Kila aliye tayari aeleze jinsi Corona ilivyomuathiri Kiuchumi na Kijamii

Kila aliye tayari aeleze jinsi Corona ilivyomuathiri Kiuchumi na Kijamii

Nina kumbi mbili za kuonesha mpira (vibanda umiza), nilikua sitegemei mshahara kabisa, lakini kwa sasa naonja uchungu wa corona kila leo naingia mtandaoni kuona kama kuna chanjo imepatikana lakini wapi. Aseeeee Mungu tunakuomba utufanyie wepesi

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hamna maisha mabaya kama ya kutegemea mshahara hasa mshahara wa serikali.
 
Nimelimiss toto langu la kihaya, mechi za UEFA ndio ilikuwa gia ya kuzugia kwa wife kuwa naenda kuangalia mechi kumbe naenda kuonana na muhaya wangu geto kwake yaani nikubanduana hadi saa Saba usiku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Kuna nyumba naiuza na mteja niliempata Yuko USA alishakubali kuinunua kupitia ndugu zake walioko tz Sasa USA Kuna lockdown hawezi kwenda bank sababu ya corona pia nahofia anaweza kubadili mawazo au ndugu zake walioko tz wakapata nyumba nzuri zaidi na ya bei nafuu.
 
Nilikuwa nafanya madili ya kuuza milango ya mbao toka mkoa A kwenda mikoa B na C .Maliasili wamechachamaa ,Wateja wanalia mambo magumu.

Faida yote nilikua ni kula bata ,kumwagilia moyo na kuweka mnyeke.Sina hata mia nikisikia mambo ya lock down natamani nijinyee.Biashara naifanya bila vibali.
 
Mbali na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na corona, nadhani ni wakati muafaka na sisi watumiaji wa mtandao huu wa JamiiForums tukaeleze ni jinsi gani janga hili limetuathiri kiuchumi na kijamii kwani ni wazi karibu kila mtu atakuwa ameguswa kwa namna moja au nyingine.

Maelezo yetu/ yako yatasaidia kutoa mwanga wa nini kinaweza kutokea au kuwapata watu wengine iwapo gonjwa hili litakuwa king'ang'anizi na pia iwapo tutalazimika kuchukua hatua kali kukabiliana na ugonjwa huu kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Tupe athari zilizukukumbuka na hata kama umefaidika na uwepo wa gonjwa hili, tueleze ni kwa namna gani kwani kila kitu kina faida na hasara zake.

Tupeana uzoefu, maana uzoefu wako mbali na mambo mengine,pia unaweza kusaidia wengine kujipanga/kuchukua tahadhari kibiashara, kijamii, kiafya n.k endapo tatizo hili litaendelea.
sie wengine hali zilikuwa mbaya teyar hii corona imekuwa kisingizio tu ila mambo yalishabumaaa muda tu.
 
Nina nyumba za wapangaji na watu wa kupokea wageni wanaishi hapo (tours) wanne ivi ila wiki ya pili wote wako nyumbani 24/7 sina lakufanya sababu aliekaa mda mchache hapo ni miezi tisa siwezi kuwaondoa ila najua kodi yangu itachelewa na sijui mpaka lini pia nilikuwa na cruser za porini mbili wiki ya nne hamna mtu aliekuja kodisha nilikuwa nataka anzisha product za saa ya ukutani ila material toka china zinachelewa still not sure kama zitasogea ....hasara ni nyingi ila lets keep pushing tusikate tamaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui nisemeje,?! INSHORT hali ni tete tumuombe sana Mungu atunusuru na hili Janga
 
Ratiba imevurugika mipaka imefungwa. Mbaya zaidi hatujui lini (if)mambo ya tarudi normal.
 
Mbali na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na corona, nadhani ni wakati muafaka na sisi watumiaji wa mtandao huu wa JamiiForums tukaeleze ni jinsi gani janga hili limetuathiri kiuchumi na kijamii kwani ni wazi karibu kila mtu atakuwa ameguswa kwa namna moja au nyingine.

Maelezo yetu/ yako yatasaidia kutoa mwanga wa nini kinaweza kutokea au kuwapata watu wengine iwapo gonjwa hili litakuwa king'ang'anizi na pia iwapo tutalazimika kuchukua hatua kali kukabiliana na ugonjwa huu kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Tupe athari zilizukukumbuka na hata kama umefaidika na uwepo wa gonjwa hili, tueleze ni kwa namna gani kwani kila kitu kina faida na hasara zake.

Tupeana uzoefu, maana uzoefu wako mbali na mambo mengine,pia unaweza kusaidia wengine kujipanga/kuchukua tahadhari kibiashara, kijamii, kiafya n.k endapo tatizo hili litaendelea.
Kwa upande wangu corona imeongeza market volatility kwenye forex hivyo pesa zinamwagika tu sasa hivi. Price zinakimbia hatati. Hakuna pair isiyomwaga pesa.
 
Binafsi kuna hela niliitarajia kuipata mwezi huu sasa nimeikosa mpaka hali itakaporejea kuwa ya kawaida na kibaya nilichukue fedha mahali nikitarajia kulipa kwa kutumia hela ambayo ningeipata huu mwezi na matokeo yake imebidi nifanye kazi ya ziada kurudisha hela ya watu.

Nashukuru sikuchukua hela nyingi zaidi kama nilivyotaka kwani kazi ya kulipa ingekuwa mara mbili.
The same same.
Nilitarajia kumaliza deni mwezi wa 5 nimesogeza muda mpaka mwezi August.
Unless otherwise tutakula nyasi. Hili balaa lisipoisha ni hatari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom