(Zaburi 148:1-14),
1: Haleluya, msifuni BWANA Kutoka Mbinguni,
Msifuni katika Mahali palipo juu,
2: Msifuni, Enyi Malaika wake wote.
Msifuni, majeshi yake yote,
3: Msifuni, jua na mwezi,
Msifuni, nyota zote zenye mwanga,
4: Msifuni Enyi Mbingu za mbingu,
Nanyi maji mlioko juu ya Mbingu,
5: Na vilisifu Jina la BWANA ,Kwa maana aliamuru vikaumbwa,
6: Amevithibitisha hata milele na milele,
Ametoa amri, Wala haitapita,
7: Msifuni BWANA Kutoka nchi,
Enyi nyangumi na vilindi vyote.
8:Moto, na mvua ya mawe,theluji na MVUKE,
Upepo wa dhoruba, ulitendalo neno lake,
9: Milima na vilima vyote,
Miti yenye matunda na mierezi yote.
10: Hayawani na wanyama wafugwao,
Vitambaavyo na ndege wenye mbawa.
11: Wafalme wa Dunia na watu wote,
WAKUU, na makadhi wote wa Dunia,
12: Vijana waume, na wanawali,
Wazee na watoto,
13: Na walisifu Jina la BWANA.
Maana Jina lake pekeake limetukuka,
Adhama yake, I juu ya nchi na Mbingu,
14: Naye amewainulia watu wake pembeni,
SIFA za utakuwa wake wote,
Wana wa Israeli, watu Walio karibu naye,
Haleluya.
Amen.🙏