Kila nikiwatazama baadhi ya Wachezaji wa Yanga SC, naamini kweli mpira ni connection hata kama kiwango kimeisha

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
11,297
Reaction score
14,588
Ukweli usemwe mpira Wetu Huu bado ni ungaunga mwana hata kama huna Kiwango (Kiwango kimeisha) Lakini ukiwajulia tu Viongozi basi unakula vizuri klabuni kwa Mshahara mnono na Kiwango huna.

Ndiyoooo!! Huu ni ukweli Mchungu kabisa tena kweli ambao ukiumeza Lazima uombe sukari ama asali ili upoze machungu.

Sasa Wachezaji Hawa Wana Kiwango gani Yanga SC?!!

(1) Jonas Mkude , huyu alisajiliwa kwa mbwembwe Nyingi Lakini Kiwango Hana na tuliambiwa Kuwa kala mkataba Wa mwaka mmoja Lakini Mpaka Sasa mwamba anadunda tu anakula mafao yake na hakuna Wa kumgusa, hata mechi hachezi yupo Pale Yanga SC kama mtalii tu.

(2) Chota Chama, huyu alisajiliwa kwa Sababu ya siasa za mpira pale karikao Lakini kiuhalisia hakustahili kabisa kuja Yanga SC, kuna za ndaniiiiii kabisa huyu alisajiliwa tu ili kuwachoma mioyo Mashabiki Wa Simba SC Lakini kiuhalisia Kiwango kimeshuka


Maoni yangu: Yanga SC waache Kusajili kwa kuwakomoa watani Wao Wa jadi (Simba SC) Bali wazingatie matakwa ya kocha na siyo mihemko mwisho Wa siku Wachezaji wanakaa benchi na Kua kama wataliii.
 
Cha muhimu tumeikomoa Simba...
 
Wajinga ndiyo waliwao
 
Sijaona mechi ambayo Mkude kapangwa akacheza chini ya kiwango. Zile mechi na Memelody Aucho akiwa majeruhi Mkude alipiga mpira mkubwa sana.Yanga imesajili wachezaji wenye viwango karibia vinalingana, chaguo la mwalimu ndio hoja iko hapo. Hata akina Kibwana wakipewa number hukiwasha vizuri tu.
 
Nikupe connection ukachezee mwananchi?
 
K
Kuna tofauti gani na Mavambo, Manual nk
 
Hajui mpira huyoo anafanya siasa tuu.
 
Chakuongezea kabisa yanga pamoja na Hilo hawakimbii mechi kisa Kuna wachezaji 4 kati ya 28 majeruhi.
 
Bila kusahau hivi baleke mlimsajiri kisa mnataka kushitakiwa cas au?
 
Juzi nilimuangalia nahodha wa Yanga Bakary Mwamnyeto anavyokimbizwa na watoto wa Songea United, nikasema kweli kazi ipo.
 
Nyinyi huwa mnaangaliaje mpira? Chama ameisha! Eti Mkude kafanyaje? Hawa hawapati tu nafasi ya kucheza ila kiuhalisia bado ni wachezaji wazuri sana basi tu hawajaingia kwenye machaguo ya kocha. Bado nina imani na Mkude na Chama
 
Unamzungumzia Chama yupi, hebu msome huyu. Siku nyingine leta facts humu siyo Facebook unaleta mihemko badala ya facts: Chama aanza na Rekodi hizi Ligi ya Mabingwa, Takwimu za Chama Yanga zaanza kutisha Ligi ya Mabingwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…