Jambo ndugu mwanakijiji,
Nakupongeza kwa kuwa moja ya wanaharakati au wazalendo wa Tanzania
unayechangia kwa kiasi kikubwa katika kujenga uelewa wa wananci katika
masuala ya siasa hususan kujua haki na wajibu wao kama raia, uhuru wa
kikatiba na kadhalika.
Nisiwe na blaablaa sana. Naomba kama inawezekana (kama mtoa makala katika
gazeti) uzungumzie swala la viongozi ambao wamepewa dhamana ya kuliongoza
taifa hili lakini hawana huruma wala nidhamu kwa wananchi ambao ni binadamu
kama wao. Wamekuwa wabadhilifu, mafisadi wa kupindukia. Na tatizo hili
limekuwa institutionalised ndani ya goverment system ikianzia ndani ya chama
tawala. Kuwa institutionalised namaanisha kuwa ni kama desturi kuwa kiongozi
na ufisadi ni sawa na mwajiriwa na terms of employement! Mtu akishakuwa
kiongozi inakuwa ni kama wajibu wake kuharibu au kutumia vibaya kupindukia
lfisi na dhamana aliyopewa. Mzee Butiku jana alikuwa anasema kuwa Je
Tutafika kama viongozi wa sasa hivi ni kinyume na wale wa enzi za mwalimu
ambapo imekuwa ni kawaida kabisa kwa waziri au mbunge kuwa mfanyabiashara au
mwanahisa katika multinational companies? Huyu mtu si ni wazi kuwa atatumia
mwanya wowote katika ofisi yake ambayo ina dhamana ya wananchi kusaidia
biashara yake at the expence of the mwananchi?? Najua haya nayosemwa ni kama
marudio ya mambo ambayo yameshaandikwa sana, lakini binafsi nahisi haya
mambo hayata expire na hayatakiwi yawe hivyo. Ni muhimu sana tukatumia
mawasiliano ya magazeti na internet kuwaelimisha wananchi wengi iwezekanavyo
na kwa muda mrefu iwezekanavyo juu ya mambo haya ili wawe imara na tayari
kuiokoa nchi yao kwa njia iliyo sahihi. Ikumbukwe pia kuwa walio madarakani
au tuwaite MAKUWADI wa WEZI WA KIMATAIFA kama alivowaita mzee Butiku jana
hawapati usingizi na wanakuna vichwa kujua watapambana vipi na juhudu za
raia na wanaharakati wa sasa ambao wanawaandama tena wamewashika pabaya. Kwa
kuwa hawa makuwadi wana nyenzo aka ofisi za serikali wanaweza kuja na hoja
za harakaharaka zisizo na ukweli wala maana yoyote kuwalaghai wananchi wa
Tanzania ambao masikini wa mungu wengi wao hawajajaliwa exposure au
awareness. Hivyo unaweza kuona ni umuhimu ulio mkubwa sana kwa hizi harakati
za vyombo makini vya habari na wanasiasa wapinzani na hata walio ndani ya
CCM ambao wana maslahi na Taifa kuwaelimisha wananchi kila kukicha ili
wazibuke masikio na akili na kisha wachangie katika kufagia hawa
Makuwadi/mafisadi kutoka katika uongozi. Itawezekana tu. Njia ni kuendelea
kusema na kusema hadi masikio yatoke ukoko wa nta iliyowekwa na CCM kupitia
viongozi wake mafisadi.
Kwanini nimeamua kukuandikia? Ninasoma Tanzania Daima la leo hapa na kabla
ya kulimaliza tayari nimepata jazba (nadhani nina weakness ya jazba)!!
Tendwa na Makamba wametosha kabisa kunifanya nikuandikie hii email. Eti
Tendwa anasema wabunge wa upinzani waende majimboni wanahitajika na wananchi
na waachane na mambo ya kuhubiri ufisadi na kupaka wenzao matope. Unajua mtu
wa namna hii kama mnakaa jirani unaweza mvizia ukamtwanga hata jiwe la
manati akiwa anajinyoosha kibarazani kwake?? Ana mapoenzi au huruma na
wananchi wanaosota kweli?? Hawa wapinzani wameanzisha mwamko na wamechangia
sana tena sana katika juhudi za creation of awareness kwa wananchi wengi
ambao walikuwa wamepuliziwa dawa ya usingizi au chloroform ili waibiwe na
hawa mabazazi? Eti anadai kuwa habari zinazoandikwa juu ya Ufisadi ni muhimu
lakini zimeshatosha kwani zinaboa tayari!! Haya Makamba nae anaibuka na
kufananisha wala rushwa ndani ya ccm sawa na waumini wa dhehebu flani wasio
tekeleza jukumu la uumini kwa mfano labda padri anayetembea na mke wa mtu
n.k. Hawa wanataka kutumia udhaifu wa wananchi wengi ambao ni rahisi
kurubuniwa na maneno mabovu ya kisiasa kama haya kujiosha. Kimsingi ni kuwa
Tendwa, Makamba na viongozi wenzao ni wabovu kupindukia tena sana na
hawapaswi hata kusikilizwa kwenye mihadhara yeyote kwa kuwa hawajawahi
kutetea taifa kwa namna yeyote zaidi ya kutetea chama tawala. Wananchi
wanakula chama? Kama hawa watu wangekuwa ni waadilifu na wangetaka
waheshimiwe wasingethubutu hata kidogo kuwasanifu wananchi kwa kiasi kikubwa
namna hiyo!! Watu wanataabika, wanavumilia kuliko punda la mizigo linalokaa
umasaini, kule dryland areas, likichapwa bakora na kubebeshwa mizigo mwendo
mrefu bila hata kunyweshwa maji lakini linaenda tu lifanyeje, halioni hata
kama linaweza kumgeuzia kibao anayelipiga kwa kumfurumusha mbio na kumtwanga
vichwa na mateke. Fine, that is ok si njia sahihi kujibu kwa kumpiga. Njia
sahihi ni kwa yule mwenye punda kutompiga punda bila sababu.
Mheshimiwa Mwanakijiji mimi nimekuandikia haya kwa sababu mimi siwezi yatoa
gazetini na sina access wala experience ya kufanya hivyo. Pia uandishi ni
kazi kwani nadhani pia siwezi andika kwa mtitiriko mzuri kama wewe. Pia
nadhani Una blog, so unaweza kuitupa hii ndani ikawafikia wengi, japo labda
utatakiwa kuedit. Kimsingi elewa kuwa imformation is power na tuendelee
kuelezana na kuelezea uma mpana iwezekanavyo kwani hii ni silaha nzuri sana
kwa hawa Makuwadi.
Wasalaam,
Mwanakitongoji!!!