwao..!" mapambano nayaendelee...
 
Nakushukuru tena na tena Mzee Mwanakijiji.
Kwa haya uliyoyasema kuhusu Mkulu, mimi nakuaminia. Ila narudia msimamo wangu niliowahi kuutoa huko nyuma kuwa ingawa Mkulu ni Graduate wa UDSM, IQ yake ni ndogo. Naamini Degree yake ni PASS ya chini kabisa ndio maana hajaweza kufanya Masters yoyote. Kama ni mambo ya IQ, msimlaumu. Mnategemea nini kwa mtu wa namna hii.
Hakuna ubishi jamaa ni HB, hivyo anapendwa na watu. Wengi hatukuyajua hayo mpaka aliposhika usukani na kuona jinsi anavyoyumbisha chombo.
Wana JF naomba msinielewe vibaya, mambo ya IQ ni IQ tuu haya uhusiano na degree ya UDSM. Kuna watu wameishia STD 7 tuu lakini wana IQ kubwa na kuna Magraduate wa Chuo wana IQ ndogo.
Kama kuna aliyesoma na Mkulu, atujulishe alitoka UD na GPA gani.
 
sisi kule kwetu kijiweni, sku zile vyama vingi vinaanza walitwambia "msiwafuate hao wanataka kumrejesha sultani" watu walitiwa hofu za kijinga na wajanja wanaendelea kufisidi nchi yetu hadi leo, huku bara wenzetu si haba mmezugwa, mmekuwa ndondocha kwa kauli za baba wa taifa za karne ya 20,tokea mfumo wa chama kimoja kuwa "rais bora atatoka CCM, bila CCM imara nchi yetu itayumba" nyimbo hizi mkiimbiwa tu wenzetu hamna tena blah blah kama hizi za nani fisadi nani mwizi.Yaani afadhali CCM itawale maisha japo ni genge la wezi na majambazi, lakini WOSIA WA BABA WA TAIFA UDUMISHWE HATA VIPI IWAVYO. shauri yenu
 
WANAJAMII,NAWASALIMU NA PIA NAWASHUKURU NAMI KUPATA NAFASI YA KUWEZA KUCHANGIA JUU YA MAMBO MUHIMU YANAYOUSU MAENDELEO YA JAMII YETU NA DUNIA NZIMA KWA UJUMLA,KIJAMII,KISIASA,UCHUMI,SAYANSI,DINI NA UTAMADUNI KWA UJUMLA
Sasa umefika wakati wa sisi kubadilika na kubadilisha mitizamo yetu,Ukiangalia mwenendo mzima wa nchi na suala zima la ufisadi inatisha!hakuna anayemuogopa mwingine, Viongozi wamekuwa kama kuku wanaofukuzana wakigombea maslahi yao.NINI HATMA YA TANZANIA? NA MTANZANIA WA KAWAIDA?
JUKUMU HILO NI LETU MIMI NA WEWE KUAHAKIKISHA KUWA TUNAFANYA KWA SEHEMU YETU ILI SIKU YA SIKU MUNGU AKITUULIZA TULIFANYA NINI TUWE NA JIBU.
 

Mkuu,
Mimi nilidhani presidaa ana masters, are you sure hana? Na mbona nilisikia at one time wanamuita Doctor? si mtu anatunukiwa udoctor baada ya kuwa na masters, hebu naomba mnielimishe hapa wajamii.
 
Kama hakuna mabadiliko ya Katiba,Tume ya uchaguzi ,mahakama huru bunge huru ,basi mtapiga makelele mengi na kusema sana ila Utawala wa SUltani CCM hata haupati habari ,watamuondoa Kikwete watamueka mwingine ,yaani wao kwa wao na wanahakikisha kihio mpya anashinda.
 
Asante Mwana Kijiji kwa taarifa na makala yako. Nashindwa kushangaa kwa balaa lililoingia katika nchi yetu kwa kipindi kifupi kupitia kwa viongozi wetu. Mungu inusuru taifa letu.
Pamoja na hayo adhabu tutakayoipata sisi watanzania ni ile ya kuwachagua tena miaka nenda rudi watu hawa hawa. Sasa hivi tunashangaa na hizi skendo, ngoja JK aingie madarakani awamu ya mwisho. Hakuna rangi ambayo hatutaiona.
 
Mkuu,
Mimi nilidhani presidaa ana masters, are you sure hana? Na mbona nilisikia at one time wanamuita Doctor? si mtu anatunukiwa udoctor baada ya kuwa na masters, hebu naomba mnielimishe hapa wajamii.

