Kila dalili zinaonesha Bwawa la Nyerere kuhujumiwa na wapigaji ili kupata kile wangekosa chini ya Hayati Magufuli

Sukuma Gang wenzio ndo wamekutuma uje uwaombee kwa Mama warudishwe!?
 
..kabudi si ndio alimdanganya magufuli sasa tunashtakiwa na kulipishwa mabilioni ya fedha? wewe unaona huyo ni mtu wa maana?
Alimdamganya nini au alimshauri sawa tu. Vitisho tu vya mashtaka ila ukiwa na washauri wapigaji mnashtakiwa na kushindwa. Mbona wenyekushitaki wamefungua mashitaka baada ya kuona hakuna tena magufuli?
 
Alimdamganya nini au alimshauri sawa tu. Vitisho tu vya mashtaka ila ukiwa na washauri wapigaji mnashtakiwa na kushindwa. Mbona wenyekushitaki wamefungua mashitaka baada ya kuona hakuna tena magufuli?

..kesi zilifunguliwa tangu magufuli akiwa raisi.

..magufuli aliitia nchi hasara, na alikuwa anakwenda kutuzamisha huku tukimuimbia na kumpamba.
 
Umeishaambiwa mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere umefika asilimia 90 kuisha,endelea kuwa na subira,Kila jambo lina wakati wake.
 
Yaani mnavyomshauri huyo Mama yenu ni kama vile mnadhani hayajui hayo unayoyasema. Mpaka wewe umejua hilo, unaamini kabisa huyo maza hajui? Huoni kama anaweza kuwa mnufaika? Acheni unafiki
 
Tupe ushaidi kama ni kweli gas inazalisha 70% ya umeme unaotumika nchini ? nini sasa sababu ya mgao?

Source: TANESCO strategic plan 2020-25.

nini sasa sababu ya mgao?
Sasa hili ndio swali la kuuliza sio eti ooh Bwawa linahujumiwa na blah blah zingine. Incompetence ya TANESCO ipo miaka yote tusipende Kila failure tuseme ni hujuma ya waziri fulani sijui mabeberu as if bila hujuma Kuna kitu tumewahi Fanya vizuri.

Mfano NIDA nani anahujumu?? Yaani kazi ya kuchapisha vitambulisho tushindwe wenyewe alafu lawama tupeleke kwa wasiohusika?
 
Hao wenyewe , wenye kushindwa kuongoza ni Nani,na kwanini Hawasimami ipasavyo.
Hao hao walipokuwa mazingira walisema stiggler haifai, walipo enda nishati , wakaenda kushindwa kusimamia, na kujaribu kufanya mabadiliko, ambayo sasa Tuna upungufu WA umeme sio mgao
 
wenyewe , wenye kushindwa kuongoza ni Nani,na kwanini Hawasimami ipasavyo
Hapa naongelea competence na tatizo hili ni la kimfumo. Ajira za serikali ni za kudumu hata ukiharibu unahamishwa tu taasisi so probability ya watu kufanya madudu ni kubwa akijua hamna la kumfanya lazima ufanisi uwe mdogo.

Na hii sio lawama kwa TANESCO tu ni pote angalia TTCL, TANESCO, TRA, TPA n.k kote huko ni ufanisi mdogo. So kuanza kulaumu ni hujuma au ni January ndio chanzo sio sahihi maana ripoti ya CAG ipo wazi madudu yalikua mengi wizara zote so tukiacha kushambulia personalities ndio tutatibu tatizo.
 
Na huo ndio ukweli wenyewe !!
 
Nikuulize swali. Kwa nini iwezekane vitambulisho vya mpiga kura inawezekana kuchapwa na kupewa wote umri miaka 18 waliyojiandikisha kwa muda mfupi ila watu hao hao ishindikane kuwapa vitambulisho vya taifa miaka mingi tu imepita sasa. Ukweli kuna watu wananufaika na kutokua na vitambulisho watu.
Unasema tunasingizia ubeberu kila kitu. Unafikiri tunakosea? Ubeberu unaanzia ndani kisha kujiuza kwa ubeberu wa kimataifa unaotafuta siku zote washirika. Usifikiri una akili sana kuliko sisi wenye msingi wa kufikiri kuhusu chanzo cha matatizo yetu yako nje. Kwa maoni yetu mama kavuruga nchi kuitoa kwenye njia sahihi ya kimagufuli. Uzembe wizi upigaji na hata usaliti wa nchi vimerejea kwa kasi.
 
Sijui hata kama unatuelewa. Januari alipue mabomba ya gesi kwa umeme ya kazi gani? Kwani yeye hataki huo uwaziri wa nishati? Mtu ni mpigaji atapigaje akibomoa?🤣. Simumesikia wakipanga ununuzi kufuru. Mita za papo kwa papo, kurepea mtandao wa usambazaji bilioni 11 etc etc tenda kibao... Huku umeme hakuna na bei na maharage wake wamesema hawashushi kukidhi wasia wa magufuli.🏃🏃
 
Uyo Mama atafanya nini wakati na yeye katekwa!
 
..kabudi si ndio alimdanganya magufuli sasa tunashtakiwa na kulipishwa mabilioni ya fedha? wewe unaona huyo ni mtu wa maana?
Usiongee kama Kasuku,be specific with evidence Kabudi alimdanganya Magufuli kwenye issue ipi.
Usisahau pia Katiba yetu inasema Rais halazimiki kufuata ushauri utakaotolewa na mtu yoyote,kama alimshauri hakusilizwa Je!
 
Usipayuke tu Mkuu, Katiba yetu inampa mamlaka Rais kutopokea ushauri wa mtu yeyote.Mimi naamini walishauri ila Magufuli na yeye alikuwa na maamuzi yake ya kukurupuka wakati fulani.
 
January alimuambia Bi.Mchele kuwa anataka kuifumua gridi ya taifa kwa trilioni 11![emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
..kesi zilifunguliwa tangu magufuli akiwa raisi.

..magufuli aliitia nchi hasara, na alikuwa anakwenda kutuzamisha huku tukimuimbia na kumpamba.
Kwani kufunguliwa kesi ndio kushindwa au kuzama? Sasa unataka nchi tuwe watiifu kwa dhuluma kwa kua tutashitakiwa tukichukua hatua kujinasua? Kushitakiwa ni jambo linaweza kutokea kufuatana na hao dhulumati wakiona uwezekano wa kushinda. Nchi ikiwa na wanasheria wa ovyo au wapenda rushwa utashindwa hata kama una haki.
 
January alimuambia Bi.Mchele kuwa anataka kuifumua gridi ya taifa kwa trilioni 11![emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Na Bi. Mchele akakubali🤣😂🤸💃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…