Mdogo mtu huwa anapitia misukosuko mingi ila kaka mtu kamwe hajawahi kaa pembeni. Tundu Lissu ana bahati kuwa na kaka kama Alute. Hakika Alute ni mfano wa kuigwa. Apewe tuzo ya kaka bora. Ila pia Tundu Lissu anaonyesha ana adabu kwa wakubwa zake kwenye familia ndo maana kaka yuko naye bega kwa bega kwenye majanga yake yote pamoja na kwamba wako itikadi tofauti kisiasa. Inapendeza sana.
Sisi wote tuige kina Lissu jinsi wanavyoonyesha kwa vitendo kuwa damu nzito. Usipompenda ndugu yako wa damu basi hata taifa hutaweza kulipenda. Upendo na uzalendo huanzia ngazi ya familia. Huwezi kuwa unachukiana na familia yako halafu utupende sisi wapiga kura wako. Patana kwanza na ndugu zako kabla hujaja kwetu.
Cha ziada kuhusu hawa Mughwai brothers ni kuwa inaonekana sio watu wa madili ya kihuni. Kuna mawakili wengi wa Arusha wamekumbwa na kashfa ya mambo machafu kwa mfano Mwale na Mawala ila hawa kina Mughwai hawajawahi tajwa.