Kila mtu ni mtumwa wa utamaduni wake

Kila mtu ni mtumwa wa utamaduni wake

Hapo utakuwa umerogwa
Mkuu, hilo lipo.
Unakuta mtu analipwa mshahara mdogo sana ambao unamwezesha tu kupata chakula lakini so kufanya shughuli za maendeleo.

Mtu kama huyo si rahisi aifurahie hiyo kazi, labda kama anaifanya tu kama burudani na si kujipatia kipato.

Anaweza akawa anatamani kuiacha ili akaitafute nyingine, lakini anashindwa kwa sababu zifuatazo:
1. Ana familia inayomtegemea. Kwa hiyo ingawa mshahara anaolipwa haumtimzii mahitaji yake yote muhimu, lakini anaona alau kuna unafuu maadam unamwezesha kuipatia familia yake chakula

2. Hana uhakika itamchukua muda gani kufanikiwa kupata kazi nyingine. Kwake, ndege mmoja aliye mkononi ni bora zaidi kuliko ndege mia porini. Isitoshe, anaweza akaacha kazi inayompa mshahara mdogo na bado asifanikiwe kuipata nyingine na ikamuwia vigumu kurudi alikotoka

3. Kwa sababu kama hizo 2 hapo juu, inamfanya mtu aendelee kuvumilia kwenye kazi anayolipwa mshahara mdogo ingawa anatamani angeondoka lakini anakosa ujasiri wa kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom