Kila Rais wa Tanzania alipoondoka aliacha nini kwa awamu iliyomfatia?

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Kichwa cha habari kimeeleweka.

Kwa faida ya wengi, waliokuwepo na wasiokuwepo awamu zilizopita. kila mmoja wetu ana mtazamo wake tofauti na wa mwengine, tujadili mafanikio na madudu ya awamu zilizopita.

Binafsi nashukuru, nimeziishi awamu kadhaa za Tanganyika kuanzia tupo utawala wa Muingereza chini ya Umoja wa Mataifa.

Naikumbuka Tanganyika ya Muingereza kwa mbali, naikumbuka Tanganyika ya utawala wa Nyerere kwa ukaribu zaidi.

Kwa kuwa viongozi waliotuongoza ni wanaadam kama sisi, hawakosi mema yao na mapungufu yao, tuyajadili waliotuwachia.

Hata kama hukuwepo na umeyasoma au umehadithiwa tu, rukhsa kuyaleta ili tuchekeche na tuchambuwe mchele, chenga na chuya.

Bila kufahamu wapi tulipotoka na wapi tupo itakuwa vigumu kuelewa wapi tunaelekea.

Tujadili.
 
Madeni
 
Nyerere katuachia nchi iliyoyumba kiuchumi japo alianzisha miradi mingi ya maendeleo wakati wake, Mwinyi katuachia kashfa ya Loliondo na IPTL, Mkapa katuachia kashfa ya kugawa mali za taifa, Kikwete kashfa ya richmond na mapesa ya escrow, Magufuli katuhumiwa kujali maendeleo ya vitu kuliko watu, (sijui hivyo vitu viliwalenga wanyama!)

Awamu iliyopo naona imeamua kufuata nyayo za Mkapa kwa umakini.
 
Nyerere==aliacha kila kitu kikiwa intact, alipambana na umaskini na hakuumaliza
Mwinyi===aliacha kila kitu kikiwa intact, alipambana na umaskini na hakuumaliza
Mkapa===aliuza kila kitu zikiwemo rasilimali; alitujengea uwanja wa mpira
Kikwete===alipambana na umaskini na hakuumaliza, alituachia vyuo vikuu vipya zaidi ya 40 na shule nyingi mpya za Sekondari za nyongeza
...................
etc
 
Back
Top Bottom