N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Kuna tabia imeenea siku hizi ya watu kujiona wanajua kila kitu.
Ukweli ni kwamba hakuna anayejitosheleza kwa maarifa au ujuzi.
Unaweza ukawa bingwa wa hesabu kiasi cha kutatua milinganyo migumu kwa dakika chache, lakini kuna kijana ambaye hajafika chuo anapiga solo la gitaa mpaka ukabaki umeduwaa (solo guitar kama la diblo dibala ni hesabu zaidi ya unazozijua tena zile ni advanced applied maths).
Unaweza ukaitwa mhandisi, ukachora ramani za majengo ya ghorofa, lakini ukifika site fundi mwenye uzoefu ndiye anayejua namna ya kushika tofali, kusawazisha ukuta na kumaliza kazi kwa ubora.
Unaweza ukawa na shahada tatu, lakini hujui hata kuendesha gari la manual. Dereva ambaye hajawahi kukanyaga chuo anakufikisha salama kila siku.
Unaweza ukawa daktari bingwa, lakini ukashindwa kutengeneza bomba la maji nyumbani kwako.
Fundi bomba ndiye anayekutatulia tatizo.
Unaweza ukawa tajiri mkubwa, lakini chakula unachokula kimelimwa na mkulima ambaye pengine hana hata akaunti ya benki.
Maisha yamejengwa juu ya mgawanyo wa maarifa na ujuzi.
Kila mtu ana eneo ambalo anakuzidi, na wewe pia una eneo unalomzidi mwingine.
Hivyo usimdharau mtu kwa sababu ya elimu yake, kazi yake au kipato chake.
Ukifika mwendokasi panga foleni acha zako huna umuhimu kama unavyodhani, ulipomzidi mwingine nae kakuzidi maradufu.
Leo unamhitaji kidogo, kesho unaweza ukamhitaji sana.
Heshimu taaluma zote. Heshimu vipaji vyote. Heshimu kila mtu.
Kumbuka: Akili si kujua kila kitu; akili ni kutambua kuwa huwezi kujua kila kitu, na ndiyo maana tunahitaji wengine.
HIYO NDIO MAANA YA MAISHA.
ACHA DHARAU
Mwisho wa siku sote sie mavumbi.