Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #261
Duh ebana eeeh hii nilishaisahau.....
I know.. Watanzania hatuna kumbukumbu nzuri mambo mengine ni kama time warp continuum..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh ebana eeeh hii nilishaisahau.....
I know.. Watanzania hatuna kumbukumbu nzuri mambo mengine ni kama time warp continuum..
yote niliyoyasema ni kweli tupu! wao wanajua na wanajua ninajua.. na wapo watu wengine ambao wanajua.. Lowassa anasema "waligongana kwa bahati mbaya na Karamagi pale Hotelini"...
Nashukuru Mungu sana Kikwete ni Muungwana sana kwenye Uhuru wa habari, maana sipati picha kipindi cha zama za uwazi na ukweli sijui kama tuneongea hivi. Kila la Kheri Tanzania maana nahisi tunaelekea kwenye demokrasia ya kweli
sisi kule kwetu kijiweni, sku zile vyama vingi vinaanza walitwambia "msiwafuate hao wanataka kumrejesha sultani" watu walitiwa hofu za kijinga na wajanja wanaendelea kufisidi nchi yetu hadi leo, huku bara wenzetu si haba mmezugwa, mmekuwa ndondocha kwa kauli za baba wa taifa za karne ya 20,tokea mfumo wa chama kimoja kuwa "rais bora atatoka CCM, bila CCM imara nchi yetu itayumba" nyimbo hizi mkiimbiwa tu wenzetu hamna tena blah blah kama hizi za nani fisadi nani mwizi.Yaani afadhali CCM itawale maisha japo ni genge la wezi na majambazi, lakini WOSIA WA BABA WA TAIFA UDUMISHWE HATA VIPI IWAVYO. shauri yenuSijui kwanini tunazungushana na kudai watu wote walioatajwa kwenye orodha ya Ufisadi wanastahili isipokuwa Rais Kikwete! Hata viongozi wanaotambua baadhi ya uzito wa tuhuma zilizotolewa na wanaodai kuwa zitiliwe maanani hujikuta wanajing'ata ng'ata kuhusu Rais Kikwete. Baadhi ya watu wamefikia mahali pa kulaumu kina Dr. Slaa kumuweka Kikwete katika kundi hilo kwani JK ni safi! Hata hivyo ushahidi wote uliopo unaonesha kuwa JK siyo safi na yeye ndiyo awe wa kwanza kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake!
a. Mkataba wa IPTL ulisainiwa yeye akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Hakuna mkataba mbovu kama huo. Kushindwa kwake kutetea maslahi ya nchi akiwa Waziri na kulisababishia Taifa hasara kubwa ilikuwa ni kilele cha kutokuwajibika na kushindwa kuongoza. Akiwa Waziri mwenye dhamana ya nishati Ndg. Kikwete alitakiwa kuhakikisha kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano inaingia kwenye mkataba ambayo inaweza kujitoa pasipo kupata adhabu kubwa. Alishindwa hivyo na hivyo kuoneshe kutokuweza kusimamia maslahi ya nchi.
b. Wakati Rada ya bilioni 50 inanunuliwa, Ndg. Kikwete alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa na wakati sakata lenyewe linaanza alikuwa ni Waziri wa Fedha. Akiwa Waziri mwenye dhamana hiyo alishindwa kabisa kufuatilia ukweli kuwa kampuni ya BAE siyo mali ya serikali ya Uingereza na ya kuwa rada yenyewe ilikuwa imeongezwa kwa asilimia 24. Kiasi hicho kinakaribiana kabisa na wastani wa asilimia 20 za fedha za umma zinazopotea katika manunuzi ya serikali (public procurement).
Alishindwa kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa letu yanalindwa na alipopata nafasi ya kuonesha busara aling'aka na kusema "kwanini sisi ni idara ya Benki ya Dunia? ni kututukana kudai kuwa tusubiri Benki ya Dunia kutuamulia nini kinatufaa".
