Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Kikwete siyo safi! - yes I said it!

How relevant and valuable this topic was and is today! Bravo MMM!

Pamoja na hila na vitisho vya CCM (zamani na hata sasa; mfano kuhujumu uandikishaji wa wapiga kura kwa uchaguzi ujao Oktoba 2015.....nk) bado tuna kila sababu ya kusimama na kuhakikisha dhuluma na ufisadi haviendelei kuitafuna nchi hii.YATOSHA. SASA BASI.

Matabaka na mipasuko ya kifedha, kijamii na kidini imezidi na kama tusipochukua hatua kali na madhubutu kuitoa CCM madarakani tutalaumiwa sana na historia na kukuhukumiwa na vizazi vijavyo.
 
Hongera sana m.mwanakijiji kutoa hoja yakinifu yenye umakini na ukweli uliokidhiri endelea kutupasha nasi tunakuunga mkono kweli Lowasa hatufai
 
Salute to you MMM,

Nakubliaa nawe yale uliyoyasema kwa uwazi 2007, leo yanaishi kwa kujidhuhirisha. Tujilaumu Watanzania kwa kushupaza shingo zetu. Kwamwendo huu nakubaliana na mada yako kumhusu Lowasa pia!
 
Kama Rais Kikwete hatabadili mwelekeo wa uongozi wake, na kama ataendelea kufanya kazi kana kwamba madai na hoja zinazojengwa ni "kelele" tu na hivyo kuendelea kufumba macho ufisadi unaoendelea nchini (na hapa simaanishi rushwa ya kutoa na kupokea tu, namaanisha matumizi mabaya ya madaraka, n.k) basi ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa Rais Kikwete hapati nafasi ya pili ya kutoitumikia Tanzania. Endapo atagundua upotofu wa uongozi wake na kusahihisha mapema ndani ya miezi sita ijayo yawezekana akajiokoa na kuukoa urais wake. Vinginevyo, Rais Kikwete atakuwa ni Rais wa kwanza kutawala kwa mhula mmoja!!

Mkuu, JK ni rais wa kwanza kutawala in autopilot mode for 9 years....

and we were just quiet and hypocritical
 
If you are magician footballer then you are lion mess if not then C.Ronaldo.
 
Kikwete amejiuzia mgodi wa tanzanite one kupitia mwanae Rizwan na jamaa anaeitwa hussein gonga kwa bei poa ya bilion 38 tu.
 
Wanabodi,

Japo huu ni uzi wa siku nyingi, lakini the facts remain the same, hivyo naitumia
Ijumaa yangu ya leo, kuitumia tena fursa ya kujitokeza kwenye Ukumbi huu wa JF, katika zile makala zangu za kuhamasisha Watanzania tujitokeze kwa wingi kupiga kura.

Kutokujitokeza kupiga kura ni kosa!. Mwaka 2010 waliojitokeza kupiga kura ni wachache kuliko waliojiandikisha, hivyo tulifanya kosa la kwanza.

Kosa la pili ambalo watanzania tulilifanya ni hili kama linavyoelezewa na nguli huyu Mkuu Mzee Mwanakijiji, katika uzi wake huu
Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Rais Kikwete ameonesha na anaendelea kuonesha udhaifu mkubwa wa maamuzi hasa kwa kuwa mtu wa kusita sita na ambaye yuko tayari kutumia uwezo wake wote kutofanya lolote.

Tanzania imefanya kosa kubwa kumchagua Kikwete. Kosa hilo vizazi vijavyo vitasimulia kama hadithi, kuwa "hapo zamani za kale kulikuwa na mwana CCM mmoja ambaye aliwapo watu matumaini sana kabla ya uchaguzi. Watu wengi waliamini kuwa mwanaCCM huyo ndiye atakuwa mkombozi na kiongozi wa kuwaonesha njia ya kufikia nchi ile ya ahadi. Walipomchagua kwa asilimia 80 ya wapiga kura, Watanzania walijawa na matumaini... Miaka kumi baadaye watanzania wanashika vichwa vyao kujuta, kwani waliyemdhania ndiye kumbe siye... !! "....
Haya ni maneno ya Mkuu Mzee Mwanakijiji , kiukweli ni maneno ya kweli kabisa kuwa ile 2005, Watanzania tulifanya makosa makubwa sana kumchagua Kikwete na kuichagua CCM, kwani ni kweli leo miaka kumi baadaye, Watanzania tunashika vichwa kujuta kwani tuliyemdhania ndiye kumbe sie!.

Maadamu Watanzania tumepata chance nyingine tena ya kuchagua, jee tuendelee kuichagua CCM?!. Kama Kikwete alikuwa siye, tukafanya kosa kumchagua na matokeo yake leo tunajuta, jee huyu CCM waliyetuletea ndiye?!, jee tumchague?!.

Naomba kutoa wito kwa Watanzania wenzangu wote, wale wenye mapenzi mema na taifa letu, tuitekeleze kauli ya Mwalimu Nyerere kwa vitendo, kuwa kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa!.

Kama ni kweli mwaka 2005 Watanzania tulifanya kosa kuichagua CCM kama Mzee Mwanakijiji, anavyosema, then, October 25, tusirudie kosa, kwa sababu kufanya kosa sii kosa, bali kosa ni kurudia kosa!.

Lakini kama Mzee Mwanakijiji, ni muongo, anamsingizia Rais wetu Kikwete kuwa ni dhaifu, wakati ukweli halisi Rais Kikwete sio dhaifu!, na madai yake kuwa Watanzania tulifanya makosa kumchagua Kikwete ni ya uwongo, yaani kiukweli Watanzania hatukufanya kosa kumchagua Kikwete na kuichagua CCM, wala Watanzania hatujashika vichwa kujutia uchaguzi wetu wa CCM, then October 25, tusifanye makosa ya kutoichagua ten
a CCM!, tukifanya kosa hili ndipo tutajuta!.

Wewe Mtanzania, hakikisha October 25, unajitokeza kifua mbele kuitumia haki yako ya kidemokrasia, kujichagulia viongozi wako, watakaokuongoza kwa miaka mitano ijayo!.

Nawatakia Furahi Day Njema.

Pasco.

 
leo hii tena mwanakijiji anataka Ccm chini ya Magufuli irudi tena IKULU? hata simuelewi
 
Last edited by a moderator:
leo hii tena mwanakijiji anataka Ccm chini ya Magufuli irudi tena IKULU? hata simuelewi

Tatizi ni kwamba tunashindwa kuelewa anataka nini. Ninachoona ni kuwa anajua kuwa CCM ina matatizo makubwa na inaonesha kuwa hamtaki magufuli (i may be wrong), na anajua kuwa UKAWA/CDM bado hatujui kama ni chama kile kile kama CCM au ni tofauti kina sera tofauti. Lakini pia ni wazi kuwa hamtaki Lowassa na iana yake ya uongozi. Ambayo Kimsingi ni ile ile ya Magufuli.

Kwa hiyo kinachoonekana ni kile ambacho hataki, lakini ni bora tumsubiri aseme ni nini anachotaka na kwanini.
 
hatimaye yametimia baada ya miaka kumi ya huyu vasco da gama kila kitu kiko zero kabisa
 
Hii kasi ya kufukua makaburi hasa yanayomuhusu JK, nini kipo nyuma ya pazia?
 
Back
Top Bottom