Kila nchi kumiliki silaha za nyuklia ndio kutazuia uvamizi na vita na kuleta heshima

Hilo ni balaa, vipi kama zikianguka mikononi mwa al shabab,boko haram au is.Je dunia itaendelea kuwa salama?
 
Nadhani hata Mataifa yenye nazo hayaoni faida yake! Maana wao wenyewe hawako tayari kujiangamiza!
Zile silaha wanazo ili kutishiana tu lakini siyo kuzitumia kupigana.
 
Zitadondokea mikononi mwa waasi.. Mfano wa Haiti wakateka bomu hilo kuna nini Tena au m23
 
Mwana unazungumzia silaha ya maangamizi ya karne na uchumi wenyewe huu...hauko sawa
 
Hilo ni balaa, vipi kama zikianguka mikononi mwa al shabab,boko haram au is.Je dunia itaendelea kuwa salama?
Uwepo wa hizo silaha kila nchi utawafanya watu wa mataifa yote watumie nguvu zote kuyamaliza na kuyaangamiza hayo makundi.
 
Nadhani hata Mataifa yenye nazo hayaoni faida yake! Maana wao wenyewe hawako tayari kujiangamiza!
Zile silaha wanazo ili kutishiana tu lakini siyo kuzitumia kupigana.
Na kila taifa likiwa nazo hakuna atakayethubutu kumgusa mwenzake.
 
Zitadondokea mikononi mwa waasi.. Mfano wa Haiti wakateka bomu hilo kuna nini Tena au m23
Hao waasi wa M23 na Haiti wakijua wengine pia wanazo hizo silaha tena nyingi na kubwa kuliko wao ni vigumu kwao kufanya chochote.
 
Wao hawakai sehemu moja wanaweza kutawanyika
 
Uwepo wa hizo silaha kila nchi utawafanya watu wa mataifa yote watumie nguvu zote kuyamaliza na kuyaangamiza hayo makundi.
sio kweli, hizo ni ndoto za mchana kweupe.kila nchi ikiruhusiwa kumiliki nukes basi itakuwa rahisi kwa vikundi vya kigaidi kuzipata na kushambulia maasimu wao
 
Kila nchi ikiwa na nuclear za kutosha hakuna atakayemtwanga mwenzake.
Kabisa mkuu. Maana hata Russia alishawishi USA ufaransa na uingereza kumuomba ukraine angamize silaha zake za nyuklia na alipoziangamiza kavamiwa
 
Back
Top Bottom