Ndio maana leo hii anapokuja na kuzungumza kuwa hawezi kuamini kuwa nchi kama Uingereza inaweza kuacha kampuni "yake" kurusha rada hiyo kwa bei hiyo wengine tunamshangaa kwani alikuwa na nafasi zaidi ya 20 ya kuweza kupinga ununuzi huo lakini alikuwa ni kinara wa kutetea tenda hiyo ya rushwa! Ni kuelewa hilo ndio utaona ni kwanini hakutaka watu wamuulize Rais Mkapa juu ya suala la rada, kwani miongoni mwa wahusika wakubwa ni yeye mwenyewe Kikwete.
c. Kama nilivyoonesha hapo juu kuwa Rais Kikwete aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Kwa hivyo nina uhakika kabisa alikuwa anajua kabisa jinsi mikataba inavyoingiwa na alikuwa na kila sababu ya kuhakikisha kuwa mikataba inalinda maslahi ya nchi na kunufaisha nchi wakati inawapatia wawekezaji faida ya kibiashara. Kwa kitendo chake yeye mwenyewe kuwa ukaribu na wafanyabiashara hao hasa swahiba wake ambaye ni mmiliki mkubwa wa ardhi yenye vito na madini Bw. James Sinclair, Rais Kikwete tangu akiwa Waziri wa Nishati na Madini na baadaye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje amekuwa mtu aliyetiwa upofu na "dhahabu".
Wakati Rais Mkapa na Yona wanajipatia tenda ya Kiwira, Rais Kikwete na Msabaha walikuwa wanajisogeza karibu na Kampuni ya Tanzania Royalty Exploration ambapo kuna madai (yanayothibitishwa na taarifa za SEC na EDGAR) kuwa Msabaha na Kikwete walikuwa na "hisa" za kiasi fulani. Kampuni hiyo ya TRE iliingia mkataba na Barrick Gold kuwa inapovumbua madini katika ardhi inayomiliki basi Barrick wanakuwa wanunuaji wa kwanza.
Ni wao TRE waliouzia Buzwagi kwa Barrick na maeneo mengine kadhaa kwa makampuni mengine. TRE inaponufaika kwa mikataba mibovu ambayo serikali inaingia na makampuni ya uchimbaji kuna watanzania wawili ambao nao wananufaika (ni wazi wapo wengine na wengine ni vigogo wengine) na dili hizo.
Ni kwanini Barrick walikuwa wa kwanza kukubali mabadiliko ya vipengele vya mikataba yao? jibu ni ushawishi wa James Sinclair na Kikwete ili kutetea kilicho chao. Kwa yale makampuni ambayo hayana ukaribu wa James Sinclair na Kikwete (JK alimualika JS kwenye kuapishwa kwake na mara nyingi amekuwa mgeni wake akija US, na binti ya JS aliyeko Tanzania ni rafiki wa karibu...) basi imekuwa vigumu kuwashawishi kubadili vipengele hivyo.
Ndio maana hadi leo hii si kweli kuwa kupitia vipengele na kuzungumza na "wakubwa" hao kuhusu mikataba kumekoma kama alivyodai mjasiriamali mwingine Nazir Karamagi alipokuwa akijaribu kupangua hoja za Zitto. Ukweli ni kwamba kamba waliitundika wenyewe serikali na ni wenyewe walioziweka shingo zao humo! wawekezaji wanatishia kuondoa kigoda!! Serikali inabembeleza!!
Anapozungumzia matatizo ya mikataba Rais Kikwete anazungumzia kana kwamba tatizo ni kipengele kimoja tu! Hajachukua muda kufuatilia uzito wa hoja hizo kwani kwake ni kelele!
d. Kikwete si Safi kwani amewalinda watu wachafu! Waswahili walisema ukiwa na urafiki na wezi, usishangae watu wakakuhisi na wewe mwizi! Rais Mkapa anapomlinda mjasiriamali Mkapa, aliposhindwa kumsimamisha kazi mara moja Ditto na kuamua kumuacha ajiuzulu huku akiendelea kupata mafao yake alionesha udhaifu mkubwa wa uongozi!
Rais Kikwete amekuwa mtetezi wa wabadhirifu akikesha kutoa vitisho hewa akijaribu kutetemesha mabua na kuangusha vichuguu huku milima ikiendelea kuganda theluji! Ukimya wake kama ule wa Mkapa ni ishara wazi kuwa walifeli darasa la Mwalimu!
