Kila mmiliki wa Nissan Murano ana story ya kusimulia...

Hizi story zina kaukweli! Mfano ni Nisan xtrail. Huwezi sikia hizo mambo kwa Toyota karibu aina zote
 
Tunaona mitandaoni mafundi wazungu wanasema gari nzuri zinazodumu ni TOYOTA. Mkazi wa Pugu unatuambia gari ni matunzo. Tumsikilize nani?
Sasa watu wote nchi nzima tutanunua Toyota jamani? Sasa hii itakua nchi au branch ya Toyota! Wengine tunapenda variety hata kama zina matatizo tunapambana nayo na hatulalamiki!

Hizo Toyota zenyewe sio kwamba ndio hazisumbui, kuna watu zimewapiga kitu kizito hawataki ata kuzisikia.
 
Hizi story zina kaukweli! Mfano ni Nisan xtrail. Huwezi sikia hizo mambo kwa Toyota karibu aina zote
Nadhani Nissan zina namna yake ya kuzitunza tofauti na toyota..

Hili suala la kulinganisha kila gari na toyota sijui wabongo tulitoa wapi...

Toyota zenyewe zilizopo nyingi ni za 2008 kurudi nyuma...

Latest toyota za sasa nazo zinahitaji matunzo kama gari za kizungu...
 
10 kwenye buku. Wakati Nissan ni 200 kwenye buku.
 
Inaitwa makapi ya Nissan
Baada ya kupepeta ikatoka hiyo
 
Hii gari Roma (msanii) aliwahi pandishwa ilikuwa na sunroof miaka hiyo ya kiza awamu ya kwanza ya Jakaya Ukumbi ambassador pub Geita mji ulizizimaa
Kumbe inafaa kwa kamupeni kabisa
 
Ndoto yangu ya land lover iko pale pale
Yale Yale!!!
Gari niliyojifunzia ilikua Land Rover 109, japo zilivuma kama ni gari imara kiuhalisia zilikuwa gari sumbufu sana,nayajua matatizo ya hizo gari kuanzia ukoko had matandu
Honestly matatizo mengi ya 109 nayaona Hadi Leo kwenye land Rover hizi latest,
They are not reliable
 
UMenikatisha tamaa.Nilitaka kununua mitsubish outlander plug in
Mjomba, usikubali kukatishwa tamaa kirahisi hivi. Sisi wengine hayo magari hatujawahi kumiliki. Tunasikia tu malalamiko ya hapa na pale.

Wakati mwingine unaweza kuta baadhi ya magari yanaonekana ni majanga kwa sababu ya ukosefu wa mafundi sahihi, kutozingatia masuala ya service, nk. Mfano hiyo Mitsubishi Outlander mbona iko poa tu na watu wanamiliki?
 
Murano first generation ukifanya service vizuri haina shida. Inafaa watu wa safari ile Vq35 kwenye mafuta sio economy ila haina shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…