Kila mwanaume aliyefika Mkoa wa Tabora na viunga vyake anakiri kuwa Tabora ni kiboko ya Upwiru

Sawa niliisoma story yako ya ex na kupelekewa Moto, shikamoo Tabora
 
Kuna msemo huwa unasema....

Baada ya kukaa na sisi kwa siku nzima au wiki nzima, mazuri yetu yachukue, mabaya yetu tuachie...

Wanyamwezi wanajituma kwenye shughuli za kilimo, Tabora hakuna njaa, huwezi kutqna na mnyamwezi ana kwashakoo au amedhoofu kwa kukosa chakula.

Tunaamini mtu akila akashiba kuna mawili, atakutendea mema au kutendea wengine mema, au atakugeuka atakutendea mabaya maana amepata nguvu ya kufanya ubaya au ataenda tendea wengine ubaya...

Sisi tunawakirimu watu kwa chakula wale washibe hadi wasaze, halafu hatujali malipo. Ila Mnyamwezi aliyekasirika kaa nae mbali, usijesema hukuambiwa mapema.

Tabora tunalima mahindi, maharage, viazi vitamu, karanga, ufuta na tumbaku kama mazao ya chakula na biashara.
Asali ipo ya kiasili na kurina kwa kutengeneza mizinga ya nyuki kwa ajili ya biashara.
Tuna mifugo ya kutosha, ng'ombe na mbuzi hivyo nyama na maziwa yapo tele. Tunafuga kuku wa kienyeji ni wakubwa hadi unaweza kushangaa na usiamini kama ni kuku.

Hayo ni mazuri na mema ya wanyamwezi, yachukue ukayaendeleze.

Mabaya utayokutana nayo yaache kama yalivyo, ukiyachukua sio tuu unaenda kuyasambaza na kuwaanika wanyamwezi, bali unajiharibu na wewe maana sifa/tabia ni nguo... utajikuta ili uisimulie vizuri/uisambaze itakuwa umeivaa matokeo yake unaowasimulia na kuwasambazia watakuona wewe ndio sio....

Wanyamwezi tumekaa palee....🤓.







 
kinachowaponza Wanyamwezi ni ukarimu wao tuu. [emoji39][emoji39][emoji39][emoji7]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha uongo, mkoa una wasichana wenye maumbile yanayohitaji kwenda mloganzila.
mi nakaa tabora, hakuna kitu
 
Acha uongo shangazi
 
Wanyamwezi wanajituma kwenye shughuli za kilimo, Tabora hakuna njaa, huwezi kutqna na mnyamwezi ana kwashakoo au amedhoofu kwa kukosa chakula.
Wahenga walishasema 'Mzigo mzito mpe Mnyamwezi' nimekuelewa mkuu, Ila ile story yako ya ex aliekua anakuepelekea Moto nilikuelewa zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…