Hongera kwa uchambuzi wako ndugu MWANAKIJIJI.
Pamoja na mambo mengi ya busara forum hii inavyo jitahidi kufanya ili kurekebisha maadili, nami ningependa kuchangia kidogo.
Japo wahenga husema kuwa samaki mmoja akiooza basi wote hali moja, kwa upande wa kapu la CCM na serikali yake samaki wote kimsingi wameoza hivyo ni vigumu mmoja kuwa mzima. Maovu mengi ya CCM kila mtu anayajua na mengi furum hii imechangia sana kuyalipua, sasa nini kifanyike?
Nionavyo mimi, JK pamoja na udhaifu wake unaotia kichefuchefu, mi nna machache ya kusema.
Utawala uliopita ndio uliomuandaa kuchukua madaraka, hivyo ilibidi naye anywe damu ya walalahoi ili afikike hapo alipo, inaonyesha kuwa uovu mwingi ambao ulikuwa chini yake na hakufanya kitu kuzuia ni kwasababu ndo ilikuwa gear yake ya kuwaacha wenzake wajichafue ili yeye apite.
Kimsingi yeye hakushiriki bali kosa lake ni hakuzuia maovu hayo alipokuwa Wizara ya madini au Fedha, kwake ilibidi afanye vile ili wenzie wamwone kuwa ni mwenzao, ndo maana wanashindwa kumlipua kwani wanajua kuwa kwasasa ameshika mipini miwili, (uchafu wao na urais).
Nionavyo mimi JK anania ya kuleta mabadiliko, japo yuko karibu kuchanika msamba katika maamuzi ya aidha kuwasaliti wenzie au wananchi walio mchagua. Mambo mengi anayo yafanya yaki maendeleo yanaonekana kimataifa na kitaifa tusipinge tu kwasabubu ya upinzani (ukiangalia uhuru wa bunge kuna transparency na debate za kweli kuliko historia nzima ya bunge la Tanzania).
Nionavyo mimi upande wa biashara na siasa kama sija kosea Tanzania hatuna sheria inayo mkataza waziri kuwa na shares au kumiliki biashara, hivyo JK yuko ndani ya misingi ya haki yake kama mtanzania wa kawaida. Halafu sioni kwanini asijaribu kuwa karibu na mtu aliye wekeza nae, kwani ingekuwa wewe Mwanakijiji ungefanyaje ungejiweka mbali na mwekezaji wako? hizo ni strategies za kibiashara tu.
Nionavyo mimi kwakuwa kapu zima la CCM limeoza je naye akiwa mmoja wao afanye nini? Kwanza na nampongeza kuwafikisha mahakamani baadhi ya mafisadi wakubwa kama Yona, Mramba, Mgonja na akina EPA (ni moja kati ya mambo ambayo asingeweza kufanya). Japo kwa wengi inaonekana ni kiinimacho fulani lakini mi naona kama ni hatua moja mbele.
Nionavyo mimi, ni maswali mengi inabidi tujiulize kama sisi, je tuna institutions za kweli za kusaidia kupambana na ufisadi na kusafisha kapu lilijaa samaki wabovu? mijadala ya hivi karibuni ya Tanesco, Bunge, Bandari, TRA, TAKURURU, Madini na Benki kuu inaonyesha ufisadi mtupu. Je tuna mahama ya kweli ambayo ni safi, FBI yetu je iko safi? DCI?
Kama ulivyosema Mwanakijiji, ukijihusisha na wezi na wewe utaoneka mwizi, lakini issue hapa ni complicated usipojihusisha nao, utajihusisha na nani wakati hakuna msafi hata mmoja?
Nionavyo mimi Tanzania tunakazi kubwa sana ya kubadisha maadili na hulka zetu za kijinga, uchafu wetu haupo kwa viongozi tu upo pia from our grass roots. Tunaishia kuwalaumu viongozi kila dakika wakati sisi ndio tunaowachagua ili walinde maslahi yetu madogo madogo. Tunapata mshahara laki na nusu, familia watoto wa tano, vimada wawili na watoto kadhaa wengine. Kila siku vikao vya kila siku kwenye baa, zungusha kwa saanaaaa. Hizo pesa tunazitoa wapi budget ya karibu mil 2 kila mwezi na sisi ni wafanyakazi wa kawaida? ofcourse lazima tumchague mtu anaye kula matawi ya juu wakati huo huo atuachie na sisi tule matawi ya chini. Culture hii ya mtanzania wa kawaida haijaanza leo, ndo maana wabongo hatuandamani hata tukikandamizwa vipi, what for?
Siku moja nilikula dinner na mkt wa chama Chadema, nikamuuliza maoni yake kuhusu CCM, hakusita kunijibu kuwa "li CCM nikama lidude fulani kubwa sana lililoshikana kwa marefu na mapana, likibiringika linabiringika kwa pamoja, likianguka linaanguka pamoja, uwezo na ufanisi wake unawazidi uwezo hata viongozi wake, ndani yake kuna mifarakano, mitafaruku, matatizo lakini nguzo zake ni imara kuliko unavyofiria"
Nionavyo mimi, ndugu Mwanakijiji CCM siyo ya kuanguka leo au JK kutoukwaa urais tena, please be reasonable, mwangalie RA pamoja na tuhuma zote hizo aliporudi kwa wapiga kura wake walimpokea kama rais, Mcheki Lowasa, Chenge and the list goes on.
Nionavyo mimi inabidi tujaribu kuzikubali juhudi za JK za kuleta utawala bora, elimu, afya na mawasiliano. Ili mkulima apate kuuza mazao yako sokoni, mwanae aende shule na mkewe apate matibabu ya uzazi hospitali. Wakati huo huo tuendelee kufaidi uwazi huu wa vyombo vya habari ambao unatuwezesha kutoa maoni yetu pale tunapo jisikia, japo sio asilimia mia (ulimsikia spika analaumu internet hapo juzi). Halafu tuendelee kushabikia wabunge wetu wakilipuana Bungeni.
Nionavyo mimi, kwa kifupi, siku moja niliposafiri kwenda mwanza kupitia Nairobi , down town Nairobi niliona maandishi makubwa yameandikwa ukutani yasemayo " KUNA MWANGA GIZANI"