Kila mauaji hushuhudiwa na macho matano

Kila mauaji hushuhudiwa na macho matano

Kuna siku nilitoka kumsindikiza wife stand pale shekilango, wakati narudi nikaona nikatize ile njia ya makaburini ilikua mida ya saa 1 asubuhi, njiani nikakuta watu wengi wanashangaa damu zilizomwagika nikasogea kuuliza kilichotokea nikaambiwa alfajiri kulikua na mapambano ya polisi na majambazi, wakati tupo pale akaja bwana mmoja alikua na pikipiki aina ya boxer alikua kavalia kanzu na kafunga kilemba alivyofika akaangalia akaona ganda la risasi na lilikua moja tu akaliokota akarudi kwenye pikipiki akawasha na kuondoka.


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kuna siku nilitoka kumsindikiza wife stand pale shekilango, wakati narudi nikaona nikatize ile njia ya makaburini ilikua mida ya saa 1 asubuhi, njiani nikakuta watu wengi wanashangaa damu zilizomwagika nikasogea kuuliza kilichotokea nikaambiwa alfajiri kulikua na mapambano ya polisi na majambazi, wakati tupo pale akaja bwana mmoja alikua na pikipiki aina ya boxer alikua kavalia kanzu na kafunga kilemba alivyofika akaangalia akaona ganda la risasi na lilikua moja tu akaliokota akarudi kwenye pikipiki akawasha na kuondoka.


Sent from my iPhone using Tapatalk
Alikuja kupoteza ushahidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji44]ushahidi muhimu sana ulipotezwa
Kuna siku nilitoka kumsindikiza wife stand pale shekilango, wakati narudi nikaona nikatize ile njia ya makaburini ilikua mida ya saa 1 asubuhi, njiani nikakuta watu wengi wanashangaa damu zilizomwagika nikasogea kuuliza kilichotokea nikaambiwa alfajiri kulikua na mapambano ya polisi na majambazi, wakati tupo pale akaja bwana mmoja alikua na pikipiki aina ya boxer alikua kavalia kanzu na kafunga kilemba alivyofika akaangalia akaona ganda la risasi na lilikua moja tu akaliokota akarudi kwenye pikipiki akawasha na kuondoka.


Sent from my iPhone using Tapatalk

Jr[emoji769]
 
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji44]ushahidi muhimu sana ulipotezwa

Jr[emoji769]

[emoji15][emoji15] duuuh, mimi ilinistua kidogo ila wengine waliona kawaida, kwa wakati ule nilikariri hadi plate number ya pikipiki ila nikapata wasiwasi na hawa jamaa zetu maana hawatabiriki.


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Nimekuelewa mshana, time will tell
Tunamaliza mwaka 2019 na taharuki za kutisha na kutosha. Kwa akili za wastani ni rahisi sana kuwanyooshea vidole wengine lakini kiroho tafsiri ni kubwa kuliko hilo.

Mojawapo ya 'case sensitive ' kwa binadamu ni kifo cha mauaji. Kifo cha dhamira. Hivi huacha fadhaa na maswali mengi yasiyo na majibu kwa wengi. Kifo cha mauaji ya dhamira huwa ni jambo la siri kubwa. Hivyo usipokuwa mahiri kwenye uchunguzi utaishia kufeli.

Wenzetu waliotutangulia kufikiri waliamua kuachana na dhana za kifo ni kazi ya Mungu... Wakiamini kabisa kila kifo cha mauaji ya dhamira hupangwa na kuna macho matano huona... Ni katika hayo macho matano utata wa mauaji husika hutatuliwa..

Ukiachana na macho ya BINADAMU, vitu navyo vina macho lakini yasiyoonekana
Majengo yana macho
Muda una macho/ mawasiliano
Silaha zina macho
Vyombo na mitambo na machine vina macho
Barabara zina macho
Mapori, maji milima mabonde misitu nknk... Kila kitu kina macho...

