Kila la heri timu ya Taifa, Taifa Stars

Fei toto.
Mwantika
Muddathir
Manula
Boko
Msuva
Samatta.
Mechi ijayo wasipobadilika. Tutegemee haya haya yaliyotokea leo
 
Kila mtu na kibonde wake , Senegal nao kombe la dunia la Russia 2018 walikuwa kama Tanzania🤔🤔🤔🤔 round ya kwanza nje
 
Mi nauliza tu, hivi wale wabunge wote waliokwenda Misri, nauli kawalipia nani? Au kodi zetu?
 
Mechi yetu ya kwanza AFCON 2019 dhidi ya Senegal huko Misri ndiyo tu imemalizika muda mfupi uliopita kwa timu yetu ya Tanzania (Taifa Stars) kuchezea kichapo cha goli 2 bila majibu.

Wote tumeona mchezo huu kupitia TV kuwa kwa zaidi ya 90% ulikuwa wa upande mmoja zaidi na bila shaka walioko huko Misri na kuuona ana kwa ana ndani ya uwanja wako very disappointed na wanaweza kushuhudia wenyewe.

Na laiti Senegal wangekuwa makini kidogo tu, ni wazi tungeweza kuchezea kichapo kikubwa zaidi cha magoli kwa idadi isiyopungua "ngumi ya mkono mmoja" ama "kidumu Chama Cha Mapinduzi"

Kwa maoni yangu naweza kusema bila shaka yoyote kuwa, tumekwenda Misri kushiriki na siyo kushindana na hivyo basi tusitegemee chochote cha maana kutoka kwa vijana wetu hawa.

Historia inaonesha kuwa kabla ya ushiriki wetu wa AFCON ya mwaka huu 2019, tumewahi tena kushiriki mashindano kama haya mwaka 1980 ambapo tuliishia katika hatua ya makundi huku tukifungwa mechi zote kasoro mechi moja tuliyoambulia droo.

Na kwa picha tuliyoiona ktk mechi hii ya kwanza tu, hata mwaka huu tutagongwa mechi zote hata ile dhidi ya jirani zetu Kenya kuna uwezekano wa zaidi ya 75% kupigwa goli za kutosha kwa sana tu

Sijaona timu ambayo iko committed kwelikweli kuchuana na timu za Algeria ya watu wanaojua wanafanya nini....

Kiukweli tulichokiona katika mchezo wa leo, ndivyo sisi sote kama taifa jinsi tulivyo.

Kwamba, tu dhaifu mno karibu katika kila nyanja iwe ni katika siasa, uchumi, elimu ama michezo ambayo ndiyo mjadala wa leo

Haieleweki hasa sababu ni nini tunashindwa kusonga mbele kwenye maeneo karibu yote huku tukiwa ni taifa kubwa lenye idadi ya watu takribani 60,000,000 na eneo la nchi la takribani kilometa za mraba zaidi ya 900,000 likiwa na kila aina ya rasrimali (natural resources) ndani yake ndani yake ikiwemo human resources

Hopefully, tatizo ni ukosefu wa UONGOZI BORA na SIASA SAFI ambazo ndizo huzaa Sera na mipango safi na endelevu kwa watu na taifa zima kwa maana ARDHI na RASRIMALI WATU kama nilivyosema wapo wa kutosha tu

Nimejaribu kuitazama na kuilinganisha nchi ya Senegal tuliyocheza nayo leo na Tanzania yetu nikagundua kuwa tunaizidi kwa mbali sana kwa rasrimali watu na ardhi

Mathalani population ya Senegal ni takribani watu milioni 16.7 tu (karibu mara nne ya Tanzania) na eneo la nchi yake ni takribani kilometa za mraba 190,000 tu (zaidi ya mara saba ya Tanzania) huku sehemu kubwa ikiwa jangwa!

Lakini wenzetu hawa wako mbali sana karibu ktk kila nyanja hususani ktk nyanja karibu zote hususani katika sanaa na michezo ambayo ndiyo mjadala wa leo..

Karibu wachezaji wao wote wanaoshiriki AFCON mwaka huu ni professionals wanaoshiriki ligi mbalimbali za kiwango cha juu huko duniani hususani barani Ulaya tofauti kabisa na sisi ambaye sana sana tunaye mmoja tu anayejulikana ingalau...

Huyu si mwingine bali ni Mbwana Samatta anayechezea moja ya club ya kulipwa kule barani Ulaya nchini Ubelgiji.

Na ndo huyo pekee tunayemtegemea afanye maajabu huko Misri. Haiwezekani hata kidogo!

Nimejiuliza sana hivi tuliwezaje hata kufuzu kwa kiwango kile tunachocheza hata kwenda kwenye mashindano haya?

Nikagundua kuwa ni kwa kutumia njia zilezile za ujanja ujanja ule ule tunaotumia ktk maeneo mengine kama vile "kushinda chaguzi za kisiasa kwa kishindo" huku tukijua kabisa mtu ameshinda kwa wizi tu wa kura na siyo kwa sababu "SMART" Sera na mipango thabiti.

Angalia tu, kuwa, Taifa Stars ilifuzu si kwa sbb tuna "sustainable plans" bali ni kutokana na mipango ya zima moto ya muda mfupi chini ya kina Albert Bashite a.k.a Christian Makonda Malyangili RC wa DSM ya kwamba njooni mshangilie timu na ikishinda watu wote mtakunywa pombe (bia) kilevi bure!!

Sasa matokeo yake ndiyo nayo. Tumekwenda Misri tukiwa tumelewa pombe kwenye nafsi na akili zetu!!

Kupitia mchezo wa leo imeonesha wazi kuwa vijana wetu hawana energy, creativity pamoja na exposure..

Jamani mambo haya tukubali tu kuwa hayaji kwa ujanja ujanja kama wa kuiba kura ktk chaguzi za kisiasa kunakofanywa na CCM kila uchaguzi ili tu waendelee kuwa madarakani huku kukiwa hakuna sera na mipango thabiti ya kuendeleza sekta ya michezo

Namalizia kwa leo kwa kusema tena ,kuwa, tulichokiona leo huko Misri, ndiyo picha halisi ya jinsi tulivyo kama Taifa na nchi chini ya serikali inayoongozwa na CCM kwa takribani miaka 58 sasa tangu Uhuru 1961!!
 
[emoji23][emoji23][emoji23]stars walikua wanasakiziana mipira kuogopa lawama kikufia niwewe huko
 
Niliwahi andika humu(kulingana na mtazamo wangu) kuwa kuna ushahidi wa kimazingira unaoonyesha kuwa kadri unavyoenda kaskazini mwa bara hili la Afrika,basi hata ubora wa binadamu nao unaongezeka kwa maana ya akili,maarifa,rangi,ubunifu,maendeleo,n.k.but with some few exceptions.

kumbuka Afrika Kaskazini ndio wanapakana/wanakaribiana na nchi za ulaya(zenye maendeleo) na nchi hizi za Afrika kaskazini ndio zimetuzidi kwa mambo mengi kwani hata katika soka, ni nchi hizi za Afrika Kaskazi/Afrika Magharibi ndio ziko juu kisoka na ndio zinatoa wacheza wengi kwenda kucheza soka ulaya tofauti na huku kwetu kusini mwa jangwa la sahara.

I believe Nature is responsible here.
 
Senegal piga hao nzi wa kijani wa Stars. Pole pole alisema Stars wakishinda ni matokeo ya utekelezaji wa sera za ccm namsubiri tufungwe nione atasema stars wanatekeleza sera ya nani
Ha ha haaaaaa......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…