Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Kikwete siyo safi! - yes I said it!

kwani mimi niko kwenye vyama vya upinzani? wao wamejitwisha mzigo wao, na waubebe kivyao vyao!! Ukiangalia sehemu fulani tayari nilishajenga hoja hiyo kuwa kwa wao kumuweka JK katika orodha ya mafisadi walifanya strategic mistake...

Yes sir, you SAID so.....awesome!!.
 
Huyu ndio JK akiongoza kundi kumkumbuka Mzee wa Butiama.
[media]http://www.nationmedia.com/eastafrican/current/images/cart22102007ea.jpg[/media]
 
Waafrika bwana! Yaani tumefikia kiwango cha kuwazawadia fedha viongozi wetu tunaoona wamefanya vizuri ktk utawala wao. Halafu akina Watson wakisema akili zetu finyu tunakuja juu. Mimi binafsi sioni umuhimu wa hiyo zawadi ya MO

Nakuunga mkono mkuu Nyani.
Kwa nini tumzawadie mtu kwa kazi ambayo alistahili kuifanya? Mtu anapochaguliwa tunataka atende yaliyo mazuri tu, kwamba hiyo ndio kazi tuliyomtuma aifanye. Kwa nini sasa azawadiwe kwa kufanya kazi yake?
 
Wenzenu wanataka wasifiwe ili wajisikie kuwa wanafanya jambo kwa wananchi. HIvyo wananchi wanapowahoji na kuwazomea haingii akilini. Wanashangaa baada ya kufanya "mema yote" hayo, kwanini Waandishi na wananchi hawaimbi sifa zao, hivi "hawaoni" matendo mema ya CCM?
 
Tulilisema hili kama mwaka mmoja uliopita! Kikwete naye si safi, yes I said it!
 
Hivi kuna kiongozi yoyote wa CCM aliye safi kweli?

wapo ila wanaamini kuwa hawajachafuka kama wengine. Hivyo usafi kwao siyo kutokuwa na uchafu bali kutokuchafuka sana. Ni sawa na aliyechafuka mikono na yule aliyechafuka mwili mzima. Wale waliochafuka mikono wanajikung'uta tu na kuwaonesha wengine kuwa ndio wamechafuka kweli kweli.
 
Aisee mwanakijiji naona na wewe unataka uambiwe uanze kusali sala za mwisho sasa
 
Mkuu Mwanakijiji, mbona naona watu wa vyama vya upinzani wanampango wakumuomba JK masamaha kwa kumsingizia kuwa yeye ni fisadi na kumweka kwenye list ya mafisadi ya Dk Slaa? Sijui wewe kwa hilo unamaoni gani kama yalioyoandikwa na Rai ni ya kweli. Nawepia utajitokeza kuomba msaamaha kama watakavyofanya vyama vinee vya upinzani?

Kumbukumbu yangu inasema kichwa cha habari ya kumwomba JK msamaha iliandikwa kama mwaka jana vile na kicha CHADEMA wakatoa tamko la kupinga. JJ pia alilileta tamko hilo hapa jamvini likisisitiza msimamo wa CHADEMA kumuweka JK kwenye list of shame.

Mtoto wa Mkulima jaribu kupembua habari za nyuma. Lakini pia kumbuka ukitaka ukweli juu ya CCM hausomwi toka MT DAIMA vile vile hukumu aliyoshinda CHADEMA haiandikwi kwa usahihi gazeti Uhuru. Natumaini umenipata!!
 
Ndiyo, aliyeshikilia mikasi na ukaguzi wa nyama - sadly!
Huyu naweza diliki sema ni safi; kama unapinga toa sababu.

Huyu naye hajapata nafasi tu, CCM ni mtambo wa kutengeza uchafu; kila aingiako huko atachafuka tu! Someni "The Lucifer effect, how good people turn evil" by Prof Philip Zimbardo, mtapata picha jinsi CCM inavyofanikiwa kuwabadilisha watakatifu kuwa devils!. Ndio maana wengine tunasema tunahitaji kuanza upya, hatutafanikiwa kwa kukata matawi na kuacha mti. Madamu watanzania tunaendelea kuwachekea na kuwachagua CCM, basi tuendelee kuliakulia hapa JF angalau inatusaidia kutoa machungu, na hapa sasa lazima tukubaliane na NN (nafikri FMES pia amelisema hili mara nyingi sana) kuwa viongozi wetu ni reflection yetu sisi, ndivyo tulivyo, until proven otherwise. Na tuta-prove otherwise, tutakapoacha kuwachagua CCM!
 
Tunarudi pale pale tu:
Namna pekee ya kupata mabadiliko ya kweli ya kisiasa na kiuchumi Tanzania ni Msajiri wa Vyama vya Siasa nchini kukifuta chama cha Mapinduzi.

