Kila mauaji hushuhudiwa na macho matano

Kila mauaji hushuhudiwa na macho matano

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tunamaliza mwaka 2019 na taharuki za kutisha na kutosha. Kwa akili za wastani ni rahisi sana kuwanyooshea vidole wengine lakini kiroho tafsiri ni kubwa kuliko hilo.

Mojawapo ya 'case sensitive ' kwa binadamu ni kifo cha mauaji. Kifo cha dhamira. Hivi huacha fadhaa na maswali mengi yasiyo na majibu kwa wengi. Kifo cha mauaji ya dhamira huwa ni jambo la siri kubwa. Hivyo usipokuwa mahiri kwenye uchunguzi utaishia kufeli.

Wenzetu waliotutangulia kufikiri waliamua kuachana na dhana za kifo ni kazi ya Mungu... Wakiamini kabisa kila kifo cha mauaji ya dhamira hupangwa na kuna macho matano huona... Ni katika hayo macho matano utata wa mauaji husika hutatuliwa..

Ukiachana na macho ya BINADAMU, vitu navyo vina macho lakini yasiyoonekana
Majengo yana macho
Muda una macho/ mawasiliano
Silaha zina macho
Vyombo na mitambo na machine vina macho
Barabara zina macho
Mapori, maji milima mabonde misitu nknk... Kila kitu kina macho...

Vifo vya mauaji ya dhamira ya kupangwa huwa na macho muhimu matano
1. Macho ya eneo mauaji yalipofanyika.
2.silaha zilizotumika
3. Muda /mawasiliano
4.Muuaji/wauaji
5. Muuliwa/ Mhanga
Mipango mingi ya mauaji hupangwa na binadamu asiye mkamilifu... Hivyo kwa asilimia 95 ni lazima ataacha kiashiria onwa ambacho kikitumika vizuri.. Kitafumbua fumbo la mauaji husika...

1. Eneo la mauaji yalipofanyika.. Tambua kwanini huzunguushiwa uzio maramoja... Hapa ni kwa ajili ya kulinda ushahidi.. Hapa hukusanywa kila kitu kidogo ambacho kiasili hakikupaswa kuwepo pale

2.silaha zilizotumika /iliyotumika ukiachana na vitu kama bunduki na sumu (ambavyo ni traceable) kuna visu kamba mikono nk. Wataalam huweza kukwambia kwa hakika hiyo ni silaha ya aina gani iliyotumika na mtumiaji ni mahiri ama la...

3.Muda husema mengi. Muda roho ilipoacha mwili. Mawasiliano ya mhanga na wauaji nknk

4. Muuaji/wauaji... Hawa hukamatika kufuatilia clued za japo juu na hii moja ya mwisho hapa chini

5.Muuliwa... Unajua kwanini wengi huuliwa kwa nyuma? Macho ya Muuliwa huhifadhi picha za matukio ya mwisho kabla ya kukata roho na ndio sababu wengi kutobolewa macho..

Kwa wenzetu waliotutangulia kufikiri wameongeza macho mengine kurahisisha ufanisi... Camera za siri na tracking devices zilizofichwa sehemu mbalimbali mpaka hata mwilini...

Mkurugenzi wa taasisi moja ya kidini na mmiliki wa shule amekutwa ofisini kwake akiwa kauliwa.. Kuna maswali muhimu ya kujiuliza

. Ofisini yuko peke yake? Ama wauaji walitegea akiwa pekeyake?
. Hana mawasiliano ya kawaida na watu wengine? Maana mwili uligunduliwa baada ya siku tano kupita...
. Hana marafiki wa kumtafuta walau kwa siku ambazo alikuwa haonekani?
. Hana familia? Kwamba baba leo jajarudi au kama imesafiri hakukuwa na mawasiliano kwa siku 5 mfululizo?
. Dhamira ya mauaji huwa ni jambo la muhimu pia.. Lakini pia wauaji mahiri hutumia historia na mazoea ya mtu kufanisha mauaji salama na kadiri muda unavyopita ndio baadhi ya yale macho matano hupoteza uwezo wake

Jr[emoji769]
 
Kwa wenzetu waliotutangulia kuona mbali macho yote matano kila moja huwa na wataalam wake rasmi tena wabobezi.. Mchanga/udongo kidogo tu usioendana na na ule wa eneo husika huwa ni break through kubwa sana
Leso iliyosahaulika, nyayo za viatu, kichungi cha sigara, alama za vidole nknk.. Ni clues muhimu sana kwenye kupata ukweli

Jr[emoji769]
 
.
journal-of-forensic-psychology-flyer.jpeg

Jr[emoji769]
 
Kwa wenzetu waliotutangulia kuona mbali macho yote matano kila moja huwa na wataalam wake rasmi tena wabobezi.. Mchanga/udongo kidogo tu usioendana na na ule wa eneo husika huwa ni break through kubwa sana
Leso iliyosahaulika, nyayo za viatu, kichungi cha sigara, alama za vidole nknk.. Ni clues muhimu sana kwenye kupata ukweli

Jr[emoji769]
Vipi hatujaweza kutumia ubongo wa aliyejeruhiwa kupata taarifa sahihi?

Maana kwa sasa wanatoboa macho ili kuficha ushahidi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kumuua sheikh inahitaji moyo.....
 
Mimi natafuta nyumba ya kupanga, kwa yotote atakaye kufa kwa maana siku hizi nyumba kazi sana kupata, hasa maeneo ya Sinza au Kinondoni, hivyo ukisikia mtu amekufa na kuacha nyumba ya kupangisha nishtue angalau wengine nyumba za kuishi pia, natanguliza shukrani zangu.
 
Mkuu umewahi kuangalia Chanel ya Discover Investigation ??

Very interesting

Back
Top Bottom