Vifo vya mauaji ya dhamira ya kupangwa huwa na macho muhimu matano
1. Macho ya eneo mauaji yalipofanyika.
2.silaha zilizotumika
3. Muda /mawasiliano
4.Muuaji/wauaji
5. Muuliwa/ Mhanga
Mipango mingi ya mauaji hupangwa na binadamu asiye mkamilifu... Hivyo kwa asilimia 95 ni lazima ataacha kiashiria onwa ambacho kikitumika vizuri.. Kitafumbua fumbo la mauaji husika...

1. Eneo la mauaji yalipofanyika.. Tambua kwanini huzunguushiwa uzio maramoja... Hapa ni kwa ajili ya kulinda ushahidi.. Hapa hukusanywa kila kitu kidogo ambacho kiasili hakikupaswa kuwepo pale

2.silaha zilizotumika /iliyotumika ukiachana na vitu kama bunduki na sumu (ambavyo ni traceable) kuna visu kamba mikono nk. Wataalam huweza kukwambia kwa hakika hiyo ni silaha ya aina gani iliyotumika na mtumiaji ni mahiri ama la...

3.Muda husema mengi. Muda roho ilipoacha mwili. Mawasiliano ya mhanga na wauaji nknk

4. Muuaji/wauaji... Hawa hukamatika kufuatilia clued za japo juu na hii moja ya mwisho hapa chini

5.Muuliwa... Unajua kwanini wengi huuliwa kwa nyuma? Macho ya Muuliwa huhifadhi picha za matukio ya mwisho kabla ya kukata roho na ndio sababu wengi kutobolewa macho..

Kwa wenzetu waliotutangulia kufikiri wameongeza macho mengine kurahisisha ufanisi... Camera za siri na tracking devices zilizofichwa sehemu mbalimbali mpaka hata mwilini...

Mkurugenzi wa taasisi moja ya kidini na mmiliki wa shule amekutwa ofisini kwake akiwa kauliwa.. Kuna maswali muhimu ya kujiuliza

. Ofisini yuko peke yake? Ama wauaji walitegea akiwa pekeyake?
. Hana mawasiliano ya kawaida na watu wengine? Maana mwili uligunduliwa baada ya siku tano kupita...
. Hana marafiki wa kumtafuta walau kwa siku ambazo alikuwa haonekani?
. Hana familia? Kwamba baba leo jajarudi au kama imesafiri hakukuwa na mawasiliano kwa siku 5 mfululizo?
. Dhamira ya mauaji huwa ni jambo la muhimu pia.. Lakini pia wauaji mahiri hutumia historia na mazoea ya mtu kufanisha mauaji salama na kadiri muda unavyopita ndio baadhi ya yale macho matano hupoteza uwezo wake

Jr[emoji769]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wenzetu waliotutangulia kuona mbali macho yote matano kila moja huwa na wataalam wake rasmi tena wabobezi.. Mchanga/udongo kidogo tu usioendana na na ule wa eneo husika huwa ni break through kubwa sana
Leso iliyosahaulika, nyayo za viatu, kichungi cha sigara, alama za vidole nknk.. Ni clues muhimu sana kwenye kupata ukweli

Jr[emoji769]
Umesoma sana James Hadley Chase.

Hapo kwenye sample ya udongo ambao sio wa sehemu husika, umenikumbusha novels za huyo mwandishi juu.

Hongera kwa kupata maarifa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa kufeli kwa moyo na kukosa msaada wa haraka wa matibabu, ndiyo chanzo cha kifo cha Sheikh Rashid Bura, ambaye ni mmiliki wa shule za Zamzam mkoani humo.

Kamanda Muroto amebainisha hayo leo Disemba 27, 2019, na kusema kuwa mara baada ya kupata taarifa hiyo, Polisi walifika eneo la tukio na kwamba hawakukuta viashiria vyovyote vya mauaji, badala yake uchunguzi umebainika kuwa alifariki baada ya kukosa msaada kwa kuwa hali hiyo ilimkuta ofisini akiwa peke yake.

