Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Kwenye mambo ya msingi ni lazima tuwe pamoja kama wananchi, hizi siasa za upambe ndizo zinatufanya nchi yetu tajiri kuendelea kuwa masikini kwa sababu ya upeo mdogo wa siasa za nchi na ukosefu wa elimu ya uraia kwa wananchi walio wengi. Hii inachukuliwa kama ndio mtaji wa watu wenye nia mbaya kwa nchi yetu na kuendelea kuwahadaa wananchi kwamba wao ndio viongozi watakao wafikisha kwenye nchi ya ahadi wakati ki ukweli wanajua kwamba wanadanganya kwa makusudi na lililo kubwa kwao ni kutafuta mtaji binafsi wao na familia zao na sio nia njema wanayoitangaza kwenye majukwaa ya siasa.

Umefika wakati sasa tuone haja ya kuwa na mgombea binafsi hata ikitokea kwamba hatokuwa na wabunge wa kutosha lakini itasaidia kutoa somo kwenye demokrasia yetu iliyo lala usingizi wa pono. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeanza na maendeleo yatakuwa yanaanza kuchukua uelekeo. Imefikia wakati mtu hakubaliki hata kwenye chama chake mwenyewe lakini kwa kutumia pesa na wapambe hata akiwachosha watu eti tunalazimika mpaka amalize dakika 90 zake, katika nchi zenye uongozi makini huu ni utani na haupaswi kuendelezwa.
 
Waafrika bwana! Yaani tumefikia kiwango cha kuwazawadia fedha viongozi wetu tunaoona wamefanya vizuri ktk utawala wao. Halafu akina Watson wakisema akili zetu finyu tunakuja juu. Mimi binafsi sioni umuhimu wa hiyo zawadi ya MO
Kwa kuwa maisha ni uchumi, mtu aliyenazo kama MO Ibrahim kaamua mwenyewe kwa ridhaa yake kutoa pesa kwa vigezo vya utawala bora wa viongozi wetu. Sioni kama ni kitu kibaya kwa kiongozi kupokea tuzo hiyo, pale ambapo ataona hana kazi na pesa hizo anaweza kutoa misaada kwani pesa haijawahi kukosa matumizi duniani, ila kinyume chake yaani matumizi kukosa pesa.
 
Amedhihirisha pale Magogogni hakwenda kuongoza au kutawala ila kula bata,trip kwa sana..
Sio kufanya vitu siriaz kwa nchi ...
 

Mwanakijiji heshima yako. Umeshusha tuhuma nzito kama asemavyo FMES na baadhi ya wengineo. Nimetoa muhitasari na kunukuu hakika uliyosema katika maeneo hayo manne kama ifuatavyo:-




SWALI LA KWANZA:
Je kama kweli yaliyoandikwa a hadi e ni kweli, Mwanakijiji huoni kuwa hitimisho lako linakuingiza nawe moja kwa moja katika kundi ulilosema awali la kuzungukazunguka au kujiumauma. Yaani kwa kifupi unaweza kumpa mtu miezi sita afuteje makosa hayo a - e ili aweze tena kuwa kiongozi wa nchi ambapo unasema vizazi vijavyo tayari vinasubiri kusimulia historia mbaya.



Baadaye Field Marshall ES alielezea na kuhitimisha,

Na Mwanakijiji ukaguswa na ukweli fulani kisha ukanena,


SWALI LA PILI:
Mwanakijiji ni kipi alichokisema FMES kimekugusa na ama kubadili mtizamo, imani yako au habari uliyokuwa nayo. Na mwisho wa makala yako ukoje sasa maana hapo ndipo kuna hitimisho; kama nilivyokueleza hapo juu hitimisho lako halilandani na tuhuma ulizoziweka dhidi ya Rais.

Binafsi sioni haja ya kusubiri mpaka makala yako ya J’tano itoke, vinginevyo basi utoe kauli yako hapa kuwa hoja uliyoianzisha hapa iwe ‘suspended’ au ‘isijadiliwe’ mpaka utakapoikamilisha!
Maana siwezi kujadili mada ambayo tayari mleta mada anatuashiria kuwa ameshaikarabati na mimi sijui huo ukarabati ni wa kiwango gani na wa kina gani.
Nakuwa makini juu ya maandishi maana sote tunaelewa kuwa hata utofauti wa neno moja tu unaweza kuleta maana tofauti kabisa katika kile unachokiwasilisha au unachotaka tukielewe hapa na kukichambua.

Samahani kama nimepitwa na wakati katika mjadala wa hii thread!

