Mbali na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na corona, nadhani ni wakati muafaka na sisi watumiaji wa mtandao huu wa JamiiForums tukaeleze ni jinsi gani janga hili limetuathiri kiuchumi na kijamii kwani ni wazi karibu kila mtu atakuwa ameguswa kwa namna moja au nyingine.
Maelezo yetu/ yako yatasaidia kutoa mwanga wa nini kinaweza kutokea au kuwapata watu wengine iwapo gonjwa hili litakuwa king'ang'anizi na pia iwapo tutalazimika kuchukua hatua kali kukabiliana na ugonjwa huu kama ilivyo kwa mataifa mengine.
Tupe athari zilizukukumbuka na hata kama umefaidika na uwepo wa gonjwa hili, tueleze ni kwa namna gani kwani kila kitu kina faida na hasara zake.
Tupeana uzoefu, maana uzoefu wako mbali na mambo mengine,pia unaweza kusaidia wengine kujipanga/kuchukua tahadhari kibiashara, kijamii, kiafya n.k endapo tatizo hili litaendelea.