"Taarifa za kiuchunguzi za awali zinaonesha kifo chake kimetokana na kufeli kwa moyo na kwakuwa alikuwa ofisini kwake hakupata msaada na simu yake ilikuwa imezima ndugu zake walishindwa kumpata na ofisini tulikuta kupo salama na hakukuwa na wizi wowote uliofanyika" amesema Kamanda Muroto.

Kwa mujibu wa Kamanda Muroto, mwili wa Bura uligundulika siku ya Disemba 25, 2019, na kuwataka waandishi wa habari, kuacha kusambaza taarifa ambazo wanakuwa hawajazithibitisha kutoka kwenye vyanzo halisi likiwemo Jeshi la Polisi ama kwa Daktari

FAMILIA YATOFAUTIANA NA POLISI

Ali Rashid Bura (26), mtoto wa marehemu na msemaji wa familia ya marehemu, Abdillah Mboryo wamesema mwili wa marehemu ulikutwa ofisini kwake bila nguo huku ukiwa na makovu matatu mkono wa kushoto, kwenye paja na mgongoni.

Mtoto wa marehemu amesema baada ya kumtafuta baba yake maeneo mengine bila mafanikio, alikwenda ofisini kwake na kukuta mlango ukiwa umefungwa na alipoufungua kwa kuupiga teke ulifunguka.

“Ndipo nikauona mwili wa baba ukiwa umeharibika sana huku akiwa amekaa chini na nguo zote zikiwa pembeni,” anasema kijana huyo.

Naye Mboryo alisema: “Mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha matatu; mkono wa kushoto, kwenye paja na mgongoni ambayo siwezi kuyazungumzia kwa sababu mimi si polisi lakini niliyaona.”

Jr[emoji769]
 
Kuna indicators zinaanza kuwaka
1. Taarifa ya polisi nayo ni tata. Mtu aliyekosa msaada kifo chake kikoje!?
2. Kamanda anasema simu ya marehemu ilijizima kwa kukosa chaji, je iliyozimwa ikoje?!
3. Fedha zote ziko intact hazikuibea, afande atueleze je marehemu kama alikuwa na milioni zikachukuliwa laki nane zikabaki hizo intact anaushahidi gani Kiasi cha fedha alizokuwa nazo marehemu kabla ya mauti.
4. Afande kwanini anatofautiana na familia ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kuwasili pale ofisini?
5. Maiti ilikutwa imekaa chini, hivi ilikutwa imelala au imekaa?

Je umri wa maafande wetu wanael mewa hadi kushindwa kutafakari incidents Kama hizi, anatoa conclusion rahisi rahisi tu.
RIP
Afande mroto ameshahitimisha hili la kifo cha huyu muislam hapo dodoma. Moyo ulizimika.

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr[emoji769]
 
[emoji15][emoji15] duuuh, mimi ilinistua kidogo ila wengine waliona kawaida, kwa wakati ule nilikariri hadi plate number ya pikipiki ila nikapata wasiwasi na hawa jamaa zetu maana hawatabiriki.


Sent from my iPhone using Tapatalk
Kuna watu wameumbwa kutunza siri.
Wengine wamefundishwa kutunza siri
Hao wasipopanga kusema wanasahau
Wanasahau hata mambo yao binafsi
Wengi wanapatikana Usalama wa Taifa
Wapo sana illa hawajulikani kiuhalisia
Kwa kuwa hatujui lengo lao kiusahihi
Tumeishia kuwapachika majina hovyo
Mara wasiojulikana na watekaji watu
Tunakosea sana na kupoteza kiungo
Ndio! Kiungo muhimu na serikali yetu
Tumebaki tukilitambua Jeshi la Polisi
Ambao ni wachache watunzao siri
Kwao siri ni mpango wa kupata pesa
Waungwana ukiona siri ya usalama
Watafute Watu wa USALAMA WA TAIFA
Ila wana maswali kuliko maswali yote
Lengo kumiliki habari ili asikuhitaji tena
Tufanze hivyo kulinda mali na nchi yetu

Bazazi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom