HESHIMA ya taifa letu barani Afrika inaporomoka.
Nakumbuka kipindi cha Kambarage, kauli zake zilikuwa
kama moto nyikani, waandishi wa kitaifa na kimataifa walitambua.
Kumbuka majibu yake pale Jomo Kenyatta na ata pale Accra na Addis.
Waliokuwepo enzi hizo watakumbuka namna ukombozi wa Afrika ulivyokuwa
ni agenda kuu ya Kambarage na vita dhidi ya mikakati ya mabeberu.
Kauli zake ziliwapasua vichwa mabeberu na hata kuogopa encounter naye.
Ngoja niwape mkasa huu:
Nafahamu wengi wenu mwambkumbuka marehemu J>F Kennedy, aliwahi funga safari
mpaka USSR kukutana na Nikita Khrushchev, akiamini amejipanga na kwa vile yeye ni Mmarekani na
taifa lenye nguvvu angetawala mahojiano na kudictate vitu. Yaliyomsibu huko ni makubwa
hatosahau, kwa maneno yake huku akitamani kulia alitamka, "He walked all over me, made me look like a fool"
Kwa muda mrefu sana hakukuwai kutokea rais wa USA kukutana na raisi wa USSR, na hii ilidumu kwa muda
wa miaka mingi, Ndipo JFK alipoamini ana uwezo na nguvu ya kumface kiongozi wa USSR
Kisa hiki ni kukuonesha namna gani viongozi wengine huwa wamejiandaa na kujipanga kwa level za juu mno wanapokutana na maraisi wenzao na media za huko.