Kuna msemo huwa unasema....
Baada ya kukaa na sisi kwa siku nzima au wiki nzima, mazuri yetu yachukue, mabaya yetu tuachie...
Wanyamwezi wanajituma kwenye shughuli za kilimo, Tabora hakuna njaa, huwezi kutqna na mnyamwezi ana kwashakoo au amedhoofu kwa kukosa chakula.
Tunaamini mtu akila akashiba kuna mawili, atakutendea mema au kutendea wengine mema, au atakugeuka atakutendea mabaya maana amepata nguvu ya kufanya ubaya au ataenda tendea wengine ubaya...
Sisi tunawakirimu watu kwa chakula wale washibe hadi wasaze, halafu hatujali malipo. Ila Mnyamwezi aliyekasirika kaa nae mbali, usijesema hukuambiwa mapema.
Tabora tunalima mahindi, maharage, viazi vitamu, karanga, ufuta na tumbaku kama mazao ya chakula na biashara.
Asali ipo ya kiasili na kurina kwa kutengeneza mizinga ya nyuki kwa ajili ya biashara.
Tuna mifugo ya kutosha, ng'ombe na mbuzi hivyo nyama na maziwa yapo tele. Tunafuga kuku wa kienyeji ni wakubwa hadi unaweza kushangaa na usiamini kama ni kuku.
Hayo ni mazuri na mema ya wanyamwezi, yachukue ukayaendeleze.
Mabaya utayokutana nayo yaache kama yalivyo, ukiyachukua sio tuu unaenda kuyasambaza na kuwaanika wanyamwezi, bali unajiharibu na wewe maana sifa/tabia ni nguo... utajikuta ili uisimulie vizuri/uisambaze itakuwa umeivaa matokeo yake unaowasimulia na kuwasambazia watakuona wewe ndio sio....
Wanyamwezi tumekaa palee....🤓.
View attachment 2792192
View attachment 2792193
View attachment 2792194View attachment 2792201
View attachment 2792202