Sababu ni hizi:
Chama cha Mapinduzi kimejivisha madaraka makubwa sana. Amini usiamini chama hiki kina nguvu kuliko Bunge, Serikali, Mahakama au chombo kingine chochote hapa nchini.
Chama hiki kina uwezo wa kuvunja sheria yoyote ya nchi bila kufanywa lolote na yeyote. Kina uwezo wa kuvunja sheria ya nchi halafu kikaliagiza jeshi la polisi na mahakama nini cha kufanya!
Viongozi wake wanaweza kukaa miaka 5 bila kufanya lolote la maendeleo kwa taifa, halafu wakati wa uchaguzi wakamwagiza mtu au taasisi yeyote ikipe chama fedha na mtu huyo akashinda uongozi tena.
Chama hiki pia kimetambua kuwa namna ya kuendeleza ufisadi ni kuhakikisha kwamba watanzania wanaendelea kuwa maskini siku zote ili wawe waoga na wasiwe na hoja. Ukiwapa sh. 10,000 au 100,000 umepata uongozi bila maswali!
Umaskini wa watanzania sio swala la hali ya nchi au hali ya hewa. Ni wale wanaojiona wajanja wachache sana wamepanga hivyo!
Chama hiki pia kinatisha. Wanachama wake ambao wangeweza kuwa viongozi wazuri (na kinao wengie kimewaficha) wanagwaya kukohoa (kusema ukweli kwenye matatizo) au kutoka kwenye chama hiki. Kupata uongozi Tanzania sio kwa sifa za utendaji bali ni kwa jinsi unavyoweza kutii wakubwa hata kwa jambo ambalo ni kinyume kabisa na maadili au hekima za kawaida za binadamu.
Kimelifanya jambo la kutoka kwenye chama kama kosa la ki-ugaidi. Hivyo wengi hawathubutu!
Lakini kina wanachama ambao wanaweza kuwa viongozi wazuri sana na watendaji wazuri sana kama nchi yetu ingekuwa na uhuru na demokrasia ya kweli. Lakini watu hawa wamezidiwa nguvu na Chama hiki.
Chama hiki kimekuwa ni taasisi iliyo mbele kuvunja sheria za nchi kuliko mtu au taasisi yeyote nyingine.

Namna ya kuleta mabadiliko ya kweli ni kukifuta chama hiki kwa sababu ya ufisadi na uvunjaji wa sheria za nchi uliokithiri ili wanachama wake watawanyike kwenye vyama mbali mbali na kuwe na balance ya nguvu za kufanya maamuzi za kisiasa.
Kwa matendo yake chama hiki hakina tofauti na mtu anayeanzisha chama kwa sababu za ugaidi au ufisadi - HASTAHILI. CCM HAISTAHILI pia. TUIWEKE KWENYE JUMBA LA MAKUMBUSHO kwa kumbukumbu na historia yetu watanzania. Sasa hivi hamna lolote jipya ndani ya CCM.
Kumbuka silaha yao kubwa ni wingi wao. Na hatari moja ya "demokrasia" ndio hiyo: kura nyingi ndio ushindi. Wendawazimu wakiweza kujiunga kwa wingi wakawa wanafanya maamuzi yao ya kiuchizi-uchizi (ukiwahoji machizi hao watakwambia kwamba ni demokrasia ndiyo inatumika), nchi hiyo ina hatari mpaka litokee kundi jingine litakolokuwa kubwa zaidi na lenye nguvu za kisiasa.
Kwa Tanzania kundi jingine ni vigumu kujiandaa na kuizidi nguvu CCM kwani CCM wataingiza mamluki wao na muda si mrefu mnaanza kuulizana "nani kajamba", "nani kajamaba" bila kupata jibu.
Kumbuka Chama hiki kina uwezo wa kuiagiza mahakama au polisi kitu chochote kile, kwa hiyo hamna pa kwenda. Ni kama vile kuwa kinyume na CCM ni sawa na kuwa kinyume na dola. Vyombo hivi ndio ambavyo vingetusaidia kujenga uswa na haki na demokrasia ya kweli (kama ipo) lakini vinashirikiana na CCM kuvunja sheria za nchi na kuwantika wananchi haki zao za kisheria.
Kama hatuwezi kupata hayo yote kwa sababu ya kuwepo fisadi CCM kwa nini tusitatue tatizo letu kubwa kwanza - kufuta CCM halafu tujenge taifa.

Nilipotoa hii mada mtu mmoja (sijui mwana-CCM yule) akadai nipunguze hasira. Kuna nini la kufurahia hapa sasa?
 
