Kila nchi kumiliki silaha za nyuklia ndio kutazuia uvamizi na vita na kuleta heshima

Kila nchi kumiliki silaha za nyuklia ndio kutazuia uvamizi na vita na kuleta heshima

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Mpango wa Marekani kuzuia baadhi ya nchi kuwa na silaha za nuclear sio sahihi tena kipindi hii ambapo kuna kushuhudia kuongezeka kwa vita na migogoro kati ya nchi.

Kinachotakiwa sasa hivi ni kila nchi iruhusiwe kumiliki silaha za nuclear kwa ajili ya ulinzi na hii inaeweza kueleweka vyema kupitia dhana za Mutually Assured Destruction(MAD) na rational deterrence.

Ni vigumu sana nchi yenye silaha za nuclear kuvamiwa, pia ni vigumu sana kwa nchi zenye silaha za nuclear kupigana vita kati yao hali itakayopelekea kuwa na "nuclear peace".

Nuclear ndio kila kitu karne hii, kila anayetaka aruhusiwe kuwa nazo ili kuleta heshima na utulivu kote duniani.
- Nuclear Peace
 
Mataifa yanayoendeshwa na uzombi ya dini ile ya chuki chuki lazima yazuiwe.
 
Kuna changamoto nyingi sana kuwa na mabomu nyuklia, mfano namna ya kutunza chemicals zinazotengezeneza hizo nyuklia, uwezo wa kuyarusha mabomu yenyewe toka nchi na nchi, madhara ya muda mrefu kwa watu (mfano kule Japan- Hiroshima au Ukraine- chenobil), budget yake- kuyatengeza... kwetu sisi hapa labda mpaka tuombe msaada wa urusi au hisani ya Marekani, uchumi wetu ukitengemaa, madini ya urani yapo ya kumwaga, changamoto ni wataalam.

Bado sana kwa kweli nchi kukimbilia huku kutunza heshima zao. Kuna njia mbadala za kuitafuta na kuitunza heshima bila hizo nyuklia...kwa hao walizonazo, makelele ni mengi na kuzitumia hawataki. Ya nini kuwa na gari zuri halafu ulipaki tu gereji kwa kukosa mafuta? Kwanini ulihudumie wakati hulitumii? Changamoto ni nyingi ndugu yangu. Tumalizane na changamoto zetu, tuwe self sufficient- kwa mfano chakula, kudhibiti kipindupindu na mazagazaga yake. Tukimaliza hapo ndio tukimbilie huko kwenye nyuklia.

Makomandoo wetu kwa sasa waendelee tu kuvunja matofali na kubeba kilo 70 huko ngerengere na siku za kumbukumbu za Muungano- inapendeza sana wakihulumiwa sana- serikali iwaletee drones na vitu vya namna hiyo. Nyuklia hapana, bado sana.
 
Sidhani kama kila nchi ina weza kuhimili gharama za kumiliki silaha hizo.
 
Wenzetu walioahidiwa bikira saba sina uhakika kama wataitumia kwa ulinzi au kuwahi kula mizigo ya ahadi
 
Mpango wa Marekani kuzuia baadhi ya nchi kuwa na silaha za nuclear sio sahihi tena kipindi hii ambapo kuna kushuhudia kuongezeka kwa vita na migogoro kati ya nchi.

Kinachotakiwa sasa hivi ni kila nchi iruhusiwe kumiliki silaha za nuclear kwa ajili ya ulinzi. Ni vigumu sana nchi yenye silaha za nuclear kuvamiwa, pia ni vigumu sana kwa nchi zenye silaha za nuclear kupigana vita kati yao.

Nuclear ndio kila kitu karne hii, kila anayetaka aruhusiwe kuwa nazo ili kuleta heshima na utulivu kote duniani.
Watu kama iran wenye roho ya wazimu wataangamiza dunia
 
Kuwa nazo hizo Kwa Dunia ya Sasa ni changamoto,pale middle east mwenye hizo siraha wamemwahidi kuzilipua humo humo nchini mwake akizidi kukomaa.
 
Mawazo ya kitumwa ,kijinga na ya ajabu sana haya. Mawazo haya ni Kwa sababu Ukraine inatiwa adabu na Urusi.
Lakini mawazo kama haya hayakuwepo wakati panama,Vietnam,Korea,Cuba,Iraq,Somalia,Libya,Syria, Yugoslavia, Afghanistan zinapigwa na NATO.

Watu wasiojitambua Dunia nzima walishangilia kupigwa kwa nchi hizo bila kujua wanqshangilia Nini,kisa TU ni amazoea ya kuangalia sinema za Hollywood.
 
Wee mrusi fake mweusi acha ujinga
 
Back
Top Bottom