 

Watanzania:
1. Mnashauriwa msipokee zawadi haramu toka kwa wagombea. Ikitokea mnahofia kuonekana wabaya (kwa kuwa wengi watakaogombea hasa toka Chama tawala ni viongozi kwa sasa, na baadhi ya wananchi huwa wanaogopa viongozi, jambo ambalo halifai), basi pokeeni (kwa usalama wenu) ila msiwachague wale waliowapa PESA, FULANA, KHANGA, & KOFIA (kama wao hawafai na vyama vyao havifai).

2. Kupiga kura NI SIRI, HAKUNA ATAKAYEJUA MGOMBEA ULIYEMCHAGUA. Watanzania waache uoga.
Hii inaanzia kwenye Mikutano ya kutafuta wagombea ndani ya Vyama, na kumalizikia kwenye Uchaguzi Mkuu wa Taifa.

3. Wananchi wana uwezo wa KUBADILISHA VIONGOZI, kwa kuwachagua wengine. Wananchi wakitumia uwezo huo ndipo wataheshimiwa na viongozi. Vinginevyo viongozi (wa Chama tawala na Serikali) wataendelea kuwadharau wananchi, na kuwasahau kwa miaka minne, kisha kuwaomba tena kura mwaka wa tano wa uchaguzi.

4. Mtu atajiuliza: Tutajuaje kama hao viongozi wengine/mbadala mfano Rais (iwe mbadala wa Kikwete ndani ya CCM au akitoka Vyama vingine- Chadema/CUF) hatakuwa failure kama Kikwete? itakuwaje?

Jibu: Inaonekana Kikwete ameshindwa kuongoza (he is a failure). Tuchague mwingine, na akiona kuwa Watanzania tumeweza kumtoa huyu JK basi atakuwa makini asiboronge, na Watanzania watakuwa wamepata ujasiri wa kuweza kumuondoa Kiongozi mbovu hata kama bado anataka kung'ang'ania madaraka. (Hili bado ndilo tatizo - Mentality)

5. Mchakato wa kuandaa mgombea dhidi ya Kikwete anapaswa kuwa wa ngazi mbili (two stages):
Kwanza kuwa na mgombea ndani ya CCM ambaye atakabiliana naye. Huyu ajitayarishe na atayarishwe. Watu wa kumpigia kampeni wawe nchi nzima na wawaelimishe wananchi ubora na mikakati ya mgombea huyo, pamoja na uzoefu wake (track record).
Pili kuwa na mgombea wa upinzani ambaye atakabiliana na mgombea wa CCM (awe mwingine aliyemshinda Kikwete, au hata akiwa Kikwete). naye afanye kampeni ya ukweli.

Kwenye stages zote mbili, ningependa kuona kampeni za ushindani kama ilivyokuwa ndani ya chama cha Democratic (US) kati ya the then Senators Barack Obama na Hillary Clinton.
 
kwahyo jk siyo safi kabisa waTZ tuamkeni jamani tujitoe kwa vizazi vye2 kwani hata wanaokula raha leo paris hawajaijenga wao,hamtaki tuenziwe kwa heshima........
 
JK alimualika JS kwenye kuapishwa kwake na mara nyingi amekuwa mgeni wake akija US, na binti ya JS aliyeko Tanzania ni rafiki wa karibu..........
 
Mi nakubaliana na wewe kabisa kua Kikwete sio safi.

Ila tukimuondoa Kikwete nani ambae ana afadhali???

Tuwe wakwelli jamani...Watanzania bado tuna mwendo mrefu..hatuna kiongozi ambae twaweza sema ni 100% kama kina Obama na Clinton...hawa wa kwetu kuna mawili,its either Ni fisadi au bongo lala (Mvivu wa kufikiria)

Kati ya hao wajinga wajinga wote waliopo mi nahisi yeye ana kauafadhali kidogo.

How i wish Lowasa na Mkapa wasingekua mafisadi...ukiondoa ufisadi wao they have the best leadership skills.

Bado watanzania inabidi tupelekwe kijeshi jeshi hadi pale tutakapokomaa na kuweza kufanya maamuzi wenyewe bila kufuata upepo-twahitaji bado kuweza kua na uhuru wa fikra,we are confined in one cirle that we have to get out and see reality.

Kutokana na hayo mi bado namchagua Kikwete,,,si kwa sababu ana uwezo ila kwa sababu katika mambumbumbu wote tulionao akiwemo na yeye ana kaufadhali...japo angebahatika kuzaliwa marekani hata u diwani asingepata
 
Jamani hii document ya mtikila inayoitwa ya uchochezi inapatikana wapi
 
Jamani hii document ya mtikila inayoitwa ya uchochezi inapatikana wapi

mfuate kanisani kwake, kwanini hujui yeye ni Reverend, ama mfuate ofisini kwake maana yeye ni mwenyekiti wa DP, Mfuate mahakamani kuu, maana pale huwa anashinda kufuatilia kesi mbalimbali ili zimuwezeshe kufanya reference za uhakika.
 
