Julius Kaisari
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 1,176
- 677
Prophet Mzee Mwanakijiji
Last edited by a moderator:
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama Rais Kikwete hatabadili mwelekeo wa uongozi wake, na kama ataendelea kufanya kazi kana kwamba madai na hoja zinazojengwa ni "kelele" tu na hivyo kuendelea kufumba macho ufisadi unaoendelea nchini (na hapa simaanishi rushwa ya kutoa na kupokea tu, namaanisha matumizi mabaya ya madaraka, n.k) basi ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa Rais Kikwete hapati nafasi ya pili ya kutoitumikia Tanzania. Endapo atagundua upotofu wa uongozi wake na kusahihisha mapema ndani ya miezi sita ijayo yawezekana akajiokoa na kuukoa urais wake. Vinginevyo, Rais Kikwete atakuwa ni Rais wa kwanza kutawala kwa mhula mmoja!!
Huyu mzee mbona simsikii siku hizi?
Haya ni maneno ya Mkuu Mzee Mwanakijiji , kiukweli ni maneno ya kweli kabisa kuwa ile 2005, Watanzania tulifanya makosa makubwa sana kumchagua Kikwete na kuichagua CCM, kwani ni kweli leo miaka kumi baadaye, Watanzania tunashika vichwa kujuta kwani tuliyemdhania ndiye kumbe sie!.Rais Kikwete ameonesha na anaendelea kuonesha udhaifu mkubwa wa maamuzi hasa kwa kuwa mtu wa kusita sita na ambaye yuko tayari kutumia uwezo wake wote kutofanya lolote.
Tanzania imefanya kosa kubwa kumchagua Kikwete. Kosa hilo vizazi vijavyo vitasimulia kama hadithi, kuwa "hapo zamani za kale kulikuwa na mwana CCM mmoja ambaye aliwapo watu matumaini sana kabla ya uchaguzi. Watu wengi waliamini kuwa mwanaCCM huyo ndiye atakuwa mkombozi na kiongozi wa kuwaonesha njia ya kufikia nchi ile ya ahadi. Walipomchagua kwa asilimia 80 ya wapiga kura, Watanzania walijawa na matumaini... Miaka kumi baadaye watanzania wanashika vichwa vyao kujuta, kwani waliyemdhania ndiye kumbe siye... !! "....
leo hii tena mwanakijiji anataka Ccm chini ya Magufuli irudi tena IKULU? hata simuelewi
Upo?Halafu hawa ndio wanataka award ya MO!