Kila aliye tayari aeleze jinsi Corona ilivyomuathiri Kiuchumi na Kijamii

Kila aliye tayari aeleze jinsi Corona ilivyomuathiri Kiuchumi na Kijamii

Kwa upande wangu nafanya kwenye NGO ya wamarekani, Sasa since tarehe 16 mwezi wa tatu tuliambiwa we have to work from home mpaka June, kwa hiyo HQ office imefungwa ambayo ipo DC and all country offices globally zimefungwa, pamoja na kwamba they provide all facilities za kutuwezesha kufanya kazi tukiwa majumbani Kama vile internet, muda wa maongezi, laptops , and other stuffs na mishahara wanaingiza on time, changamoto ni kufanyia kazi nyumbani huku watoto wote wapo likizo, to be honest imenifanya nashindwa kugawa muda wangu maana nikiona mtoto analia nanyanyuka nataka nikae nae, nikiona Hawa wengine wanacheza natamani nicheze nao,ikifika muda wa kupika, naingia jikoni Kama kawa, yaani kaa vile Sasa rtiba ya nyumbani naip akipaumbele kuliko ya ofisini. na pia kukaa nyumbani tu Yani morning to evening 24/7 sio kitu kirahisi hasa kwa sisi tuliozoea kutoka asubuhi na kurudi jioni.

Pili, Kuna zile transport allowance za kila mwezi kwa Sasa zimesimamishwa maana Kila mtu anafanyia kazi nyumbani, kibongo bongo transport allowance huwa hatuitumii yote tuunasave ingine tunaingiza kwenye Mambo mengine na hapa hatujui Kama hiyo June watasema tuanze kwenda ofisini au wataongeza muda, hii inategemea Hali itakavuokua kule Marekani

Mbaya zaidi Hawa wenzetu wanaamini kwamba serikali yetu haotoi data sahihi kuhusu wagonjwa wa Corona nchini kwa hiyo kila kukicha wanatuasa kuchukua tahadhari na kukaa ndani Kama huna Sababu ya msingi ya kutoka maana wanaamini wagonjwa ni wengi tofauti na idadi inayotangazwa

Kiukweli mi nshachoka kukaa ndani Kama Mwali[emoji3][emoji3]
Mbali na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na corona, nadhani ni wakati muafaka na sisi watumiaji wa mtandao huu wa JamiiForums tukaeleze ni jinsi gani janga hili limetuathiri kiuchumi na kijamii kwani ni wazi karibu kila mtu atakuwa ameguswa kwa namna moja au nyingine.

Maelezo yetu/ yako yatasaidia kutoa mwanga wa nini kinaweza kutokea au kuwapata watu wengine iwapo gonjwa hili litakuwa king'ang'anizi na pia iwapo tutalazimika kuchukua hatua kali kukabiliana na ugonjwa huu kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Tupe athari zilizukukumbuka na hata kama umefaidika na uwepo wa gonjwa hili, tueleze ni kwa namna gani kwani kila kitu kina faida na hasara zake.

Tupeana uzoefu, maana uzoefu wako mbali na mambo mengine,pia unaweza kusaidia wengine kujipanga/kuchukua tahadhari kibiashara, kijamii, kiafya n.k endapo tatizo hili litaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
week iliyopita tumeitwa makao makuu ya kampuni ninayofanyia kazi na kuwekwa wazi kuwa kuanzia sasa shuguli zoote zinafungwa rasmi kwahiyo hali halisi tunaiona so hakuna wakumdai mwenzake.
kila mtu apambane na hali yake, tutakuwa tunapigiana simu tu kujuliana hali, ukimpia mtu simu ukiona hapokei then hapatikani BASI UJUE KISHAKUFA.
 
Pole mate,
Kuna Annual event huwa tunaifanya April lakini kwa sababu ya Corona imebidi tuahirishe. Huwa namake some money na nilishakua nishaweka mipango yangu sawia the Boom Corona hiyo. Nimechukia sema basi tu.

Leo ingekua harusi ya sister angu mmoja hivi lakini Corona imebidi wasogeze mbele kwenye tarehe zisizojulikana.


Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom