Kila la heri timu ya Taifa, Taifa Stars

Huyu jamaa kwenye upangaji wa timu ana mapungufu kiasi chake! Mpaka mheshimiwa Rais wetu Jpm anafahamu hasa kwa alichotufanyia kule Lesotho.

Muda huu na yeye Mheshimiwa atakuwa pale ikulu anasikilizia tu maumivu kama sisi wengine. Na ingekua ni amri yake, bila shaka angemtumbulia huko huko Misri! Huku sidhani kama angefika.
 
Nafahamu.
Bado sio kwa mpira tunaocheza haitoshi kujitetea.....
Ni kweli lakini hawa watu bado wanatuzidi mbali sana hata kwa uwezo wa mchezaji mmoja mmoja huo ndo ukweli
 
Kuna muda Watanzania inabidi tukubaliane na hali halisi, wachezaji wetu wengi ni wa viwango vya chini sana kulinganisha na Senegal.
Timu ina Coulibaly, Gaya, Kouyate, Balde na wengine unategemea nini hapo!?!?
Tushukuru Mungu tumefuzu kimazabe tuwe tayari kwa matokeo yeyote.
 
Senegal leo wamekua wakarimu sana yaani hawataku kutufunga mengi sana.
 
Kiwango hamna kabisa.. Kipa wa Senegal kurelax tu..mpira wa bongo magazeti. Hamna kiwango kabisa mle..tusidanganyane kwa kiwango hiki tutanusa fainali

Yaani unawaza fainali hata kushika nafasi ya pili kwenye kundi ni fainali itakuwa
 
Zaidi ya kukata viatu sijaona mpira Tanzania. Wasituumizie Mbaye Niang wetu jamani. Senegal inategemea kufika final. Mwantika anabore hadi refa aliamua kumfokea. Mwantika anachezea team gani hapa Bongo?

Yanga huyo
 
Jamaa kiwango mlima halaf wote wanakipiga yuropu.

wote warefu starz wafupi.

Mipira yote ya juu na inayotambaa yote yao
 
Hivi tukija kutana na watani zetu,jirani hapo si watatuoshea sana kama hali yetu ndio hii.
 
Mpira siku zote ni maujuzi na sio makele wala siasa. Kama huna maandalizi ya kutosha ushindi sahau. Hii ndiyo falsafa ya Mpira.
 
Nawakumbusha tu jamani

Kikosi cha SENEGAL 🇸🇳 kilichipo humo

1. Mendy - Rennes, France
2. Wague - Barcelona, Spain
3. Sabaly - Bordeaux, France
4. Sane - Shalke, German
5. Koulibay - Napoli, Italy
6. Ndiaye - Galataslay, Turkey
7. Sar - Rennes, France
8. Gana - Everton, England
9. Niang - Rennes, France
10. Diata - Bruge, Belgium
11. Keita Balde - Milan, Italy.
 
Hawa Taifa Starz niwakuchapa fimbo, wanacheza kama watoto wa shule ya msingi 😡 .
 
Kuzidiwa hata sikatai...

Namibia mwenyewe kwa Morocco kazidiwa saana.

Ila alikaza na alikuwa anaeleweka.
Ni kweli hapo tunacheza na 1 kwa soka Africa wakati sisi ni 36, hiyo timu iliyo uwanjani hapo ni mchezaji mmoja tu anaecheza ndani wengine wote ni ulaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…