MM - you have vision.

Kuongoza Taifa si Kazi lelemama, Baba wa Taifa aliliona hilo na akaonya kwamba mtu anayeingia Ikulu awe amejiandaa kwamba ni yapi amejipanga kuwafanyika watanzania - sina uhakika na maandalizi binafsi ya Rais wetu kama aliyafanya vilivyo kabla ya kuingia White Hse!

Sasa miaka mitano imeisha - anakuja tena Kuomba mingine mitano sasa sijui kwa lipi jipya?
 
Umenikumbusha mgombea mmoja ambaye baada ya kura alijikuta akipata 0. Mshangao ni kwamba hata yeye hakujipigia kura. Ndivyo ulivyo. Sivyo nilivyo. Mimi Naweza tena zaidi ya wakina Kikwete 20.
 
????????????????????????????????????????.................................................mmmhhhhhhhhhhhhhhhh!
 
bado mimi nasema ni SAFI napinga hiyo kaka,kama with something fikiria kama ni wewe katika possition yake ungefanyaje kaka?
 
Tunahitaji kiongozi mmoja tuu ambaye atabadilisha nchi hii ,wala sio wawili au watatu mfano Africa ipo kama akina Jerry Rawlings uliona alichokifanya sasa hivi hapo jirani Paul Kagame anatesa tuu tunamuona sasa hivi Goodlucky Jonathan wa nigeria katika miezi miwili ya utawala wake ndoza za umeme nchi nzima zinakuja ,anafanya vitu vyake,Mheshimiwa KiKwete sasa basi miaka mitano kacheza mandebele muache ampuzike kwa amani ,Hafai hata kidogo,marafiki ni wengi mno na kazi yake haihitaji mambo kama anayofanya aondoke mwenyewe tuu tutamheshimu sana nakasirika mno kwa sababu nilikuwa mteja wake maarufu lakini amenizingua kwa tabia zake za uvivu wa kufikiri na kukosa ari ya kusimama wima kuongoza nchi, hivi anaona tabu tunazopata majirani zake hapa DSM,shida zote foleni barabani mainzi kwa ajili ya marundo ya matakataka, ,umeme,shida ,maji taaaabu weee, mlo mmoja, vibaka kama kazi , Sisi wote pamoja na wotot0 wetu (Kasoro yeye na familia 100 ) walioko tumboni tunaumwa presha,yote hiyo kasababisha yeye ,Kwa heri mzee mwezi wa kumi nenda salama tuachie Ikulu yetu
 
Habari za uhusiano huu kati ya JK na James Synclair zinajulikana ila zimekuwa zikidhibitiwa na ikulu ili zisisambae kwa wananchi; inaelekea sasa ikulu imechoka kulinda uozo huu! Mwaka 1996, akiwa katika ziara ya rais nchini Marekani (Washington DC), Kikwete alikuwamo katika mwaliko wa kwenda kumtambulisha Mkapa kwa Synclair. Baada ya mkutano wa kufahamiana, James Synclair alipatia Mkapa Master Card 'kama zawadi'. Mkapa alipokea na kushukuru sana. Wasaidizi wa Mkapa tuliokuwa katika msafara huo (watu 4 tu; mimi, Kiwanuka, Kiwete na [jina kapuni]) hakuna aliyejua hiyo credit card ilikuwa na dola ngapi yarabi! Aidha ni vigumu kujua iwapo hiyo ilikuwa zawadi (kama Synclair alivyosema) au rushwa ya kwanza kwa Mkapa akiwa rais na mkuu wa dola, ili ahakikishe Kikwete anaendelea kubaki serikalini kulinda maslahi ya Synclair. Kwa maneno ya Synclair akimweleza Mkapa, alisema, "Mr President, [akimshika Kikwete] this is a great man....a friend of mine...all the wealth I have today.... it is because of this man".
Hao ndio viongozi wetu; Mkapa na Kikwete, ambaye ni ndiye rais wetu wa sasa, na huyo ndiye James Synclair, rafikiye kipenzi wa rais wetu wa sasa. Watanzania ndio watakoaendelea kulipa garama za urafiki wa hao wawili.
Habari za siku nyingi?
 
Mwanakijiji ushanitia hofu,kwani umenifanya nihisi kuwa huyo swahiba wa mkuu wa nyumba yetu anaweza kuwa ndiye 'rais' wa mirija yetu ya uchumi yakhe!
 

sophist.. sasa hivi hili limerudi kwa Kikwete naye..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…