Kila Jumamosi ya kuamkia Jumapili huwa silali kwa sababu ya makelele ya makanisa

Hauko serious na usingizi , watu wanalala kweny mkesha , watu wanalala na mbuzi hao wanatafuna usiku mzika ...Yaani kelele mtu anapiga kweny eneo lake wewe unapata tabu aiseee.
 
Kuna jirani yangu alikuwa anasema hapa kwetu kuna bar basi , siku moja ya ijumaa kuamkia jmosi alisema walipiga mziki hakulala , kwa hiyo alitaka kwenda kuwashtaki kwa kingozi wa mtaa .

Nikamuuliza walikuwa wanapiga nyimbo gani? Akasema baada ya kwangaru walipiga ''bia tamu "

Nikamwambia wewe ulikuwa unasikiliza mziki ndio maana hukupata usingizi.
 
Watanzania hatuna elimu ya mipango miji,Sehemu zilizopimwa zina madaraja.

MAKAZI ONLY ,MAKAZI NA BIASHARA ,HUDUMA ZA JAMII etc kama mtu unataka kupumzika nunua MAKAZI ONLY huko hutokuta BAR ,KANISA wala MSIKITI.
Hicho kitu cha maeneo rasmi hakipo tena hapa Tz.
Eneo lolote hapa Tz unaweza kukuta hizo shughuli. Kwa sasa kuanzia Masaki, Osterbay, Msasani, Mbezi beach nk kuna makanisa, mabaa, viwanda, ofisi, night clubs na makazi ya watu. Hakuna utofauti, kila kitu kiko vurumai.
 
Ni kweli mkuu yaani hakuna hicho kitu saivi Kuna vituo vya mafuta karibu kabisa na makzi ya watu ama kumbo za starehe ni hatari
 
Hizo ndio changamoto za kukosa mipango mji, kila kitu kinafanyika mahali popote
Kwa mji kama wa Dar hilo balaa ndiyo limezidi.

Naishi Mbezi Shamba Makabe aisee kuna church moja ya mabati ipo Msakuzi (karibia 3.3 km kutoka nilipo) lakini kila siku saa kumi alfajiri nikistuka huwa naisikia ikiungurumisha sasa huwa najiuliza mimi nilie mbali kiasi hiki nawasikia vipi kuhusu wale walio jirani?ni mtihani sana serikali inapaswa kuliangalia hili.
 
Dance according to the tune....kuwa mlokole
 
Ukisikia swali lisilokuwa na kichwa Wala mguu ndo hili
 
Serkali imetutelekeza kabisa sijui wanalipwa ni shida kubwa sana
 
Unazisikia kelele kwa sababu unazipa attention
Nilitaka nimjibu hv umeniwahi,mm nikiwa na usingizi mzito naweza kulala hata juu ya hayo maspika yanayopiga kelele[emoji23][emoji23] halafu kingne yeye anazipa sana attention hzo kelele!.inatakiwa uzipuuze na hutopata nazo shida,nishawahi kupanga karibu na kanisa kwa kutokujua aisee ilikuwa noma mwanzoni kama mwezi hv nilikuwa silali lkn baada ya kuzipuuzia kelele huwezi amini zilikuwa hazinikeri!
 
We kweli maiti kwahiyo mtu anayebet alipi Kodi kweli jomo kenyatta hakukosea kukuita maiti
 
Jitathimini upya akili yako ww
 
Watanzania hatuna elimu ya mipango miji,Sehemu zilizopimwa zina madaraja.

MAKAZI ONLY ,MAKAZI NA BIASHARA ,HUDUMA ZA JAMII etc kama mtu unataka kupumzika nunua MAKAZI ONLY huko hutokuta BAR ,KANISA wala MSIKITI.
Mkuu unaandika as if wote ni matajiri au hatuijui hiyo mipango miji,ukisema nunua makazi only unataka wote tukajazane Masaki Upanga Posta maana hata hiyo Kariakoo yenyewe hakuna mipango miji.

Shida inaanza na serikali haiko active kushughulikia mapema haya mambo,iko hivi;mimi nanunua kiwanja 20x20 sehemu kabisa panaonekana ni kwa ajili ya kuishi watu lakini naweka ninachokiita Kanisa then naanza kero za kelele kwa wenzangu,mtaa una viongozi yupo balozi,yupo mwenyekiti wapo wajumbe wa mtaa na wote hizo kelele wanazisikia kwanini mapema wasimfate huyo nabii sijui muinjilisti wakamkumbusha sheria zinavyosema kuhusu anachokifanya?kwa sababu hizo kelele zinatembea mbali lakini wao kimyaa kama hamna kinachoendelea!

Kuna Misikiti na Makanisa huwezi kuhoji kwanini yapo sehemu fulani kwa sababu ukiitisha street map za makazi utakuta ni sehemu zilishatengwa kiasi wakazi ndiyo wageni lakini Makanisa mengi ya mabati huyakuti kwenye ramani za mitaa na ndiyo yanayoleta purukushani mitaani.
 
Kuna mwenzio juzi kaja na nyuzi ya kukerwa na adhana ya asubuhi kumbe ata huku nako pia
Hlf ukiangalia adhana ya alfajiri inakuamsha ujiandae na pirika zako
 
Watanzania hatuna elimu ya mipango miji,Sehemu zilizopimwa zina madaraja.

MAKAZI ONLY ,MAKAZI NA BIASHARA ,HUDUMA ZA JAMII etc kama mtu unataka kupumzika nunua MAKAZI ONLY huko hutokuta BAR ,KANISA wala MSIKITI.
Utashangaa jirani yako linajengwa kanisa au msikiti. Unafikiri haya makanisa yote na misikiti ni maeneo rasmi? Wameamua tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…