Anapoona kuwa madai ya ubadhirifu Benki Kuu, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu, n.k kuwa "kelele za upinzani" na kuwa "ndiyo demokrasia" anaonesha udhaifu mkubwa usiomstahili kiongozi wa nchi. Haiwezekani upotevu wa mabilioni ya fedha, matumizi mabaya ya madaraka kuwa viwe ni "kelele" tu!
Rais ni lazima we mtu ambaye hapuuzii masuala mazito na hayafanyi kuwa ni ya kijinga. Kwa mtu kuwa mpinzani hakuifanyi hoja yake kuwa "kelele". Leo hii wana CCM wenzake wanazungumza wazi kuhusu tuhuma hizi na kudai kuwa wanaotuhumiwa (akiwemo yeye mwenyewe) wajibu siyo suala la kupuuzia!
e. Rais Kikwete ameonesha na anaendelea kuonesha udhaifu mkubwa wa maamuzi hasa kwa kuwa mtu wa kusita sita na ambaye yuko tayari kutumia uwezo wake wote kutofanya lolote. Hivi hadi nini kitokee ndipo Rais Kikwete atajua kuwa mambo haya si ya kupuuzia? Wakati Lowassa ameenda kukutana na Karamagi kule London na mkataba wa Buzwagi ukasainiwa je Rais Kikwete alifahamu ujio wa Waziri wake Mkuu? Je walikutana? Kama Rais hakujulishwa kutiwa saini kwa mkataba mkubwa namna hiyo na Waziri Mkuu anakutana na Waziri mwingine pasipo ujuzi wa Rais je haoni ni ukosefu mkubwa wa kiutawala!? Lowassa alifuata nini London na kukutana na Karamagi badala ya kukutana na Rais?
Leo hii watu wakihoji mazingira ya kusainiwa mkataba huo kwanini hiyo iitwe kelele!
Tanzania imefanya kosa kubwa kumchagua Kikwete. Kosa hilo vizazi vijavyo vitasimulia kama hadithi, kuwa "hapo zamani za kale kulikuwa na mwana CCM mmoja ambaye aliwapo watu matumaini sana kabla ya uchaguzi. Watu wengi waliamini kuwa mwanaCCM huyo ndiye atakuwa mkombozi na kiongozi wa kuwaonesha njia ya kufikia nchi ile ya ahadi. Walipomchagua kwa asilimia 80 ya wapiga kura, Watanzania walijawa na matumaini... Miaka miwili baadaye watanzania walishika vichwa vyao kujuta, kwani waliyemdhania ndiye kumbe siye... !! "....
Kama Rais Kikwete hatabadili mwelekeo wa uongozi wake, na kama ataendelea kufanya kazi kana kwamba madai na hoja zinazojengwa ni "kelele" tu na hivyo kuendelea kufumba macho ufisadi unaoendelea nchini (na hapa simaanishi rushwa ya kutoa na kupokea tu, namaanisha matumizi mabaya ya madaraka, n.k) basi ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa Rais Kikwete hapati nafasi ya pili ya kutoitumikia Tanzania. Endapo atagundua upotofu wa uongozi wake na kusahihisha mapema ndani ya miezi sita ijayo yawezekana akajiokoa na kuukoa urais wake. Vinginevyo, Rais Kikwete atakuwa ni Rais wa kwanza kutawala kwa mhula mmoja!!
Nakushukuru tena na tena Mzee Mwanakijiji.
Kwa haya uliyoyasema kuhusu Mkulu, mimi nakuaminia. Ila narudia msimamo wangu niliowahi kuutoa huko nyuma kuwa ingawa Mkulu ni Graduate wa UDSM, IQ yake ni ndogo. Naamini Degree yake ni PASS ya chini kabisa ndio maana hajaweza kufanya Masters yoyote. Kama ni mambo ya IQ, msimlaumu. Mnategemea nini kwa mtu wa namna hii.
Hakuna ubishi jamaa ni HB, hivyo anapendwa na watu. Wengi hatukuyajua hayo mpaka aliposhika usukani na kuona jinsi anavyoyumbisha chombo.
Wana JF naomba msinielewe vibaya, mambo ya IQ ni IQ tuu haya uhusiano na degree ya UDSM. Kuna watu wameishia STD 7 tuu lakini wana IQ kubwa na kuna Magraduate wa Chuo wana IQ ndogo.
