We jamaa huko serious, Design yenu ndio nyie mnasema nikiwa na Milioni naanzisha biashara ya kuku sijui nitapata kiasi gani etc.
Duniani mkuu Hakuna Kama Dp world, yani hawana Alternative, ukiona mpaka China ambaye hakubali Makampuni ya Nje yafanye kazi kwake Amempa Bandari Dp world ujue anachofanya hata wao hawawezi.
Crane unazoonesha hapo ni mataka taka ya Alibaba, hapa Tunaongelea Meli kupakuliwa kwa chini ya Masaa 48 toka wiki mpaka wiki mbili za sasa, Unaongelea Crane za kisasa zinazobeba Container zaidi ya moja kwa wakati mmoja, Unaongelea logistics za Kuhifadhi maelfu ya Container na Container liwe Visible kupelekwa Destination bila kupangua pangua, Logistic yake hapo sio ya kitoto, unahitaji software za Maana.
Mimi nimefanya kazi ICD inahandle tu Container 300-500 na kivumbi chake unakiona, ukijichanganya tu Container wakati wa kutoka inabidi upangue container kadhaa upate container yako na kila Container linapoguswa na Crane ni 50,000 hio, uzembe kama huo unaweza ingizia Kampuni hasara ya mamilioni.