Kila ndoto ina sababu na kusudi, usije ukapuuza ndoto yako hata moja

Kila ndoto ina sababu na kusudi, usije ukapuuza ndoto yako hata moja

Niliota watu wawili kazini wananifukuza nitoke mahala nilipo nirudi nyumbani kwetu mkoa B

Nini hii?
Mkuu omba Sana , yaan katika ulimwengu wa roho Kuna vita inaendelea kazini kwako, so yakupasa uombe Sana uvunje hizo roho zinazofanyanvita na wewe. Ofisini kwako Kuna watu wanataka ufukuzwe , Ili wakalie nafasi yako so usipoomba itakuwa kweli, hivyo kazana kuomba.
 
Habari, mkuu ukiota wewe na mkeo mmepata mapacha wawili wa kike, ila kwenye ndoto hawaji kama wachanga ila wanaonekana kama watoto wadogo wa miezi kadhaa au mwaka.
Kuota mmejifungua ni baraka , ambayo itawwjia kwa haraka Sana , yawezekana mtaanzisha biashara au whatever ambayo itakuwa kwa haraka saana
 
Wewe usinidanganye. Kwa zaidi ya muaka kumi naota naokota hela na haijwahi kutokea naokota hela kama kwenye hizo ndoto.
Hii ndoto inategemea ulikuwa unaokota pesa za aina gani, noti au sarafu, au pesa za kigeni, .ukiota unaokota au unapewa au unaokota pesa za kigeni zenye thamani au noti, wewe utafanikiwa Sana maisha I kwako but ukiota unaokota coin au unapewa ni roho ya umaskini inakufatilia.
 
Ninaomba tafsiri ya ndoto hii.

Tulikua tunakunywa chai na ndugu zangu akiwemo mama yangu..pembeni kuna kitu kama gogo hivi..sasa akaja ndugu yangu akalishika lile gogo.Kumbe ni Joka kubwa mno..lilivyoamka tukakimbia..ila likamvingirisha mama pale..hapo hapo nikastuka.

Msaada please nmeota leo leo hii.
 
Ninaomba tafsiri ya ndoto hii.

Tulikua tunakunywa chai na ndugu zangu akiwemo mama yangu..pembeni kuna kitu kama gogo hivi..sasa akaja ndugu yangu akalishika lile gogo.Kumbe ni Joka kubwa mno..lilivyoamka tukakimbia..ila likamvingirisha mama pale..hapo hapo nikastuka.

Msaada please nmeota leo leo hii.
Hiyo haiitaji nguvu kubwa kutafsiri. Hapo maana yake ni kwamba "mbaya wenu hatoki mbali, mpo nae around anawazoom tu mnapofanya mambo yenu"
 
Ndoto hii inaashiria kwamba Unamumiza mtoto wako wa Ndani kihisia, anaweza kuwa mtoto wako au unaye ishi nae humtendei vyema, kwa kukandamiza hisia zake zote au kutokumruhusu hali ya kujitokeza na kucheza nje, Kumkosoa, kumuadhibu. Pia huashiria Mzazi wa Ndani ni mkali kutokana na dini yake, malezi ya familia, mawazo ya dhambi n.k) Sio ndoto nzuri, inaweza kuhusiana na unyogovu au uharibifu wa kihisia, Ikiwa ndoto inajirudia au unahisi huzuni sana - tafadhali tafuta usaidizi. Ikiwa hayo hauyatendi kwa mtoto.
Uongo hiyo ni ishara ya yeye kusaidiwa na mitambiko yao dhidi ya maadui
 
Bado najiuliza sana tafsiri za ndoto huendana na dini au imani flani?? Maana ukifuatilia tafsiri ya ndoto kwa waislam ni tofauti kidgo na tafsiri ya wakrito ndoto inaweza kuwa ile ile ..... mfano kuota una paa ....ila naendelea kujifunza nipo darasani na walimu wangu ni nyie
 
Kuota unapita Barabarani mtu anakustua nyoka huyo ,unaangalia humwoni kunakuwa na kigizagiza anaendelea kukusisitiza huyo nyoka
Unaendelea kutizama kwa mkakini,mbele unaona nyoka wengi na Hatari ila wamejeruhiwa vibaya wapo katikati ya Barabara,mmoja wa wale nyoka akajitutumua kutaka kuondoka nikampiga na fimbo nikaona haina madhara kwake ndio nikiona jiwe kubwa nikanyanyua kumpiga nalo hapo anapata madhara anapasuka
Nini maana yake?
 
Back
Top Bottom