Kila nikikumbuka kuwa nilisema "Sitafanya kazi chini ya laki 3" baada ya kumaliza University

Kila nikikumbuka kuwa nilisema "Sitafanya kazi chini ya laki 3" baada ya kumaliza University

Watoto wa 90 ambao bado hatujatoboa,na maisha yametupiga.braza anatusalimia🤣🤣🤣🤣
 

Attachments

  • download (1).jpeg
    download (1).jpeg
    6.9 KB · Views: 3
Umezungumzia kuhusu ndumba that is real ?

Ukitangaza unafukuzia mchongo basi huo mchongo haufanikiwi.
Uchawi upo mkuu, na nilikuwa nasoma kitab flani hiv experience ya South Africa jamaa anaargue kuwa umefungana sana na dhana ya HUSDA (envy), husda sio jealousy. Husda ni kijicho yani ulichonacho ukikose hata kama yule anyetaka ukose hawez kukipata

Kwa muktadha huu uchawi umegandamana na "kupinga maendeleo", so uchawi hauwez kuutenganisha na umaskini. Uchawi hauwez kuutenganisha na kukwama kwenye jitihada zote za kuuondoa umaskin na wachawi wenyewe ni maskin ambao hawana suluhu la kutoka hapo. Ni watu dhaifu kwa macho ya nyama, dhaifu kwa mali, mawazo lakin very strong spiritually. Wakisema utaona au fanya kitu hiki tuone kama utaweza ujue hapo safari yako ndefu.

UcHawi upo, mzungu mwenyew shughuli yake anaujua. Mana umefungamana sana na elimu ya nyota au unajimu, elimu ya mitishamba na traditional healing. Mzungu kauelezea sana kwenye vitabu vya mapinduz ya maarifa (renaissance period)
 
Sasa hivi natamani nipate ata kazi ambayo nitalipwa ata laki na nusu ila sipati

Kweli MAISHA yana ramani na aliyemchorea masikini pen ili mgomea njiani

Napata makapi vinono navitamani
View attachment 3051725
Yatapita, sisi wenyewe wakati tunakaribia kumaliza tulikuwa tumekaa tunajisema. Nakumbuka nikasema bila milioni 3 mimi sifanyi kazi. Baada ya hapo sasa....
Lakini yote kheri walau sasa hivi ninazitengeneza nje ya ajira rasmi.
 
Back
Top Bottom