Kila aliye tayari aeleze jinsi Corona ilivyomuathiri Kiuchumi na Kijamii

Kila aliye tayari aeleze jinsi Corona ilivyomuathiri Kiuchumi na Kijamii

Kuna Annual event huwa tunaifanya April lakini kwa sababu ya Corona imebidi tuahirishe. Huwa namake some money na nilishakua nishaweka mipango yangu sawia the Boom Corona hiyo. Nimechukia sema basi tu.

Leo ingekua harusi ya sister angu mmoja hivi lakini Corona imebidi wasogeze mbele kwenye tarehe zisizojulikana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Daahh kiukweli Biashara yangu ya Nguo imetetereka , Dogo hauzi kama ilivokua.


Wenye Fursa jamaan ,tupeane tips hasa kwenye hiki kipindi
 
Dunia ipo na inaingia kwenye GREAT ECONOMIC DEPRESSION again

Tunapambana Biological War kupitia hii Biological Weapon iliyoachiwa

Hivyo kwa namna hali inavokwenda mambo yanazidi kuwa magumu sana


#Stayhome safe COVID-19 is everywhere
 
Kuna dogo ananidai pesa ndefu kiasi nimenata na beat la korona kumwambia kua sasa hivi mambo magumu sababu ya korona aniongezee miezi sita mbele kumbe ni fix tu sina hela ya kumlipa kwa sasa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh! Sijui itakuwaje, Allah atuongoze maana nishaanza kulihisi joto tayari...

Ushauri wangu kwa wana JF wenzangu:

1. Dont invest katika assets yoyote ile kwa muda huu wa mpito

2. Save as much as you can

3. Nunua chakula cha mda mrefu kama dagaa, maharage nk. kisha hifadhi

4. Ishi kimachale, kuwa tayari kwa lolote lile kwa muda wowote (Haswa wafanyakazi wa company binafsi)

5. Alert familia yako mapema kuhusu janga la corona waanze kujipanga

Note. Precaution is better than cure!
 
Back
Top Bottom