Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mbali na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na corona, nadhani ni wakati muafaka na sisi watumiaji wa mtandao huu wa JamiiForums tukaeleze ni jinsi gani janga hili limetuathiri kiuchumi na kijamii kwani ni wazi karibu kila mtu atakuwa ameguswa kwa namna moja au nyingine.
Maelezo yetu/ yako yatasaidia kutoa mwanga wa nini kinaweza kutokea au kuwapata watu wengine iwapo gonjwa hili litakuwa king'ang'anizi na pia iwapo tutalazimika kuchukua hatua kali kukabiliana na ugonjwa huu kama ilivyo kwa mataifa mengine.
Tupe athari zilizukukumbuka na hata kama umefaidika na uwepo wa gonjwa hili, tueleze ni kwa namna gani kwani kila kitu kina faida na hasara zake.
Tupeana uzoefu, maana uzoefu wako mbali na mambo mengine,pia unaweza kusaidia wengine kujipanga/kuchukua tahadhari kibiashara, kijamii, kiafya n.k endapo tatizo hili litaendelea.
=======
Baadhi ya Michango ya Wanachama

Mimi kwa kila wiki nilikuwa nalaza 200k+ pale SportPesa. Pasa hivi mechi hakuna, hali imekuwa tete na mtaani mzunguko wa pesa umepungua sana.
Mambo yamekuwa magumu.
Sent using Jamii Forums mobile app
=======
Nadhani kitu kikubwa ni uncertainty, lini ugonjwa utaisha watu waendelee na shughuli zao
=======
35% ya kipato changu imeondoka, 65% iliyobaki sina uhakika nayo. Namuomba Mungu shule zifunguliwe.
=======
Kuna Annual event huwa tunaifanya April lakini kwa sababu ya Corona imebidi tuahirishe. Huwa namake some money na nilishakua nishaweka mipango yangu sawia the Boom Corona hiyo. Nimechukia sema basi tu.
Leo ingekua harusi ya sister angu mmoja hivi lakini Corona imebidi wasogeze mbele kwenye tarehe zisizojulikana.
Sent from my iPhone using JamiiForums
=======
Dunia ipo na inaingia kwenye GREAT ECONOMIC DEPRESSION again
Tunapambana Biological War kupitia hii Biological Weapon iliyoachiwa
Hivyo kwa namna hali inavokwenda mambo yanazidi kuwa magumu sana
#Stayhome safe COVID-19 is everywhere
=======
Duh! Sijui itakuwaje, Allah atuongoze maana nishaanza kulihisi joto tayari...
Ushauri wangu kwa wana JF wenzangu:
1. Dont invest katika assets yoyote ile kwa muda huu wa mpito
2. Save as much as you can
3. Nunua chakula cha mda mrefu kama dagaa, maharage nk. kisha hifadhi
4. Ishi kimachale, kuwa tayari kwa lolote lile kwa muda wowote (Haswa wafanyakazi wa company binafsi)
5. Alert familia yako mapema kuhusu janga la corona waanze kujipanga
Note. Precaution is better than cure!