JK ana doctorate ya heshima. Hata rais wa ZnZ Karume anayo ya heshima jana nimeona TV ameandikwa Dr. Kwa bongo usishangae lazima na yeye ajiunge na mlolongo wa watendaji wake kujipachika udokta ili angalau wafananie.
 
Hongera Mwanakijiji. Taarifa zote ninazoo!!!!! Kisu kinakaribia mfupa. Kwa mtaji huo na kwa vile Vyama vyote vya Upinzani ni matawi madogo ya CCM na kama ni kuandikisha kipya ni mapaka watu wa Usalama wafanye Vetting yao ndio uende kwa Mgosi kuandikisha chama itabidi tutumie mbinu za Madagascar kwani waalimu watakuwa wamepoa ifikapo Oktoba 2010. Kwa faida ya wasomaji wako ni kwamba wakati mchakato wa IPTL unaanza Kikwete alikuwa Waziri wa Nishati baada ya machafuko ya OIC .;Cleopa Msuya akapewa uwaziri Mkuu na Jakaya akawa Waziri wa fedha ndipo waliposaini mkataba wa IPTL kwa hiyo alikuwepo kwa niaba ya Serikali. Wakati Mjadala ulipofanyika wa kuridhia makataba wa IPTL 1997 kIKWETE akiwa Waziri wa Mambo ya nje Kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri ilipokuja hoja ya kuwafukuza IPTL iliyoletwa na KATIBU mkuu nISHATI Patrick RUTABAZNIBWA kikwete alikuwepo na Chenge akishirikiana na Zero (Sumaye) waliyumbisha kikao kwamba atafutwe Arbitrator matokeo yake tunayajua TANESCO walilipa Dola milioni moja kwa ARBITRATOR NA TUKALIWA kesi walishinda;yeye alikuwepo leo hii anasema IPTL inunuliwe haraka. Ni kweli huyu Bwana ni fisadi mkubwa hana tofauti na Rostam. Pesa za Kugombea URais walimpatia mafisadi wakiongozwa na Lowasa. Za uchaguzi haswa walichukua IMMA Advocates (KUPITIA DEEP GREEN) akiwepo mwanaye Ridhwani kama mKurugenzi. Huku wakijua LITALIPUKA WAKAMUA KUIFILISI ILE KAMPUNI wakijiamini kwamba kwa sheria za nchi hii kampuni ikishakuwa Liquidated huwa haidaiwi kwani kisheria haipo. Masha akapewa zawadi ya Uwaziri kama birthday cake huwa mtu hanyanganywi!!anaogopa akimfukuza atatoa siri. Kimsingi ni kwamba ni sawa na "RANSOM" ameweka rehani madaraka yake.Ndio maana amekuwa kasuku''Nataka tuwe makini tusifanye makosa serikali ikashitakiwa'' Asipozinduka atajuta kuliko anavyojuta Mkapa kwani tutakapoanza kuwatoa mkuku ''No retreat No surrender'' hata makaburi yao tutafukua!!! Kama sio kizazi hiki hata 2030 aluta continua hahahaaaa!!!!
 

Du kweli jamaa una hasira! ulivyo flow inaonyesha wazi umekerwa. Thanks for the information.
 


KAKA,NI KWELI KWAMBA KAMA KITU WEWE HUJAKISIKIA HAKINA UKWELI?kama unataka kwenda sawa na mwanakijiji basi jaribu KUMECHANISE SOURCES zako za information,au vp?

NINAKUBALI STAILI YAKO ULIYOIMALIZIA.........kweli inasikitisha sana!kwa hili na mimi NAUNGA MKONO.IT HURTS,I FEEL SO MUCH PAIN!

SHIMO WAMETUCHIMBIA,WANATUMBUKIA WENYEWE
 
Hapa nguvu sina........miafrica bana utaona tayari yamempitisha tena 2010.
Mi naona hatuna chetu tujipange kuanzia 2050 kizazi chao kitakapo kuwa kimepukutika.
 
.............................Kwa mtaji huo na kwa vile Vyama vyote vya Upinzani ni matawi madogo ya CCM na kama ni kuandikisha kipya ni mapaka watu wa Usalama wafanye Vetting yao ndio uende kwa Mgosi kuandikisha chama............................ !!!!



HAPA KAKA UMEPIGA IKULU!yani ukweli mtupu yani.dah!mimi hapa nimeshachangaywa ubongo hata sielewi niongee nini!ANYWAYS ngoja niendelee kupitia............
 
haya yote yanajulikana kwa mtu yeyote anayetaka kujua siyo siri. Ndio maana nashangaa watu wanazungumzia mgongano wa maslahi! Sheria zetu wenyewe (walizozitunga wao) wamezitengeneza ili wao wawe wafaidikaji wa kwanza kabisa wa ubovu wa sera zao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…