Kila mmoja akitimiza wajibu wake atakuwa amesaidia kujenga nchi nzuri

Kila mmoja akitimiza wajibu wake atakuwa amesaidia kujenga nchi nzuri

Joined
May 30, 2020
Posts
67
Reaction score
108
Uchaguzi Mkuu wa 6 kwa mfumo wa Vyama Vingi Tanzania utafanyika tarehe 28/10/2020 siku ya Jumatano na kwa Mara ya kwanza unafnayika siku ya Kazi ambayo kwa umuhimu wake Serikali imeaamua kuifanya siku hii ya Uchaguzi kuwa ya Mapumziko--hili linahitaji Pongezi nyingi sana maana litaleta hamasa kubwa kwa Wapiga Kura kujua kuwa linakwenda kufnayika tendo takatifu la kuutafuta Viongozi wetu

Kabla ya UCHAGUZI kila Chama hupita kwa wananchi kuuza ilani yao MKATABA WA JAMII (Social Contract) ili wawee kuchaguliwa; na wakishinda kwa kura huunda serikali ambayo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ibara ya 8(a-c) mamlaka hutoka kwa Wananchi na Serikali huwajibika kwa wananchi na sio wananchi kuwajibika kwa serikali--- hii ndio maana ya MKATABA WA JAMII-Social contract;

Kampeni za UCHAGUZI Mkuu zilianza taehe 28/8 na zitahitimishwa 27/10 baada ya siku 60 za kuuza maneno kwa wananchi;

Kwa nini nimeandika "Kama kila mtu akitimiza wajibu wake atakuwa amemsaidia Rais Magufuli kushinda badala ya kujipendekeza pendekeza bila sababu?

Kati ya mambo yanayohitahi PONGEZI ni Jinsi NEC ilivyoandaa Maadili yanayozuia Matumizi ya RASILIMALI ZA SERIKALI kwa maslahi ya Kisiasa ya Upande 1 maana kulikuwa na uwezekana wa kufaya hivyo; sasa kuna wimbi la watu kujipendekeza ili waonekana kuwa wanamuunga Mkono Mgombea angalau kama atashinda aweze kumkumbuka katika ufalme wake;

(1) Unamkuta Mwl Shule ya Msingi au Sekondari badala ya kuwafundisha wanafunzi vizuri wakafaulu vizuri, Yeye anatamani kuvaa sare za wagombea UDIWANI ili akishinda amsaidie kuteuliwa kuwa MWL MKUU /HEADMASTER; hili nimelishuhudia kabisa na Mwl anakuambia bila hivyo mwanangu nitafia ubaoni

[2] Nurse au Daktari anatakiwa kuwepo katika kituo chake cha Kazi - iwe Zahanati,Kituo cha Afya, Hospital ya WIlaya/Mkoa na sio kutaka kufanya siasa ama muda wa Kazi au baada ya masaa ya kazi kwa lengo la kutaka kuonekana kwa Wagombea kwa ahadi ile ile ya kusaidiwa kuwa Incharge wa Kituo,DMO,RMO, Mratibu wa Mradi nk--hii itakuwa sio sahihi

[3] Mtumishi wa Serikali anayekaa Ofisini anatakiwa kuwahudumia wananchi vizuri ili waridhike na huduma na sio kutaka kujipendekeza kwa wagombea ili wakishinda nao wamsaidie kuwa Mkurugenzi Msaidizi, Katibu Tawala au Nafasi yeyote-- hii sio sawa, kila Mtu afanye kile ambacho anapaswa kufanya bila kutegemea kupata rewards yeyote au asante. Mtu anayehusika na kuwalipa wastaafu Mafao yao, anatakiwa atende jinsi inavyotakiwa na sio wastaafu wanakaa miezi hadi 5 wanasubiria pensheni-huku wewe unataka kuvaa sare za siasa ili Mgombea Ubunge naye akuone akukumbuke kama atakuwa Waziri--Hiy nayo ni ubatili pia

(4) MaDC,RC,RAS.KM, DAS,DED, HoD au Wakuu wa Taaisis wanatakiwa kutenda HAKI na kuondoa upendeleo mahala pa Kazi, kuwatendea vile ipasavyo watumishi walioko chini yao ili nao waridhike na kupunguza malalamiko kwa SERIKALI lakini kama nao watataka kufanya siasa na kujipendekeza ili waendelee au wabakie kwenye NAFASI zao, watakuwa wanakwenda kinyume kabisa na matarajio ya serikali au NEC kwa sababu Maadili ya Uchaguzi yanasema kuwa Serikali itaendelea na majukumu yake bila kuonyesha upendeleo kwa chama au Mgombea yeyote; Kama kila MTU aliyepewa Ofisi ya UMMA atatenda jinsi inavyompasa, malalamiko na manung'uniko kwa wananchi au watumishi yatapungua sana;
sasa wewe DC unataka kuonyesha mapenzi na mahaba kwa Mgombea Ubunge ili akishinda akukumbuke kufanyaje wakati naye anawaza namna ya kukumbukwa na kupata unaibu waziri?

(5) Endapo kila Mtu aliyepewa Nafasi ya Utumishi ama wa UMMA au kwa sekta binafsi atatenda kwa mujibu wa sheria na Kanuni za uendeshaji wa taasisi, wananchi watafurahia matunda ya utumishi na serikali ya chama chochote itapata credibility kwa wananchi na kwa Mungu pia. Mwl wa shule ya Kanisa ya English medium, anatakiwa kutenda haki kwa wanafunzi wote na sio kujipendekeza kwa mtoto wa DEO/REO ili aweze kumsaidia kupangiwa ajira serikalini; Ni muhimu zaidi kila mtu akafnaya kile ambacho anapaswa kukifanya na sio kujenga UTAMADUNI mpya wa kujipendekeza pendekeza na hatimaye huzalisha mfumo wa rushwa rushwa katika jamii.

(6) Mgombea wa CHAMA chochote kitakachoshinda uchaguzi na kuunda serikali iwe ni ACT,CUF,CCM,CDM au ADC, anatakiwa kutumia Ofisi ya Umma kwa kutenda Haki hasa kama atafanya UTEUZI wa Nafasi Nyeti za Kikatiba kama KARIBU MKUU KIONGOZI, AG, UWAZIRI MKUU,UWAZIRI, NAIBU WAZIRI,DPP,CAG, RC,DC,DAS,MAKATIBU WAKUU,au nafasi yeyote afanye hivyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za Nchi na sio kwa mapenzi yake tu; Jaji mmoja wa Uingereza aliwahi kusema kuwa "Hakuna mtu mwenye hekima/busara kuliko sheria"; na uteuzi wowote ukiwa makini kila mtu ataona kuwa huyu amestahili na kupata baraka za Mungu;

Tuepuke kujeng Nchi ambayo vijana wanaosoma VyuoVikuu wanaamini kuwa huwezi kupata Kazi bila kujipendekeza au kufahamiana na watu;

Tanzania itaendelea kuwepo hata baada ya 2020-2025,
Mungu ibariki Tanzania na watanzania wote
 
Back
Top Bottom