Kila nikizunguka Tanzania naiona legacy ya hayati Magufuli ambayo haitafutika kirahisi

Kila nikizunguka Tanzania naiona legacy ya hayati Magufuli ambayo haitafutika kirahisi

Nikitembea kwenye barabara za lami ambazo alizisimamia kwa zaidi ya miaka 20 na kurahisisha usafiri hapa nchini naona hayati alilitendea jema taifa letu.

Vipi kuhusu Mfugale Flyover na Kijazi interchange!

Leo hii Kibaha mpaka Mbezi foleni ni story iliyosahaulika.

Stand ya kisasa ya ya Magufuli bus terminal, Dodoma na miji mingine ni mifano ya kumkumbuka.

Nikiongelea manunuzi ya ndege watu wataponda,lakini alithubutu kununua cash.

Jambo kubwa ni kudiversify maendeleo, hili hatasahaulika maana kila kona ya Tanzania ilipata maendeleo.
Hakuna la ajabu; aliomba kura ili awatumikie wananchi.
 
Kwanini hao kina mama hawakuenda kulala chini viwanja vya jangwani au biafra wameenda kulala Muhimbili? Na kwanini hivyo vitanda visingepelekwa viwanja vya mnazi mmoja au sabasaba? Je aliyepeleka vitanda vya milioni na aliyejenga jengo la mabilioni nani kafanya jambo kubwa?

Hii ni mifano inayoainisha kwamba uongozi ni mwendelezo, hatua yoyote ya muendelezo inayofanywa na mwingine si ya kusifiwa kuliko mwingine. Kila mmoja namefanya kea hatua yake kadri ya uwezo ulivyoruhusu na changamoto za wakati huo.

Ni Watanzania tu ndio Wana akili za panzi kwa kiwango cha kutosha. Vipi ukamuone wa maana kuliko wote aliyejenga kilomita 20 za lami yombo au buza halafu umuone si wa maana aliyejenga barabara kutoka mwanza hadi Dar? Maisha ni kuendeleza kea njia bora zaidi pale palipoanzwa na aliyetangulia.
Sina ubishi na hili...Naamini kama wewe...
 
Back
Top Bottom