Ubarikiwe mwana wa Mungu.Asante Mungu kwa pumzi hii, sifa na utukufu viwe kwako ewe utatu mtakatifu, ndiwe peke yako Mungu mkuu!
Ubarikiwe mwana wa Mungu Kwa kujaliwa moyo wa IBADA na shukrani.Zaburi 150:1-6
[1]Haleluya.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake;
Msifuni katika anga la uweza wake.
[2]Msifuni kwa matendo yake makuu;
Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
[3]Msifuni kwa mvumo wa baragumu;
Msifuni kwa kinanda na kinubi;
[4]Msifuni kwa matari na kucheza;
Msifuni kwa zeze na filimbi;
[5]Msifuni kwa matoazi yaliayo;
Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
[6]Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.
Haleluya.
[emoji120][emoji120]Amen
Teh teh tehMwisho wa siku wote tunakufa, kushukuru ni wendawazimu tu!
Kwanini unashukuru wakati unajua fika hiyo pumzi ni ya kukodi lazima atakuja kuichukua tu.Salaam , Shalom!!
Hakuna Cha Bure yupo MMILIKI , mtoaji, Muumba wa vyote,
Sisi WANADAMU Kwa ujumla wetu, masikini Kwa tajiri, mgonjwa Kwa mzima, mrefu Kwa mfupi, mweupe Kwa mweusi nk nk tunavuta PUMZI ya uhai Bure kabisa.
Wema Kwa waovu, tunapata Bure PUMZI ya uhai.
Wenye dini Kwa wapagani, tunaye Mungu mmoja atupaye Pumzi ya uhai Bure.
Wote Kwa nafasi zetu, tupite katika Uzi huu kumshukuru Mungu Kwa Kila nama atakayokujalia kumsifu na kumshukuru.
Ukiquote mstari wa Neno la Mungu, ni sawa, ukiweka wimbo ni sawa, ukishukuru Kwa maneno ya kinywa chako ni sawa, na hata ukisema tu "ASANTE", yatosha.
Karibuni🙏
Ilimradi tu unavuta Pumzi ya Bure, mshukuru Mungu basi.Mkuu hili litakuwa kanisa la JF !
Tuombe,
E mola utuhurumie na utuburikie sie wana wapotevu 'Watanganyika'
Utubariki tuendelee kuwa na maarifa.
Udumu.
Ubarikiwe mwana wa Mungu aliye hai!!Ninakushukuru Mungu sababu umesema yatupasa kushukuru kwa kila jambo[emoji120]
Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Amen🙏Ilimradi tu unavuta Pumzi ya Bure, mshukuru Mungu basi.
Ubarikiwe mwana wa Mungu aliye juu,Mhubiri 9:10-11
[10]Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu/kaburini uendako wewe.
[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Amen
Tumsifu na Kumshukuru YWHN Mungu mkuu ambaye yupo kabla ya Mwanzo na ataendelea kuwepo baada ya mwisho.Salaam , Shalom!!