Kwa namna umesema ni sawa na kusema at least ukinunua gari used kwa bei ya gari mpya unakuwa umepunguza usumbufu wa kujua ubora wa gari sababu atakaelitumia na kukuuzia atakupa ushuhuda wa ubora wa hilo gari baada ya kulitumia muda mrefu sana na kulichoka kisha akakuachia kwa bei kuzidi ya soko kwa model mpya ya gari hiyo hiyo uliyonunu.
So nikuulize swali, mfano akija mtu akakuuzia iphone 7 pro max iliyotumika tena na mtumiaji zaidi ya m'moja kwa bei sawa na ya Iphone 15 pro max mpya ya dukani, utanunua na kujiona umefanya maamuzi sahihi? [emoji848]
Yaani, utasema afadhali nimenunua hii iphone 7 pro max imetumika lakini ipo vema sana na aliye tumia amenihakikishia alinunua ikiwa mpya na ameithibitisha kuwa ni original na ina guarantee ya ubora. Sipendi kununua hizi za sasa nasikia unaweza lipia bei ya juu na ukauziwa za kichina ingawa ni mpya [emoji848]
Unaweza kuwa mwendawazimu kiasi hicho kwenye matumizi ya pesa yako uliyoitolea jasho kununua kitu used na cha zamani kwa bei ya juu sawa sawa na bei ya modeli mpya ya hicho cha zamani ikiwa mpya kabisa bila kutumika popote? [emoji848]