Kila mmiliki wa Nissan Murano ana story ya kusimulia...

Nissan ni magari ya ajabu Sana, jamaa yangu hapa Kariakoo ameagiza nissan X trail ya 2016 na imeshakufa gear box ndani miezi miwili Tu.
CVT transmission za nissan ni majanga matupu , Kwa mfano hiyo nissan Murano ya 2003 ni matatizo Tu ya kujitakia kama unamiliiki
 
Gari ni matunzo, kama huwezi kulihudumia gari lako, nakushauri ununue baiskeli tu

Kuna mdau hapo juu ameeleza changamoto ya Mitsubishi, Mimi natumia kwa miaka mingi sasa na sijaona changamoto zake

Useme nazingatia service, Kila baada ya miezi 2 lazima nipeleke garage ili walichunguze chunguze maana napenda kutumia kusafiri nalo safari za mbali
 
Mfanya biashara wa yadi ya magari wa bongo anaagiza gari kutoka Asia limetembea kilomita laki 4 kasoro...
Analeta yadi anarudisha nyuma mileage inaonekana ni kilomita 50,000 imeenda, mbongo ananunua anatembea nalo miaka miwili, anamuuzia mwenzake, mnunuzi kwa kutozingatia matunzo gari linaharibika... mnunuaji wa mwisho anaanza kutangaza habari kila kona 'gari flani ni bovu sana'... 'usinunue gari flani ni mabovu sana hayo magari'...

Mimi hizi story za kusema gari flani ni bovu ni vyema huyo anayesema aje na uthibitisho hapa kwamba alinunua 0 kilomita kutoka Japan halafu likaharibika mikononi mwake... tofauti na hapo siwezi kuchukulia serious....

Gari zenyewe wabongo wengi wanaomiliki, kuanzia Japan hadi bongo gari imemilikiwa na watu watatu ama wanne tofauti....

Hio Nissan kuna mtu anayo, anakwenda nayo shamba na anabebea mizigo, sijawahi kuona analalamika shida yake, alikuwa na Nissan na amenunua tena hio hio Nissan zote Murano ila model year tofauti, ikiwa na maana ana experience nazo nzuri hizo gari....
 
Itoshe kusema kwamba wamiliki wengi wa magari hapa nchini hawakuwa bado na uwezo wa kumiliki gari na kulihudumia. Watu wanalalamika sana. Mara unywaji wa mafuta mara hivi mara vile. Kama unaona hali bado haijatengemaa kwenye kipato kuwa na subira tengeneza stable cashflow kwanza.
 
Umesema sahihi Mkuu, changamoto tunanunua gari second hand tena humuhumu show room zetu

Ila gari ukiagiza Japan moja kwa moja, haliwezi kusumbua ukizingatia service
 
Nissan Juke hazizungumzwi sana kama kaka zake Murano,X trail na sasa Dualis.

Ni kwamba hazisumbui or? Na resale value yake siyo mbaya.
 
Nissan Murano tatizo mtu katoka kumiliki Toyota ghafla kahamia Nissan Nissan inahitaji matunzo sana. Kama Subaru lakini watu wananunua tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…