Huyu naye hajapata nafasi tu, CCM ni mtambo wa kutengeza uchafu; kila aingiako huko atachafuka tu! Someni "The Lucifer effect, how good people turn evil" by Prof Philip Zimbardo, mtapata picha jinsi CCM inavyofanikiwa kuwabadilisha watakatifu kuwa devils!. Ndio maana wengine tunasema tunahitaji kuanza upya, hatutafanikiwa kwa kukata matawi na kuacha mti. Madamu watanzania tunaendelea kuwachekea na kuwachagua CCM, basi tuendelee kuliakulia hapa JF angalau inatusaidia kutoa machungu, na hapa sasa lazima tukubaliane na NN (nafikri FMES pia amelisema hili mara nyingi sana) kuwa viongozi wetu ni reflection yetu sisi, ndivyo tulivyo, until proven otherwise. Na tuta-prove otherwise, tutakapoacha kuwachagua CCM!

Kumbe Mwanakijiji naye alimpigia kura Kikwete!!! Yaani sikujua kuwa na yeye anaweza kuwa kwenye kundi la ndivyo tulivyo na kujidai sivyo alivyo.
 
mzee mwenzangu, kanuni kadhaa za uchafu zinasema hivi:

a. Mwenye kuchezea uchafu, naye huchafuka
b. Kuupaka uchafu rangi na kuunyunyiza marashi, hakubadili ukweli kuwa bado ni uchafu.
c. Aliyechafuka mikono, na aliyechafuka shati, na yule ambaye ni viatu tu vimechafuka kwenye uchafu ule ule wote ni wachafu, hawachekani.
4. Ni vigumu kumwambia mtu mchafu asafishe wachafu wenzake!

Binafsi, I don't like this Kikwete guy coz I think hajui anapoipeleka nchi yetu. In other words, hana vision of the future.

Having said that, siwezi nikam-characterize kuwa "sio mtu safi" kwasababu kama ilivyo case ya Mkapa, naamini kuwa hakuna kiongozi perfect.

Kama mwanafalsafa wa kale wa-kichina, Liu Shao-ch'i, aliwavyowahi kusema, "there is no such thing as a perfect leader either in the past or present, in China or elsewhere. If there is one, he is only pretending, like a pig inserting scallions into its nose in an effort to look like an elephant."

Ingekuwa jambo la busara basi (kama tutakubaliana na Liu), ku-focus zaidi kwenye good traits za leadership, na sio labels za nani sio safi na nani ni msafi zaidi. Coz I think bado tunasafari ndefu sana mpaka kufika huko mnakotaka tufike leoleo. Kwamba: ILI MTU AIONGOZE NCHI INABIDI AWE SAFI KAMA MALAIKA. I think ndicho mnacho dream hapa.

And I suppose Hii mijadala tunayoiendesha hapa either tunajifurahisha tu, ama tunataka tu kutoa nje chuki tulizonazo kama part ya therapeutic exercise. Lakini ukweli ni kwamba mijadala hii itakuwa na maana miaka 40, 50, 60 ijayo... Kwasasa, well, binafsi sidhani kama ina make any sense at all.
 
Kama hilo ni kweli kwanini ulisema Mkapa ni safi!?
 
JK Yupo kwenye list of shame , first eleven akiwa na mganga wa Timu Kingunge Mwiru.
 
Kama hilo ni kweli kwanini ulisema Mkapa ni safi!?

Kwasababu nilikuwa nataka tujadili hili suala zima la ufisadi katika picha kubwa kuliko jinsi mbavyo linajadiliwa hapa JF na nchini kwa ujumla. Kwamba wale ambao tumebahatika kuishi ng'ambo, tusilazimishe wale walioko Tanzania kubadilika overnite kama nchi za magharibi zilivyofanikiwa.Kwamba inabidi tuwe realists kidogo. Sio ku-hate just to get hate out of our sytem. Kwamba nilitaka ku-shift discussion kwa kutimia heading ambayo ilikuwa provocative (I think unafahamu saikolojia Mwanakijiji: ili kuwafanya watu wa-pay attention/engage, hunabudi kuwa provocative. Maana kila nilipokuwa naingia humu, nilikuwa nakutana na arguments mbazo hazijengi. Kwahiyo kwa standard zangu: Mkapa ni safi, Kikwete ni safi (japo sipendi utendaji wake). Mimi focus yangu ipo kwenye utendaji, sio labels.
 
kama mtu ni mchafu, hata ukimpamba vipi kwa mapambo na kumpulizia manukato.. unachofanya ni kuficha tu uchafu wake na kuhairisha kunuka kwake. Sasa ukiamua kubadili na kumuita msafi, utakuwa umebadili label lakini hutakuwa umemfanya msafi.

Kwa hivyo tunaweza kuwaita wezi, majambazi, walarushwa n.k wote wasafi ila tuangalie utendaji wao tu. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewafanya kuwa wasafi na wenye maadili?

Sawa Mkapa ni safi... Msafi kwa sababu hajachafuka, au msafi kwa sababu hajakutana na uchafu, au msafi kwa sababu hatutaki kukubali kuwa ni mchafu?
 
Back
Top Bottom