kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Wazungu hawakuanza leo kuzitaka rasilimali zetu. Wakati wa kutafuta uhuru kuna watu wetu walitumiwa na wakoloni kuzuia tusipate uhuru. Hata baada ya kupata uhuru kuna watu walitumiwa na wakoloni kupora uhuru na rasilimali zetu. Watu hawa wanaona viongozi wanakosea kwenye kila kitu, eti wao kwa msaada wa wazungu watafanya vizuri kama wakiongoza nchi.
Wajinga kabisa, Afrika kuna nchi gani ambayo iko vizuri kwakuwa viongozi wao wako karibu na wakoloni? Kuna viongozi ambao walikuwa karibu na wakoloni kama Mobutu, Kamuzu Banda na Jomo Kenyata?. Je, nchi zao leo zina afadhali gani kimaendeleo?
Hapa kwetu wakina Kambona na Mtei nao walikuwa wanampinga Nyerere kwa kukataa sera za wakoloni. Sasa hivi tunao wahuni wanaopinga namna taifa linavyoendeshwa, eti wako nyuma ya wazungu.
Hatudanganyiiiikiiii.