Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 384
- 758
Miaka kadhaa iliyopita, wakati tukiwa mdogo na marafiki zangu wengi , miongoni mwa rafiki yangu wa karibu sana huyu ndugu yangu wote tumezaliwa mwaka mmoja tofauti ni tarehe na miezi,
Tulifanikiwa kusoma shule za mzingi pamoja ingawa kila mmoja alisoma shule yofauti ila tulikuwa madarasa yakufanana, rafiki yangu huyu alitoka kwenye familia bora wazazi wake walikuwa ni watu wakubwa tu ofisi za umma
Matokeo ya darasa la saba yalipotoka bahati mbaya sikufanikiwa kuchaguliwa kujiunga elimu ya sekondari ya serikali, na bahati nzuri rafiki yangu yeye alichaguliwa, kitendo ambacho kilinisikitisha kwa wakati ule kwamba kwanini mimi sikuchaguliwa?
Kutokana na uwezo wa wazazi wa ndugu yangu huyu na shule aliyochaguliwa walikataa kumpeleka shule ile ambayo ilikuwa ya bodii ambayo ilikuwa wilayani huko
Wazazi wake walimchagulia shule ya sekondari ambayo ilikuwa mkoani Mwanza kwa kipindi kile ni miongoni mwa shule za private ambazo zilikuwa ni bora
Nawashukuru wazazi wangu wanilipelekea shule ya private pia tukaanza masoma ya sekondari, baada ya miaka 4 kukamilika matokeo ya sekondari yalitoka mimi nilifanikiwa kupata matokeo ya kuniwezesha kuendelea na kidato cha 5 na 6 lakini mwenzangu hakufanikiwa.
Nilifanikiwa kuendelea na shule ya serikali kwa maosomo ya kidayo cha tano na sita lakini mwenzangu hakufanikiwa. Hivyo alianza mchakato wa kutafuta sifa za kujiunga na kidato cha 5 na 6
Rafiki yangu alirudia mithani wa kidato cha 4 kupata sifa za kuendelea na kidato cha sita yaani credit 3 za kumwezesha kuendelea na masomo
Mwaka wa kwanza wa kurudia hakufanikiwa, mwaka wa pili aliporudia pia hakufanikiwa.
Miaka yote hiyo miwili mimi nilifanikiwa kumaliza elimu ya kidacho cha sita na kuendelea na chuo, rafiki yangu huyu hakukata tamaa akarudia tena kwa mwaka wa tatu , Mungu sio athumani akafanikiwa kupata sifa za kuendelea na kidato cha tano
Akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita kwa mfumo wa binafsi yaani QT akafanikiwa kumaliza elimu ya kidato cha tano na sita kwa miaka 2
Mara baada ya kumaliza elimu yake ya kidato cha sita nilikuwa mwaka wa kwisho wa chuo, rafiki yangu alifanikiwa kupata chuo kikuu akaendelea na masomo.
Akiwa mwaka wa kwanza wa chuo nilifanikiwa kumaliza elimu yangu ya chuo na kufanikiwa kupata kazi
Miaka ikaendela ndugu yangu huyu akamaliza chuo, na mara baada ya kumaliza chuo hakufanikiwa kupata kazi.
Alitafuta kazi bila kuchoka , wakati anaendelea na masomo nilifanikiwa kufunga ndoa na kupata watoto, ndugu yangu huyu akiwa bado anatafuta kazi.
Alitafuta kazi mwaka 1, mwaka 2 , mwaka 3, 4 , 5 na mwaka 6, Mungu sio athumanj ndugu yangu huyu akafanikiwa kupata kazi , na Mungu akamlatia mke na familia kwa kipindi kifupi tu.
Siku zote na mara nyingi tunaishi kwa kujiringanisha na watu, badala ya kujiringanisha na Mungu.
Kuna neno moja ambalo lilinichukua miaka mingi kulieelewa kila nilipokuwa nasoma biblia sikuwai kulielewa kwanini limeandikwa hivyo
Kwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao na nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili.
2 Wakorintho 10:12
Mara nyingi tunajipia kwa kuangalia wenzetu walipo, ambavyo sio ukiangalia vidole vyako vyote vimezaliwa siku 1 lakini havilingani sio kwamba kile chembamba au kifupi ni dhaifu hapana kila mmoja amewekwa kwa wakati wake na kwa kusudi lake.
Nimejifunza hata kama mmezaliwa siku moja na mkasoma pamoja sio kwamba mnalingana kile mmoja alipotoka tumboni kwa Mungu alikuwa na kusudi lake, tafuta kujua kusudi lako hacha tabia ya kujilinganisha na watu
Wakati flani nilikuwa na hiyo changamoto ya kuangaliwa wenzangu wapo wapi? Wanafanya nini na wakati mwingine kujiona mnyonge, ila nilipomtafuta Bwana nijue kusudi langu hapa Duniani nilijifunza kumshukuru Mungu na kuwa mpole maana kila kitu Mungu kaweka kwa makusudi na kwa wakati wake