Ujumbe ni kwamba umekuwa 'zebaki' - you can be any form, tofauti na zamani. Then, kuwa na hamsini zako as you wish kama unadhani hiyo ndiyo njia uliyoichagua. Kuna makosa mengi tunafanya, tusidhani "hana shida, atanielewa tu." Huo ndio mwanzo wa tatizo. Kwa wenye ndoa, ukianza kuona ukali unazidi kwa watoto, ujue something is not right somewhere. Haiwezekani wakati mwingine watoto mliowatafuta miaka nenda rudi, all of a sudden wawe wa kutukanwa, kuamrishwa wafanye hiki au kile na kupigwa - asubuhi, mchana na jioni - na kila siku! Hapo shida si kwa watoto, shida Iko sehemu nyingine na watoto wanakuwa tu 'scapegoat'.