Uchaguzi 2020 Kikwete: Wanaosema Mikoa ya Kusini imesahaulika kimaendeleo hawaijui vizuri mikoa hiyo

Uchaguzi 2020 Kikwete: Wanaosema Mikoa ya Kusini imesahaulika kimaendeleo hawaijui vizuri mikoa hiyo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete amesema wanasiasa na wagombea wanaosema mikoa ya Lindi na Mtwara imesahauliwa na imeachwa nyuma kimaendeleo hawaijui mikoa hiyo na waongo.

Dkt. Kikwete ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika mkoa wa Lindi kwa wagombea wanaopitia Chama Cha Mapinduzi(CCM). Uzinduzi ambao umefanyika leo katika uwanja wa mpira wa miguu wa Ilulu, manispaa ya Lindi.

Alisema hakuna Mkoa wowote ambao unavitu vyote. Kwani mambo ambayo yamefanyika katika mikoa hiyo yanaweza kuwa yasiwepo mikoa mingine. Hali kadhalika yaliyopo katika mikoa mingine hayapo katika mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara. Kwahiyo siyo kweli kwamba mikoa hiyo imeachwa nyuma na imesahauliwa. Kwahiyo wanaosema hiyo uhenda hawaijui au wameamua kupotosha kwa makusudi.

Kikwete ambaye alitaja mambo mengi yaliyofanyika katika mikoa hiyo ikiwamo miradi ya maendeleo alisema mambo yaliyofanyika yanaoneka dhahiri na mabadiliko ni makubwa. Kwani yanayoonekana katika mikoa hiyo hayakuwepo.

Rais mstahafu huyo wa awamu ya nne alitolea mfano wilaya ya Nachingwea jinsi ilivyobadilika kimaendeleo. Akibainisha kwamba alipokuwa katibu wa CCM wa wialaya hiyo mwaka 1986 ilikuwa siyo jambo la ajabu kusikia watu wameliwa na Simba au kutembea bila kukutanana nyoka. Lakini hivi sasa Nachingwea imebadilika na inamaendeleo makubwa. Hayo ya simba na nyoka yamebaki kuwa ni historia.

Kuhusu miundombinu katika mikoa hiyo alisema hali ya barabara ilikuwa mbaya. Hasa kutoka katika mikoa hiyo kwenda Dar-es-Salaam. Hata hivyo tatizo hilo limekwisha. Kwani hivi sasa kuna barabara ya lami. Barabara ambayo ujenzi wake ulianza katika awamu ya tatu ya utawala chini ya hayati Benjamin Mkapa. Ambapo katika utawala wake yeye alimalizia.

Alisema kazi ya kuleta maendeleo kwa wananchi ni endelevu. Hata hivyo mambo mengi yamefanyika na yanaonekana, lakini baadhi ya wagombea na wanasiasa hawataki kuyasema kutokana na hofu ya kuharibikiwa dhamira zao.

" Kwamiaka mitatu mfululizo mkoa wa Lindi ilikuwa kinara kwa matokeo ya kidato cha nne na sita. Lakini hawataki kusema, wanakumbusha mambo ya zamani ambayo hayana mahusiano na hali ilivyo. Hata matatizo ya korosho yamerekebishwa hayapo lakini kwakuwa wamekosa hoja wanasema hata yazamani," alisema Kikwete.

Aidha Kikwete alisema kunakila sababu ya wananchi kuchagua CCM kiendelee kuwa chama tawala kutokanana kusimamia na kuendeleza amani, utulivu na mshikamano. Mambo ambayo yanasababishwa na sera unganishi na jumuishi. Huku akiweka wazi kwamba bila sera jumuishi na unganishi kungekuwa na migogoro.

Alisema licha ya Tanzania kuwa na watu wengi, eneo kubwa na watu wenye itikadi za vyama tofauti, dini tofauti na makabila tofauti takribani 120 lakini wananchi wanaendelea kuwa wamoja na wanaishi kama ndugu. Kwahiyo kunahaja ya kukipa ridhaa CCM kiendelee kutawala na kuunda serikali.
 
Anatuletea mambo ya historia hapa hatujasahau alivyotuma jeshi kwenda kuchukua gesi ya watu wa kusini huku akila 10% ya ujenzi wa bomba la gesi.

Huyu ndiye wa kumwamini? Tapeli.

Kala kashiba kavimbewa Sasa anacheua moja ya waasisi wa wizi na ufisadi mkubwa unaendelea mpaka leo nchini.
 
Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete amesema wanasiasa na wagombea wanaosema mikoa ya Lindi na Mtwara imesahauliwa na imeachwa nyuma kimaendeleo hawaijui mikoa hiyo na waongo...
Naunga mkono hoja. Maneno kuntu sana.

Ufipa wakija hapa wataanza kurusha miguu hovyo kama wanataka kubakwa.
 
Kama Mimi nimefanya haya, waliokuwepo awamu zote walikuwa wanafanya nini?.Mbona hawakuyafanya haya?

Jakaya anafanya kwa sababu ya wanafamiliya wawili ambao ni wagombea,Lakini nafsi yake anaumizwa na mgombea wao.
 
Anatuletea mambo ya historia hapa hatujasahau alivyotuma jeshi kwenda kuchukua gesi ya watu wa kusini huku akila 10% ya ujenzi wa bomba la gesi

Huyu ndiye wa kumwamini? Tapeli

Kala kashiba kavimbewa Sasa anacheua moja ya waasisi wa wizi na ufisadi mkubwa unaendelea mpaka leo nchini.
Hivi wewe ni mtu mzima au kijana wa kijiweni kwa lugha ya hiuo ya kichokoraa? Huwezi kujenga hoja bila kutukana? WaTz waungwana na wastaarabu tunawashangaa wewe na hao viongozi wenu waliowafundisha/mnaiga matusi.
 
Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete amesema wanasiasa na wagombea wanaosema mikoa ya Lindi na Mtwara imesahauliwa na imeachwa nyuma kimaendeleo hawaijui mikoa hiyo na waongo...
Mzee wetu mwenye kuheshimika sana Jakaya, hayo ni kweli uliyafanya wewe na Mzee Mkapa tena miaka ileee. Ijapokuwa kuwa na wewe ulizengua ktk suala la gesi. Ila huyu, nasema huyu, na ninarudia kusema huyu, ambaye ulituletea siyo kabisa.

Ebu ulizia huko issue ya korosho na tishio la kutaka kuwapiga shangazi zao, pengine ndipo utakapo zitambua hisia zao za moyoni.
 
Lindi mwaka 2000 inaonyesha miaka ya nyuma ilikuwa moto sana

 
Hivi wewe ni mtu mzima au kijana wa kijiweni kwa lugha ya hiuo ya kichokoraa? Huwezi kujenga hoja bila kutukana? WaTz waungwana na wastaarabu tunawashangaa wewe na hao viongozi wenu waliowafundisha/mnaiga matusi.
Kutukana? Kama Kuna mtu anatakiwa kutukanwa ni Kikwete kwa ufisadi na kutuletea Dicteta Ikulu.
 
Lindi ilipokuwa Lindi kwa mujibu wa wazee wanasimulia uchumi ulikuwa umechangamka na mpangilio wa mji ni uthibitisho tosha makao makuu ya mkoa Lindi shughuli za biashara na kilimo kilichangia muonekano huu.

 
Back
Top Bottom