Kama kuna aliyesoma na Mkulu, atujulishe alitoka UD na GPA gani.
Mkuu,
Mimi nilidhani presidaa ana masters, are you sure hana? Na mbona nilisikia at one time wanamuita Doctor? si mtu anatunukiwa udoctor baada ya kuwa na masters, hebu naomba mnielimishe hapa wajamii.
Hongera Mwanakijiji. Taarifa zote ninazoo!!!!! Kisu kinakaribia mfupa. Kwa mtaji huo na kwa vile Vyama vyote vya Upinzani ni matawi madogo ya CCM na kama ni kuandikisha kipya ni mapaka watu wa Usalama wafanye Vetting yao ndio uende kwa Mgosi kuandikisha chama itabidi tutumie mbinu za Madagascar kwani waalimu watakuwa wamepoa ifikapo Oktoba 2010. Kwa faida ya wasomaji wako ni kwamba wakati mchakato wa IPTL unaanza Kikwete alikuwa Waziri wa Nishati baada ya machafuko ya OIC .;Cleopa Msuya akapewa uwaziri Mkuu na Jakaya akawa Waziri wa fedha ndipo waliposaini mkataba wa IPTL kwa hiyo alikuwepo kwa niaba ya Serikali. Wakati Mjadala ulipofanyika wa kuridhia makataba wa IPTL 1997 kIKWETE akiwa Waziri wa Mambo ya nje Kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri ilipokuja hoja ya kuwafukuza IPTL iliyoletwa na KATIBU mkuu nISHATI Patrick RUTABAZNIBWA kikwete alikuwepo na Chenge akishirikiana na Zero (Sumaye) waliyumbisha kikao kwamba atafutwe Arbitrator matokeo yake tunayajua TANESCO walilipa Dola milioni moja kwa ARBITRATOR NA TUKALIWA kesi walishinda;yeye alikuwepo leo hii anasema IPTL inunuliwe haraka. Ni kweli huyu Bwana ni fisadi mkubwa hana tofauti na Rostam. Pesa za Kugombea URais walimpatia mafisadi wakiongozwa na Lowasa. Za uchaguzi haswa walichukua IMMA Advocates (KUPITIA DEEP GREEN) akiwepo mwanaye Ridhwani kama mKurugenzi. Huku wakijua LITALIPUKA WAKAMUA KUIFILISI ILE KAMPUNI wakijiamini kwamba kwa sheria za nchi hii kampuni ikishakuwa Liquidated huwa haidaiwi kwani kisheria haipo. Masha akapewa zawadi ya Uwaziri kama birthday cake huwa mtu hanyanganywi!!anaogopa akimfukuza atatoa siri. Kimsingi ni kwamba ni sawa na "RANSOM" ameweka rehani madaraka yake.Ndio maana amekuwa kasuku''Nataka tuwe makini tusifanye makosa serikali ikashitakiwa'' Asipozinduka atajuta kuliko anavyojuta Mkapa kwani tutakapoanza kuwatoa mkuku ''No retreat No surrender'' hata makaburi yao tutafukua!!! Kama sio kizazi hiki hata 2030 aluta continua hahahaaaa!!!!
Mwanakijiji,
Mimi sijawahi kulisikia, kama ni kweli basi huenda hapo sio tu kuna moshi mkubwa bali hata moto wenyewe unawaka. Kwanini Lowassa akutane na Karamangi kinyemelea?
Pili hili la Kampuni ya Tanzania Royalty Exploration, je ni kweli Msabaha na JK wana hisa? Kama ni kweli basi pia hapa
patakuwa na moto mkali.
Kama madai yako yote haya Mwanakijiji ni sahihi, basi nchi yetu imekwisha. Huyu JS amefikaje mpaka kuwa karibu na JK?
Kweli inasikitisha sana!
.............................Kwa mtaji huo na kwa vile Vyama vyote vya Upinzani ni matawi madogo ya CCM na kama ni kuandikisha kipya ni mapaka watu wa Usalama wafanye Vetting yao ndio uende kwa Mgosi kuandikisha chama............................ !!!!
Umeanza tena! naona hujipendi. Waache wale wala wali wale wali wao!